Nimeifuatilia sana mada kwa kusoma mawazo ya watu bila kuchangia. Na hapa sitachangia bali nitaendelea kusoma mawazo ya watu.
Kuna huu mchango wa mwandishi nguli ninaye mheshimu sana (Richard Mgamba) mshindi wa tuzo za CCN.
Amechangia haya kwenye makala hii kwenye moja ya mitandao kuhusu makala ya Kibanda.
"Wasifu mzito na historia za kutukuka? Ninaheshimu sana mawazo ya Kibanda lakini nashindwa kujizuia kuhoji baadhi ya sifa alizotoa kwa hao anaowaita wateule. Kwanza ni kweli CCM imefanya ilichokifanya, lakini kinachotia shaka ni sifa wanazopewa hawa watu.
Mathalan, Kinana amekuwa Waziri wa Ulinzi, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, na hatimaye akawa kampeni Meneja wa Mkapa na Kikwetesijui katika kipindi hicho alilifanyia taifa hili kitu ghani cha kutufanya tuseme ana wasifu mzito na historia iliyotukuka. Kampuni ya kinana na wenzake hawajalipa mabilioni waliyochota NSSF kwenda kujenga kiwanda cha madawa mikochenina mradi ukafa mpaka leo. Hizi siyo fedha za serikali, ni fedha zetu sisi watanzania wafanyakazi. Kamuulizeni, akikana mnione.
Pili, Philip Mangula alikuwa katibu mkuu kwa miaka kama kumi hivi wakati wa Mkapa, na akatuhumiwa na wana-mtandao hawa hawa kwamba alihongwa na kundi la Sumaye ili kumuhujumu JK katika mchakato wa 2005. Siyo hilo tu wakati wa kuchotwa kwa mabilioni ya EPA pale benki kuu upo ushahidi mkubwa kwamba alihusika kutoa recommendations kwa baadhi ya wachotaji kwa sharti la kwamba asilimia fulani inakwenda katika chama.
Ushahidi upo na kama mnabisha katafuteni maelezo ya wakili Maregesi katika tume ya kuchunguza ufisadi huu, na pia ya kwake yeye Mwenyewe Mangula mbele ya tume.
Zakhia Meghji ndiye mliyemshambulia hapa katika vyombo vya habari kwamba hafai kuwa waziri eti kwa sababu ni fisadi tangu akiwa mali asili na hatimaye wizara ya fedha. Au mnataka kutuambia kwamba zile kashfa zilikuwa za kutunga ili hatimaye wateule wenu waingie katika baraza la mawaziri?
Mwigulu Nchemba naye anayo historia iliyotukuka ambayo iliandikwa lini na wapi?
Napata shida sana kuona tunakuwa wepesi wa kutoa sifa badala ya kusubiri kuona utendaji wa wahusika hawa. Mangula alipogombea uenyekiti wa CCM akapigwa chini akalalama kama Sumaye na kusema uongozi ndani ya chama umekuwa ni wa kulangua kama bidhaa, lakini leo amerejea katika nafasi ya juu kwenye Chama ambacho uongozi unauzwa kama bidhaa.
Kwa kifupi, hawa jamaa ni wale wale waliokuwepo juzi, jana, na leohivyo kuwapa sifa kibao ni ushabiki usio na kifani. Tusubiri tuone makeke haya ya kuanza kwa mbwembwena hii ni kawaida ya CCM, maana hata 2006 walianza kwa kutembelea masoko yetu, kukagua madaraja, na sifa kibao, lakini leo, hali imegeuka. Kazi ipo".