Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Bado haupo sahihi. Nadhani wewe hiki kifaa hauelewi kinafanyaje kazi.unachanganya unatakiwa uelezee thermostat inahusikaje na cooling wewe umetupia tu Onyo
nimeelezea katika post yangu point ya 2 kuwa thermostart ni kifaa kinachokaa kati ya engine na rejeta inahusika na kuhifadhi joto la maji ya injini yasipoe ili asubuhi au huko kwenu Mafinga kwenye baridi utakavyowasha mlipuko ndani ya cyilinder combustion itokee
yeye ana Nissan xtrai tena Dsm kwenye joto hiyo kitu atupe mbali na wala asiirudishe kwani kinazuia (Block) utiririkaji wa maji mpaka gari lipate joto
How does the thermostat in a car's cooling system work? Any liquid-cooled car engine has a small device called the thermostat that sits between the engine and the radiator. ... Its job is to block the flow of coolant to the radiator until the engine has warmed up.
Gari za Ulaya matumizi mengi si ya hapa Afrika asikilize ushauri wa mafundi sio sio wa wauzaji wa magari au hadithi za mitaani
sasa gari ipo Dsm kwenye joto 38c eti liwake kwenye 100c ataachaje kusikia gari inachemsha au ina joto
Member MissM4C kamsikilize fundi wa cooling system sio dereva mzoefu
Thermostat hata kwenye friji ipo kazi yake kuu ni kuregulate flow ya coolant pale inapohitajika na ikitakiwa kusimamishwa ili kubalance kiwango cha joto.
Unaposema thermostat inahifadhi joto hivi unaifahamu hata kwa muonekano ipoje?! Inahifadhi joto katika sehemu gani labda tueleze mkuu?!
Labda tu nikuelekeze kuwa haijalishi upo mkoa gani au taifa gani, thermostat huwa haiachi kufanya kazi yake. thermostat huwa inaruhusu maji kupita kulingana na kiwango cha joto ambacho imesoma. Kazi yake ni kuruhusu coolant ipite hadi itakapokuwa na kiwango cha chini kabisa cha joto kinachohitajika kwenye Engine ndipo itafunga then joto likipanda inafungulia tena coolant iflow kushusha hilo joto chini.
Unapotoa thermostat ina maana maji yataflow muda wote gari linapokuwa on na hiyo ni hatari sana kwenye engine kwasababu oil itakuwa ipo katika temperature ambayo sio sahihi kuiruhusu kuflow vema katika kila kona ya engine na hivyo kusababisha internal wear ya engine block.
Ndo maana gari nyingi za wabongo utasikia bangili za mapiston zinakufa haraka au piston zinalika upande.
Nenda kajifunze tena kuhusu kazi ya thermostat na namna inavyofanya kazi.