Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Msemaji maarufu wa kikosi cha kivita cha Hamas ambaye kwa takriban mwezi mzima uliopita hakusikika akitoa takwimu za uwanja wa mapigano,leo amesema mateka 9 wanaowashikilia wamekufa kutokana na mashambulio ya jeshi la Israel huko kusini ya Gaza.
Kwa idadi hiyo,Abu Ubaida amesema jumla ya mateka waliokuwa wakiwashikilia ambao wamekufa imefikia 70.
Abu Ubaida ameeleza hayo kupitia chaneli yao ya telegramu ambayo imekuwa ikitoa matangazo kila siku kutoka Gaza tangu vita vianze hapo mwishoni mwa mwaka jana.
Matangazo hayo huwa yanaendelea hata umeme ukiwa umezimwa na mawasialano ya intaneti kukosekana eneo hilo.
Kurudi kwa Abu Ubaida kunapingana na matangazo ya awali ya Mosad yaliyoashiria kifo cha kiongozi huyo wa Hamas.