Hii topic ina mambo mengi sana my dia
Yaani ni kama umekusanya mafaili ya ofisi tatu za Mamlaka za Kodi nchi za USA, China na Brazil halafu umeweka ktk kajidude kamoja kadogo (flash)
Kwanza naomba nikurekebishe kwamba
Sexual Abuse tunatafsiri kwa kiswahili kama
Unyanyasaji wa Kijinsia
Naomba sasa nielezee kisa kimoja cha
Unyanyasaji wa Kijinsia.
Kuna mdada ana mtoto mmja ameolewa, ana miaka minne katika ndoa yake, alizaliwa miaka 24 iliyopita.
Yeye na mume wake walikua wana pendana sana na mpaka sasa mdada anasema bado anampenda tena sana mume wake.
Ananiambia, " Yaani CPU, siku hizi mume wangu kabadilika sana kiasi najuta hata kuolewa yaani kidogo kanitukana mara mshenzi mara mjinga mara ananitisha kunipiga kwa kusema mimi simjui vizuri ndio maana nashindwa kufanya atakavyo.
Ukweli ninachanganyikiwa mume wangu anakuwa kigeugeu anaweza akakwambia "mimi sipendi uvae nguo ndefu", ukivaa fupi kwa muda huo aliosema anafurahi sasa itokee siku nyingine akuambie tutoke ukivaa hiyo nguo fupi anaanza
" . . . . unaenda kumuonyesha nani? Unatakautongozwe kwani mimi sikutoshi? "
Ukivaa ndefu au suruali ananyamaza.
Juzi simu yangu ilijizima nikiwa salon iliyo nje ya uzio wa nyumba tunayo ishi. Akampigia rafiki yake akaja mpaka saloon nikaongea naye kupitia simu ya rafiki yake. Jamani hakutaka kukata simu mpaka muda wa kazi uishe, karudi home hakuna salam ananiambia "utanieleza uliko kuwa" huku anatafuta mkanda aanze shunghuli. Mimi nikamwambia mimi sijatoka hata gengeni sikwenda.
Siku hiyo ndipo alipo mwita mtoto wake mwenye miaka minne nilimkuta naye akamuuliza, ndipo mtoto akamwambia "mama leo hajaenda mahali zaidi ya saloon anako sema" mume wangu akaona aibu akaondoka.
CPU, hata sasa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananiambia nisimkumbushe anakasirika mpaka nashindwa hata kuendelea kumuuliza. Ni mengi lakini naomba unisaidie "