Serikali huwa haishindi kesi kwasababu huwa inaendeshwa na emotion badala ya facts, Inaonekana hapa ofisi ya mwanansheria mkuu haikumshauri DPP vizuri na hii ni upotezaji wa muda kwa kumshataki mtu kwa hisia badala ya vidhibiti.
haki imetendeka at last,kwenye dunia hii iliyojaa waongo,mabazazi,mahayawani,waliokosa utu,mkweli siku zote ataonekana adui,na inahitaji ujasiri wa ziada kuwa mtu huyo,shall truth only set us free!
hakimu waliarwande lema wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, hivi punde amewaachiwa huru, mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, absalom kibanda na mjumbe wa bodi ya jukwaa hilo, theophil makunda katika kesi ya jinai ya uchochezi iliyokuwa inawakabil.
Katika kesi hiyo pia salmson mwigamba alikuwa anashtakiwa kwa makala aliyoandika kwenye gazeti la tanzania daima, yenye kichwa cha habari "waraka maalumu kwa askari wote" iliyotafsiriwa kuwa ilikuwa ya kuwachochea wanajeshi.
Wakati huo, kibanda alikuwa mhariri mtendaji wa tanzania daima na makunda alikuwa kaimu mkurugenzi mtendaji wa mwananchi communications ltd iliyochapisha gazeti hili.
Hakimu amesema walishtakiwa kwa hisia, na kwamba hisia haziwezi kuwa na mashiko hataka kama zina nguvu kiasi gani.
Mkuu righteye, usiwe na mhemko wa kisiasa unaokosa weledi wa kuchuja mambo. Kesi iliyokuwa inamkabili Samson Mwigamba ni ya kuandika makala iliyokuwa inadaiwa na Jamhuri kuwa ni ya kichochezi. Kesi hiyo ndiyo imekwisha leo na Samson Mwigamba ameonekana hana hatia na Mahakama.
Hilo suala la uhaini pia ni kama mmelishwa -----. Uhaini (treason) ni kosa linalofanywa tu dhidi ya dola (state). You can not commit treason against a political party. Tafuta kesi ya Hamis Ali Machano na wenzake dhidi ya Jamhuri ambapo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilisema wazi kuwa uhaini ni kosa ambalo hufanywa dhidi ya dola na kwa kuwa Zanzibar haikuwa dola basi uhaini usingeweza kufanywa na wakata rufaa huko Zanzibar.
Msomi mwenzagu Tundu Antipas Mughwa Lissu alipotoka kimantiki na kisheria alipokuwa akiutangazia umma kuwa Samson Mwigamba na Kitila Mkumbo ni wahaini. I repeat, you can not commit treason against a political party, never!!!
Na Kibanda kuhamia magazeti ya magamba..Kesi hii ndiyo iliyotengeneza nafasi ya CCMagamba, kumtishia na kumshawishi Migamba aisaliti CHADEMA.