Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Unataka hoja au matusi?nadhani unanijua kwamba vyote naviweza,sema leo sitaki kusema ovyo,ni hivi bwana mdogo,waulize hata members wa cc ya ccm kama wapo unaiowajua waliokuwepo kinana akiwemo watakueleza misimamo yake huko kamatini,sema alwayz maamuzi ya kikao yanatizama wingi wa wajumbe waliounga mkono jambo fulani so yeye kama yeye hata kama angependa mwisho wa siku kikao kinatoka na maamuzi ya pamoja,huo ndio utaratibu wa vikao kijana,na hii ni popote hata huko chadema kata uliko.

Lakini ukweli jamaa ni strategist mkali sana. alikuwa military strategist na sasa ndani ya ccm itakuwa balaa. kwa kuwa walimuomba akubali hiyo nafasi atataka kuwaonesha kwamba hawakukosea,huo ndio ukweli hata kama hatuupendi sana,alichofanya kibanda ni kuuamsha upinzani uje na mbinu mbadala kwa kuwa jamaa si wa katibu wa kawaida kama wawili waliopita na kumbuka sasa atafanya kazi na mzee mangula ambae nae si mtu wa mizaha wala kuchekeshana kama mzee makamba

Kuhusu alifanya nini kwenye kamati kuu,ni pamoja na kupambana vikali namafisadi kumhami spika sitta asifukuzwe uanachama ccm na kuvuliwa uspika,yeye alijenga hoja juu ya hoja kamati kuu nzima kimya na akawaambia wazi mnataka kumfukuza spika kafanya kosa wakati yeye anafanya kazi yake na kiukweli anatusaidia sana angalau kuonekana kwamba bado kuna watu ambao hawako karibu wala hawaungi mkono jambo la ufisadi ambalo wapinzani wamelishikia bango na kuungwa mkono na wananchi,baada ya hoja zae ndipo kamati ikiongozwa na mzee mwinyi na yeye kinana ikaundwa na jk
 


Sasa yeye Kinana ana prefer nani awe Rais?
January?
 
Umeshachanganyikiwa sasa unaanza kuuliza matusi, kwani hapa ni Blogu yenu na mpuuzi mwenzako Mange Kimambi ambao midomo yenu ni kama makalo ya vyoo na hamjisikii raha bila kutukana? nioneshe ni wapi kwenye bandiko langu ni wapi kuna matusi?

Ceteri Palibus, Kinana kwangu ni Msomali tu na ni Fisadi sawa na mafisadi wengine, na kwenye medani za kivita mimi natambuwa Jenerali Sarakikya pekee kwa upande wa Arusha, sasa ni wakati muhafaka kwa Bashe kuongeza speed ya biashara yake ya meno ya Tembo maana King maker Msomali mwenzake yupo in collaboration with Prince Ridhiwani.
 
Najua hunaga hoja alwayz zaidi ya matusi,so kabla ya kuanza mjadala na wewe mtu inabidi achukue tahadhari maana hawezi jua kama uko kwenye siku zako au uko poa kwa wakati husika,anywayz nimefurahi kujua kama na wewe ni member wa ile blog ya dubai iliyohamishia makao makuu yake miami na huwa unaenda kuangalia hayo matusi.
 
Sasa yeye Kinana ana prefer nani awe Rais?
January?

Jnauari a.k.a. mzee wa bajaji!! no way,kinana hana mtu personal but as i said jamaa ni strategist mkali sana na amekwenda pale kuisaidia ccm kurejesha heshima na hatimae kutumia uwezo wake kwa kushirikiana na wenzake pale kuipatia ccm mgombea bora wa urais ambae hana doa na wala hatoki kwenye makundi hasimu ya wataka urais,lengo ni kuwa na mgombea atakaeunganisha chama,hawa wataka urais watazidi kuleta mgawanyiko utakaokipasua chama kama wataachwa na mmoja wao kushinda
 


Basi kama ndo hivyo Migiro ataweza kuwa na nafasi au unaonaje?
 
