Agizo kuu la Yesu ni kuhubiri injili na kuwafanya mataifa au watu wote kuwa wanafunzi wake, na kuwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Mt 28:18-20 SUV.
Kweli kabisa Mtumishi. Bwana Yesu Kristo alisema hivyo lakini unataka kaniambia kwamba wanafunzi wake Yesu waliasi??? Hawakumtii Yesu??? kwa Sababu hakuna hata mmoja aliyewahi kubatiza kwa jina La Baba, Mwana na Roho mtakatifu. Naomba ufuatane nami kwa kirefu kidogo.
Yesu alipokuwa hapa Duniani aliwahi kumpa Simon Petro Funguo Mathayo 16:19 "
Nami nakupa wewe Funguo za ufalme wa Mbinguni lolote utakalofunga duniani litakua limefungwa Mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani litakua limefunguliwa Mbinguni"
Lakini pia Kabla ya Yesu kuondoka aliwahi kusema kwamba Roho mtakatifu atakuja aliye Mwalim
Yohana 16:13"
lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote "
Yaani baada ya Roho mtakatifu kuja atatuongoza atutie katika kweli yote.
Jambo hili kila msomaji wa Biblia anajua kwamba lilitimia katika siku ya Pentecoste siku chache tuu baada ya Yesu kupaa.
Swali ninalokuuliza je wanafunzi wake Yesu walisahau kile Yesu alichoowaambia???Je waliasi?? Je wakristo wanaobatiza katika ubatizo unaodai wewe wanajua au wana ufunuo kuliko baba zetu mitume kwa maana tunadai kwamba ukristo umejengwa juu ya mitume na manabii.
Nasema hivi kwa sababu hakuna Mtu yeyote narudia tena hakuna MWANAFUNZI YEYOTE wa Yesu aliyewahi Kubatizwa au kibatiza katika Jina La Baba Mwana na Roho mtakatifu.
Baada ya kuja kwa Roho mtakatifu aliwaelekeza wabatizwe kwa Jina la Yesu Kristo.
Matendo 2:34
Petro akawaambia Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina Lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu kwa Kuwa Kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na kwa watoto wenu na kwa wote walio mbali watakaoitwa na Bwana Yesu wamjie "
Matendo 8:16
Filipo akawabatiza Wasamaria kwa jina la Yesu Kristo.
Matendo 10:48 (Petro yupo kwa mataifa nyumba ya Kornelio)
akaamuru wabatizwe kwa Jina Lake Yesu Kristo.
Matendo 19:5 (mtume Paulo kwa waefeso)"
walipoyasikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu "
Kwa kumalizia kabisa mkuu ni kwamba Biblia inatuasa kwamba lolote tunalofanya tufanye katika Jina la Yesu Kristo.
Wakolosai 3:17
na kila mfanyalo kwa neno au kwa Tendo fanyeni katika Jina la Bwana Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye, .
Swali la uchokozi kwa nini karibu kila kitu tukiomba tunamaliza na Jina la Yesu Kristo inapokuja ubatizo watu hufanya tofauti tunatumia vyeo/Sifa badala ya jina??
Next time ukitoa pepo mkuu usitumie Jina la Yesu Kristo tumia Baba Mwana na Roho mtakatifu uone kitakachokupata. [emoji23][emoji23]
Anyway nina mengi ya kuandika ila ngoja niishie hapa...