DDODMA.
KAMBI ya Upinzani Bungeni imetoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ikidai kuwa anajihusisha na mtandao wa ujangili nchini.
Hii makala ni ya mwaka gani kwani? Any way huu ni muda wa vitendo si porojo; Yu wapi Mzee Mangula? Sio yule ambaye juzi tu alikuwa akihojiwa pamoja na Dr.Slaa kwenye kipindi cha uzalendo huku akionekana kutetemeka wakati wote?kuhusu kinana! Tunamzungumzia Kinana huyu huyu ambaye jana kawaambia wananchi kwamba wasitaraji kama katiba mpya itawapa maendeleo; hata watu wakajiuliza kama kinana anafahamu maana ya maendeleo katika upana wake? Au Kinana yupi mnayemzungumzia!
Ni Kinana huyo unayesema ni makini ndiye aliyeiuwa CCM Morogoro, baada ya ziara ya mkoa wa Morogoro ambapo Kinana na wapambe wake walikuwa wanazomewan kila wanapoenda, hasa milaya ya Ifakara Kinana alizomewa kaiasi alitaka kurusha ngumi , ni hapo Ifakara wateule wa CDM walipoenda walikusanya kadi CCM yapata 3,000 wakazikoka moto. Wewe kibanda umesahau hili?
Kila siku tunapiga kelele humu ndani tukisema fanyeni jambo la kwanza kwanza (First thing First) tunaambulia kuitwa magamba! CCM haijawahi kushinda uchaguzi eti kwa kuwa ina wagombea wazuri au ina sera nzuri. CCM hushinda kwa kuwa ina mikakati timilifu, basi!!