Nina hamu sana siku moja kwa kuwa sasa makamba ambae alikataza debate hayupo paandaliwe debate between slaa na kinana,nadhani wengi ndio mtapata fursa ya kumjua yule msomali kwa upande tu wa jinsi alivyokua na uwezo mkubwa wa kujenga hoja,the guy is a good speaker na kila mtu atampenda,he's like obama kwenye suala la kujenga hoja na pia ana upeo mkubwa sana katika mambo mengi
 
Sina huo muda, nyinyi ndio mnatufataga wenyewe huku JF na picha zenu za Bikini ushuzi ukidhani huku watu tunaentertain mambo ya kipuuzi.

Hivi Blog nayo siku hizi ina makao makuu? kwani kuwa na blog si ni laptop, modem na digitital Camera tu? au ndio maana Wakurugenzi wengi siku hizi maana mtaanza hadi kujiita wakurugenzi wa blogu.
 
Basi kama ndo hivyo Migiro ataweza kuwa na nafasi au unaonaje?

Aaah boss i can't predict kuna determinant nyingi kumpata rais,jk 2005 ndani ya sekretariet alikua na mtu mmoja tu marehemu mama salome mbatia,lakini katibu mkuu mzee mangula,mapuri,msome na wengine hawakua wake lakini bado haikutosha kumzuia
 
Aaah boss i can't predict kuna determinant nyingi kumpata rais,jk 2005 ndani ya sekretariet alikua na mtu mmoja tu marehemu mama salome mbatia,lakini katibu mkuu mzee mangula,mapuri,msome na wengine hawakua wake lakini bado haikutosha kumzuia


But naona January anaweza 'kupata bahati'...
sababu hana maadui wengi...
na baba yake now ni very popoular na anamdai Kikwete hisani ya kumsaidia kumdhibiti Lowassa
mkutano uliopita.....njia ni nyeupe kwa January..unaonaje?
 
Nimeiona hii "this is just the begining utajuta uliandika makala hii!"
 
Last edited by a moderator:

Naona unazidi kupotea njia kuelekea porini mpaka umesahau kinachojadiliwa,rudi kwenye hoja acha vioja kama huna hoja piga kimya,then endelea kushiriki mjadala kwa njia ya kusoma,jf haina mwenye sema nimewahi kushauri tu ili kuepuka kuwa na watu wenye upeo mdogo(wewe si mmoja wao)pengine kungekua na utaratibu wa kujadili maombi ya waombaji uanachama kuona kama yanakidhi standards za jf kabla ya mtu kupewa hiyo membership,hili lingetusadia sana kupunguza idadi ya members wasumbufu,wakorofi,wasio na hoja pamoja na wahuni.
 
But naona January anaweza 'kupata bahati'...
sababu hana maadui wengi...
na baba yake now ni very popoular na anamdai Kikwete hisani ya kumsaidia kumdhibiti Lowassa
mkutano uliopita.....njia ni nyeupe kwa January..unaonaje?
The Boss Lowasa haamini katika bahati bali mikakati tu, ni afya peke yake ndio inayoweza kuwa kikwazo cha kuwa Nomineted ndani ya CCM For Presidency.

Ondowa mawazo yako kuhusu January, Tanzania si nchi ya kufanya majaribio ya Urais, kosa hili bado tunatumikia adhabu yake halafu wewe unakuja na same idea? hili ni kwa pande zote CCM na Chadema, 2105 hatuhitaji wagombea Urais wa majaribio bali tunahitaji mtu commited. January he need to grown up kwanza the same to Zitto Kabwe.
 


Wewe naona hunielewi kabisa
mimi sijasema January anafaa au namuunga mkono
hapa namuuliza Kim sababu Kim huwa anakuwa na inside info za ccm

Namuuliza kuhusu January sababu January na yeye anataka kuwa Rais
weather anafaa au hafai sio swali hapa....
hapa swali ni ndani ya CCM wanasemaje?
 
