Acha makasiriko tafuta hela": kauli inayochochea mmomonyoko wa maadili

Acha makasiriko tafuta hela": kauli inayochochea mmomonyoko wa maadili

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Kwa wakati huu wakati taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la kukosa maadili kumetokea pia namna nyingi za shetani na wafuasi wake kuwakatisha tamaa wale wote wanaopigania maadili mema. Imefikia wakati mtu ambaye anashauri kuhusu mwenendo mzuri kwenye jamii kudhalilishwa na kuonekana mjinga na fukara. Hii kauli ya "ACHA MAKASIRIKO TAFUTA HELA" imepata umaarufu mitandaoni na nje ya mitandao katika kuwapuuza wale wote wanaotaka jamii iwe na maadili mema.

Kwa mfano kwa sasa kuna idadi kubwa ya watu maarufu hasa wasanii wanaofanya mambo ya aibu ila akitokea mtu kwenye platforms zao za mitandaoni kuonyesha kupinga badi hushambuliwa na mashabiki wa msanii husika. Hata kwenye familia ambazo sio maarufu utakuta mama kajiachia hovyo hovyo mbele ya watoto wake wa kiume lakini ukitaka kukemea kuna mawakala wa shetani hujitokeza na kukuambia "acha makasiriko tafuta hela" na wengine husema "ACHA KUPANGIA WATU NAMNA YA KUISHI"

Ninachoweza sema ni kuwa hela imekuwa ikitafutwa kwa maelfu ya miaka iliyopita hadi leo lakini haiwezi kuwa sababu ya kukiharibu kizazi hiki kwasababu ya kutafuta hela. Ninashauri pia wanaofanikiwa kupata hela nyingi wazitumie katika namna sahihi na isiwe katika namna ya kuiharibu jamii.

Kwa mfano kwenye haya mambo ya ushoga ukiuliza ni nani huwaingilia hawa vijana mara nyingi jibu huwa ni mtu fulani mwenye hela kama kigogo serikalini, wanasiasa, wafanndyabiashara na matajiri wengine''. Lemutuz alishawahi post huko Insta kuwa kuna Kigogo wa zamani alioa mwanaume mwenzake.

Tafadhalini watanzania tutafute hela na maadili tuyalinde. Pesa iwe baraka na isiwe chanzo cha laana.
 
Huenda vigogo hao wanaoingilia vijana wa kiume wanafanya hivyo kama moja ya sharti la kishirikina ili kulinda nyadhifa zao na biashara zao. Ushirikina una masharti mengi ya kishetani
 
Duh! Kijana mzima wa kiume unaliwa mkuyenge na bosi/tajiri fulani kwa malipo gani hayo ya kudhalilishwa? Huu ni ushetani
 
Huenda vigogo hao wanaoingilia vijana wa kiume wanafanya hivyo kama moja ya sharti la kishirikina ili kulinda nyadhifa zao na biashara zao. Ushirikina una masharti mengi ya kishetani
Wenye hela wanatuhumiwa mno kuwala vijana wa kiume.
 
Huenda vigogo hao wanaoingilia vijana wa kiume wanafanya hivyo kama moja ya sharti la kishirikina ili kulinda nyadhifa zao na biashara zao. Ushirikina una masharti mengi ya kishetani
Ndio uhalisia
 
Hela ya serikali si yako, ukipata nafasi butua.

WhatsApp Image 2023-04-14 at 8.33.16 AM.jpeg
 
Back
Top Bottom