Acha lawama, ni wewe ndiye unayepaswa kuwajibika juu ya maisha yako

Haswa
 
hiyo ni kwasisi wanaume tu!.
Hata wanawake waache, mwanamke asilalamike mwanaume wake kuchepuka, bali akae chini na kujiuliza kwa nini anachepuka, akigundua mwanaume ni tabia yake na yeye hawezi kuendana na hiyo tabia anapaswa kujistaafisha kwenye hayo mahusiano. Lawama hazihitaji maana huyo mwanaume hakutafutiwa
 
Mwisho wa siku ni wewe:
1. Ukiwa Bora ni wewe
2. Ukiwa lofa ni wewe
3. Ukiwa mjinga ni wewe
4. Ukiwa mzembe ni wewe
5. Ukiwa masikini ni wewe
6. Ukiwa tajiri ni wewe
7. Ukiwa hodari ni wewe
8. Ukiwa mbivu ni wewe
9. Ukisubiria bahati ni wewe
10. Ukichukua hatua yakuona fursa ni wewe
11. Ukiwa na mawazo hasi ni wewe
12. Ukiwa na mawazo chanya ni wewe

...............ongezea kwa sababu ni wewe.......
 
Nakubaliana na wewe 100%. Kwa mfano sasa hivi, tuache kuilaumu CCM na tuingie barabarani kuiondosha kwenye madaraka kwa sababu inazidi kuleta umaskini.
Ingia mwenyewe barabarani kwasababu wewe ni masikini wenzio sisi sio masikini tunafurahia nchi
 
Ingia mwenyewe barabarani kwasababu wewe ni masikini wenzio sisi sio masikini tunafurahia nchi
Jiongelee mwenyewe, huyo tajiri mwenzako umeongea naye saa ngapi?, by the way hakuna tajiri anayesema kuwa ni tajiri.
 
Jiongelee mwenyewe, huyo tajiri mwenzako umeongea naye saa ngapi?, by the way hakuna tajiri anayesema kuwa ni tajiri.
Huo umasikini upo kwenye ukoo wenu sisi kwenye ukoo wetu sio masikini barabarani ingia wewe na ukoo wako ambao ni masikini msiongelee wengine
 
Just calm down!.. jiangalie wewe...wewe ndiye kiongozi wa maisha yako, hata kama ni katika hali duni kiasi gani, muamuzi wako ni wewe.
 
Vp na wale wanaolamu chama cha siasa ...kuwa wako hapo kwa sababu ya hiko chama🤔🤔
 
Vp na wale wanaolamu chama cha siasa ...kuwa wako hapo kwa sababu ya hiko chama🤔🤔
Mchezo wa lawama haukosi sababu ndugu, unakupa liwazo na pumbazo la kutosha unajisahau kuishi maisha yako unabaki na bila fulani ningee.... bila Chama X ningee..... mwisho wa siku "it is too late to catch the train".
Vicious cyle of ........
Hao jamaa wanajichelewesha wenyewe ila kama wapo humu nina uhakika Jamii forum inatia elimu tosha linabaki suala la mtu binafsi.
 
Ukweli mchungu. Tumebaki kulaumu mifumo tuliyoikuta bila kufanya mabadiliko (kupambana).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…