Acha kulalamika vifurushi kupanda, anza kuwa na data plan

Acha kulalamika vifurushi kupanda, anza kuwa na data plan

heartbeats

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
6,736
Reaction score
10,669
PUNGUZA MATUMIZI YA MTANDAO YASIYO NA TIJA.

👉🏿 Punguza kutizama video za kuchekesha na zisizofundisha chochote.

👉🏿Punguza na Acha kutizama video zenye maudhui ya NGONO hapa MB zinakwenda sana bila faida

👉🏿Punguza na futa magroup ya telegram yenye maudhui yasio na faida, mfano magroup ya xx,magroup ya gossips, magroup ya siasa

👉🏿Punguza na achana na WhatsApp video call zisizo na msingi,sijui kunyegezana &kukojozana n.k yasio msingi.

👉🏿Acha kupost punguza kupost na ku VIEW video status zisizo maana mfano nyimbo,gossips, Post biashara zako na picha za kujenga na quotes za msingi

ANZA KUFANYA YENYE TIJA KAMA HAYA;

👉🏿 Dowload pdf books za kufundisha na kujenga upate marifa hata ya kuwapa wajukuu na wanao

👉🏿 Kuwa bussy kiasi katika mitandao yenye kujenga na kutatua changamoto na kuhabarisha vitu vya uhakika mfano. #JamiiForums,NASA,TRADING FACTORY, Entreprenure forums n.k

👉🏿Tafuta free online course jifunze kwa bando ilo ilo upate maarifa sio kupoteza muda

👉🏿Tazama youtubes video za kujenga na kuongeza maarifa kichwani Fanya udanload tena kwa lowa quality ili wakati huna bundle uwe unatizama

👉🏿Anza biashara za mtandaoni kama Affitlate marketing,Dropping shipping,FOREX&STOCK, n.k

👉🏿Kuwa busy na mambo ya msingi tu,mtu huna hela muda wa kuanza kutizama vichekesho na ukacheka unaupata wapi

Kama unakipato basi huwezi lalamika
NB.Fanya upendacho kwa manufaa yako na taifa

Wako ktk ujenzi wa taifa email
godimpare2@gmail.com
 
Pia badala ya mda wote kushinda na simu, jitahidi kufanya shughuli ndogondogo hapo nyumbani. Kama kulima lima bustani, kung'olea majani kuzunguka nyumba, usafi wa mazingira, pruni miti, nk. Pia unaweza kutumia mda wako kufanya mazoezi kama jogging, kutembea nk. Pamoja na kukusaidia kupunguza matumizi ya bando, pia utakua unaimarisha afya na kujiepusha na punyeto.
 
Umekaa ukaona siku yako haiendi vizuri ukaamua kuandika ujinga ili upate attention mtandaoni.

Ulijuaje video za ngono zinakula sana MB kama wewe siyo Mwalimu wa kutazama video hizo chafu.
Kakushauri tu! Kuwa mpole, yeye pia Ni mtu mzima inawezekana alishapitia utazamaji wa pornography akaacha, siyo dhambi kukushauri.

Hizi hasira mkuu ukitafakari vizuri utaona hujamtendea haki jamaa yetu huyu. He is giving what he thinks it's good for us!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie rukenirukeni tu mwisho wa siku mb ni zilezile 420. 🤣🤣
Sijui hizi zitatosha kujifunza forex na NASA na akina fileti Nani nani sijui
Yaani akili yangu imegoma kabisa kukipokea hiki kifurushi cha mb 420. Naona bora niwe sina data kabisa nijue moja😁😁
 
Hayo mateso yote ya nini? Uzi wako hauna msaada. Kila mtu ana namna yake ya kutumia Internet na kwa namna inayomfaa.
Kingine, malalamiko ya watu ni sahihi kabisa; tuliaminishwa yatafanyika maboresho bora, na gharama za Internet zingeshuka. Ajabu, hali imekuwa kinyume chake—wacha tulalamike.
 
Umekaa ukaona siku yako haiendi vizuri ukaamua kuandika ujinga ili upate attention mtandaoni.

Ulijuaje video za ngono zinakula sana MB kama wewe siyo Mwalimu wa kutazama video hizo chafu.

Napasuka leo kwa kicheko eti mwalimu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamani huu ni muda wa kumuombolezea hayati mzee wetu sio muda wa kutukataza kuangalia videos ambazo ni rahisi kuzifanyia rehearsal
 
Kakushauri tu! Kuwa mpole, yeye pia Ni mtu mzima inawezekana alishapitia utazamaji wa pornography akaacha, siyo dhambi kukushauri.

Hizi hasira mkuu ukitafakari vizuri utaona hujamtendea haki jamaa yetu huyu. He is giving what he thinks it's good for us!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sihitaji ushauri wenu nyote wawili.
 
hata ukichukua hatua hizo, makampuni bado yanaweza kukuibia data ili iishe haraka ulazimike kununua tena
 
Nawakumbusha tu ,bado tupo uchumi wa kati ...
 
Pia badala ya mda wote kushinda na simu, jitahidi kufanya shughuli ndogondogo hapo nyumbani. Kama kulima lima bustani, kung'olea majani kuzunguka nyumba, usafi wa mazingira, pruni miti, nk. Pia unaweza kutumia mda wako kufanya mazoezi kama jogging, kutembea nk. Pamoja na kukusaidia kupunguza matumizi ya bando, pia utakua unaimarisha afya na kujiepusha na punyeto.
🤣🤣🤣😂😂😂
 
Back
Top Bottom