Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Siri ya Kuepuka Huzuni na Unyonge Kwenye Maisha:
Punguza Matarajio
Moja ya vyanzo vikubwa vya msongo wa mawazo na unyonge kwenye maisha ni tabia ya kutarajia watu wafikirie na kutenda kama unavyofikiria wewe.
Tunapoweka matarajio makubwa kwa watu, tunajisahau kuwa uhalisia wa maisha yao na vipaumbele vyao vinaweza vikawa tofauti kabisa na vyetu.
Fikiria mifano hii:
Mfano wa 1: Wewe una desturi ya kuwajulia hali ndugu zako mara kwa mara. Ndani ya nafsi yako, unatarajia nao wakukumbuke kwa kiwango hicho hicho. Wasipofikia kigezo hicho, unajikuta umebaki na huzuni na upweke.
Mfano wa 2: Kwenye mahusiano, unamjulia hali mwenza wako kila wakati kuonyesha upendo wako. Unatarajia na yeye afanye vivyo hivyo, lakini unagundua yeye hana kabisa habari na mfumo huo wa maisha.
Tatizo sio wao kutokupigia simu au kutokutafuta. Tatizo liko kwako kwa kutaka kulazimisha kila mtu afikirie kama wewe. Binadamu tunatofautiana.
Ukifanikiwa kuujua na kuukubali ukweli huu, utaepuka unyonge na mawazo hasi. Utafahamu kuwa wewe na wao ni watu wawili tofauti kabisa.
Chukua somo hili leo, litakusaidia kulinda amani ya moyo wako na kuepuka huzuni zisizo na lazima.
Ni hayo tu!