Acha kuwa na wasiwasi sana kuhusu yaliyotokea nyuma au yanayo kuja mbeleni

Acha kuwa na wasiwasi sana kuhusu yaliyotokea nyuma au yanayo kuja mbeleni

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Acha kuwa na wasi wasi sana na mambo yaliyotokea huko nyuma katika maisha yako au ambayo yanayo kuja huko mbeleni

Screenshot_20241111_115615_Google.jpg

Usiyape kipaumbele na vuta pumzi ndefu,ishi wakati uliopo sasa na kuwa mwenye shukrani kwa wakati ulionao na ulipo sasa

Mda huu ndio ambao tunao,kwahiyo sahau mambo kama ingekuwaje au itakuwaje,kubaliana na yaliyo tokea na tambua yameshapita ishi kwa wakati uliopo nao sasa

Kumbuka tunaishi mara moja na tuna bahati kuwa tupo hai

Ni hayo tu!
 
Mi nikiwazaga kuna kipindi jf tulikua tunapata vocha daah naumia sana (yaliyopita)

Naumia zaidi baada ya uzi wetu kurudishwa ila mod wakapita nao.. (yajayo)
😂😂😂😂

Ni sehemu ya maisha,dunia haikuumbwa mambo yawe mazuri kila siku kuna nyakati ambazo mambo hayaendi kama tunavyotaka,ndio maana hata dunia yenyewe imeinama kidogo katika mhimili wake kuonyesha mambo siku zote hayata kuwa sawa boss
 
Mada nzuri sana
..Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
..Ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.
..Tusi isumbukie kesho mana kesho itajisumbukia yenyewe
..KESHO yetu ni ya Mungu ,tusijivunie kuhusu kesho siri ya kesho yetu anayo Muumba wetu.
**NANI KAIONA KESHO?

NINI TUKIFANYE.
Tufanye mambo yote kwa utukufu wa Mungu sio kwa mashindano wala kwa kujivuna ila kila mmoja wetu ampende mwenazake(jirani) na amuhesabu mwenzake kuwa ni bora kuliko yeye
Tutambue ulimwengu mzima/dunia na vyote viujazavyo ulimwengu na wakaao ndani yake ni mali ya Mungu.
Tujinyenyekeze mbele za Mungu tuwe na utu kwa watu tuwe wanyenyekevu na wenye upendo,tukimtumainia Mungu,tukimpendeza Mungu na wanadamu
TUKIJUA DUNIANI sio kwetu,sisi ni wasafiri ,DUNIANI tunapita.(KIFO NI HAKIKA KWA WOTE WENYE MWILI WATAKUAFA LAZIMA)

Lakini tunapitaje duniani tuache alama nzuri maisha yetu yawe kielelezo kizuri cha mtu mwema.
 
Attachments

  • images - 2024-11-11T121745.974.jpeg
    images - 2024-11-11T121745.974.jpeg
    28 KB · Views: 4
😂😂😂😂

Ni sehemu ya maisha,dunia haikuumbwa mambo yawe mazuri kila siku kuna nyakati ambazo mambo hayaendi kama tunavyotaka,ndio maana hata dunia yenyewe imeinama kidogo katika mhimili wake kuonyesha mambo siku zote hayata kuwa sawa boss
Mi nikifikilia kuwa hakuna kitu kinadumu milele daah huwa nainjoi sna najikuta kama molecules in air
 
Ni sahihi kabisa hata ukiwa na nyakati ngumu unajua ipo siku moja kila kitu kitaisha,inaleta matumaini na faraja pia
Sana mkuu..
Inafikia kipindi hata kifo tena inakua si jambo la kustukiza ukiishi ndani ya hii misingi..
Nathing permanent... Sio mapenzi, maisha, matatizo wala nini..
Ni kuyakabili tu na kuishi nayo...
 
Mada nzuri sana
..Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
..Ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.
..Tusi isumbukie kesho mana kesho itajisumbukia yenyewe
..KESHO yetu ni ya Mungu ,tusijivunie kuhusu kesho siri ya kesho yetu anayo Muumba wetu.
**NANI KAIONA KESHO?

NINI TUKIFANYE.
Tufanye mambo yote kwa utukufu wa Mungu sio kwa mashindano wala kwa kujivuna ila kila mmoja wetu ampende mwenazake(jirani) na amuhesabu mwenzake kuwa ni bora kuliko yeye
Tutambue ukimwengu mzima/dunia na vyote viujazavyo ulimwengu na wakaao ndani yake ni mali ya Mungu.
Tujinyenyekeze mbele za Mungu tuwe na utu kwa watu tuwe wanyenyekevu na wenye upendo,tukimtumainia Mungu,tukimpendeza Mungu na wanadamu
TUKIJUA DUNIANI sio kwetu,sisi ni wasafiri ,DUNIANI tunapita.
Lakini tunapitaje duniani tuache alama nzuri maisha yetu yawe kielelezo kizuri cha mtu mwema.
Asante sana boss kwa maneno yenye hekima na busara kubwa,yanatia faraja na yanaleta matumaini pia

Hiki ni chakula cha ubongo ambacho ni muhimu sana kwa maisha yetu
 
Sana mkuu..
Inafikia kipindi hata kifo tena inakua si jambo la kustukiza ukiishi ndani ya hii misingi..
Nathing permanent... Sio mapenzi, maisha, matatizo wala nini..
Ni kuyakabili tu na kuishi nayo...
Kwanini ulijiita poor brain wakati naona ni rich brain😂😂
 
Back
Top Bottom