But naona January anaweza 'kupata bahati'...
sababu hana maadui wengi...
na baba yake now ni very popoular na anamdai Kikwete hisani ya kumsaidia kumdhibiti Lowassa
mkutano uliopita.....njia ni nyeupe kwa January..unaonaje?

sidhani kama anatosha kwa nafasi hiyo kwa sasa,maadui anao wa kutosha pia,mtu kama ngeleja,ridhiwani na wengine wengi hawamtazami vizuri,sem dogo mjanja mjanja sana,kajichomeka kwenye makundi yote,kwa lowassa yuko,kwa jk yuko kwa membe si sana lakini yupo yupo kimtindo,mpango wake yeye sio sasa bali baada ya rais ajae kupita,anachotaka ni kuwa na nafasi na sauti kwenye serikali ya rais ajaye,ushawishi wa babake ndio ulimsaidia juzi kushika nafasi ya pili nyuma ya tyson kwenye uchaguzi wa nec viti 10 vya bara a.k.a. kapu.
 
Boss huyu dogo mimi huwa simuelewi yuko upande gani,kuna saa unaweza kudhani ni shabiki wa chadema na slaa lakini wakati mungine unamuona anacheza ngoma ya lowassa ila huwa hana hoja siku zote,watu wa aina yake ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu,ni wa kuogopwa kama ukoma kwa kuwa ni wachochezi wa kawaida tu
 

Heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hebu nisaidieni,hivi Gazeti la Tanzania ni la CAHDEMA?????samahani jamani hii kitu imenistua sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hebu nisaidieni,hivi Gazeti la Tanzania ni la CAHDEMA?????samahani jamani hii kitu imenistua sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hueleweki hata unataka kusema nini zaidi ya kujamba mashuzi tu hapa.
 
Kupita pale Lumumba na kupiga soga Falcon Restaurant wala siyo kuwa Insider, ni watu wanaosikiliza porojo tu za vijiweni, kiukweli swala la mgombea Urais kwa CMM mpaka sasa hivi ni mtihani, ila upepo utakapovuma au kubadilika ndio utaonesha mwelekeo.

January bado sana kwenye fitina za kugombea Urais, nadhani haya ndio madhara anayotuachia JK sasa Urais umeonekana ni Urahisi kweli ndio maana kila mtu anadhani anaweza kuwa Rais.
 
Nadhani A. Kibanda ako na tatizo kubwa sasa na sioni tiba ya haraka kuponya kansa anayotaka kuipanda miongozi mwa Watanzania. Sina hofu na utashi wake pamoja na akili zake kama anamuona Kinana ni bora hiyo ni shauri yake. Mashaka makubwa naanza kuyapata pale ambapo anaanza kwa kishindo kusema hoja za ufisadi ambazo zinatolewa na makundi mbalimbali kumhusu Kinana eti ni hoja nyepesi na hazina mshiko, eh Mola wangu hawa ndio watanzania tulionao eti nae ni mhariri wa chombo fulani? Kwa kazi yake na wadhifa alionao ni budi akatanguliza kuwa na 'HAYA' angalau kidogo na ni 'haya' tu ndio itakunyima uhuru usio kifani kwa kuogopa kuingilia uhuru wa wengine. Maoni binafsi ni haki ya msingi ya mtoa maoni lakini pale ambapo unatoa maoni kuhusu ukweli uliyopo ni budi kuzingatia kuwa maoni yako hayawapi nafasi watu wengine kutambua kuwa wewe ni bomba tu la kupitia sauti lakini anaetoa sauti eti yupo kilomita 2000. Ndivyo wengi wa watoa maoni katika thread hii wanavyomfananisha A. Kibanda katika makala hii. Mwenyezi Mungu amsaidia na kumrudishia weledi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…