Acha uvivu soma hii uone

kanewi

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
298
Reaction score
200
Mjomba kwenye miaka ya 70 alipata safari ya masomo nchini Urusi,kipindi hicho alikuwa na miaka 25 hivi,.akiwa kule alikuwa kila jpili anakwenda kwenye makanisa kuabudu mungu wake lkn alikuwa anajikuta kijana yupo peke yake kanisa zima,warusi wakawa wanamshangaa sio kwa sababu ya rangi yake bali kwa umri wake wakawa wanamuuliza kama anatatizo lolote,.ujue ni nadra sana kumkuta kijana makanisani kwenye miaka ile sijui kwa sasa,yeye alikuwa anawajibu kuwa hana tatizo lolote,.

Siku moja wazee wa kanisa ikawabidi wamuwekee kikao ili wamuhoji,akaitwa jmosi moja usharikani na kumuhoji sana baada ya kuridhika kuwa hana tatizo bali ni utamaduni ambao huku kwetu ndo tumeuzoea,.wazee wale wakamuambia kuwa,.kawaida wao kule huenda kanisani kutubu kwa madhambi waliyoyafanya kipindi cha ujana wakati wanatafuta,.

Wakamuambia kuwa kijana katika kutafuta unaweza kukutana na mambo mengi sana ya hatari ambayo wengine wanadiriki kuua bila kukusudia ilimradi kupata,kupokea rushwa,kuiba,kudhurumu kwa mtindo wa viji NGO'S,.wakamuambia tafuta hela kwanza kwa staili yoyote ile then njoo utubu kwa kutoa sadaka uzeeni,.

ROZI MUHANDO AMEIMBA''UOGA WAKO NDO UMASIKINI WAKO....UNAJIROGA MWENYEWE''jamaa aliogopa kuona wazee wa kanisa wanamshauri aache kwenda kanisani kwa umri wake ule bali akatafute alafu aje uzeeni,kwetu ni tofauti.,kabisa ni tofauti,.kuna vitabu huku mitaani vimeenea vinapumbaza watu hasa vijana,utasiki ,THINK BIG,.GET RICH, BE A BIG MONEY MAKER,Na vingine,.ukisoma utasikia...fumba macho na sema ,,NITAFANIKIWA MARA 24,KAA SEHEMU TULIVU NA ANGALIA JUU NA SEMA ''YES I CAN WIN'' Na upuuzi mwingine humo,.

Ndg life is not so simple just like what these books say,.kimbiza mtaani hacha kusema nitafanikiwa uku umekaa chumbani umefumba macho,hayo ni mambo ya imani kwenye nyumba za ibada ndo maana wale wazee wakamuambia mjomba toka kanisani acha biblia nenda mitaani kimbiza life is not from the church but from the street,.hebu hii haihitaji elimu,fuatilia matajiri au watu waliofanikiwa kama walikuwa wanavisoma hivi vijitabu vya uongo vinavyokopy maneno kwenye biblia na kuja kuwatia uvivu watu,.achana navyo tafuta kitabu cha,.RICHDADY POORDADY hiki ndo kitabu kinakupambinu zote sio za kukaa kivulini na kusali,.NENO ''TAFUTENI NANYI MTAPATA''Linatosha kuwa sara,,unapotafuta ndio kumheshimu Mungu kwani umetekeleza neno lake..
 
Walikuwa wanamuona chizi, wakati huo nani anathubutu kusogelea kanisa Urusi?
 
umenena vyema sana,kuna watu wana mavitabu ya ujasiriamali lukuki,audio cds lkn hawana hata mradi wa genge,wanalala wanaota utajiri tu.
 
Kuna mtu aliwahi kunipa mavitabu sijui "how to make profit while sitting, sijii vitabu vya Ben Carson, sijui vya yule Mjapani the akaniambia eti nikimaliza kuvisoma yaani mimi ni kufumba na kufumbua, na hapo sasa nilikuwa ndiyo namaliza chuo sina hata sehemu ya kusoma gazeti niweze kuaply kazi.Kinachotupumbaza Watanzania tunadhani eti maisha ni rahisi.Maisha ni mtihani vitabu hivo ni vya kusoma wakati umepumzika kama vile tunavoangalia movies kwa kujifurahisha.Utajaza vitabu mpaka koridoni bila kupambana wewe kama wewe hamna kitu zaidi tu ya kuimprove english yako kutoka kwenye hizo novel
 
Mh naomba nipite.Na ukifa kabla ya haujafika huko?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
unajua jamaa hawagawi vitabu bure, wanauza wanapata pesa wakiwa wamekaa na kutoa mipango ya new York huku watu wanakimbizana nahatuoni chochote. Ni kama IMF na WB walivyokuwa wanakuja na mipango isiyofaa Africa, anyway vinasaidia watu kuweza kuanz kufikiri kwa namna nyingine
 
Nani kakuambia utakufa kipindi ukishazeeka? Tazama sasa hivi vijana wenye miaka 30 wanakufa.
Usiishi kwa theory zilizotoka kwenye midomo ya watu wengine.
Na hivi vitabu unavyotaja vinatoa motivation tu na inspiration.
Kumbuka "If you want to become successful in business you should live with successfull business men,if you cant live with them call them,if you cant talk to them,go to the book store which is near you and buy a book talk about success in business
 

That's right!
 
Thats utter nonsense nani kakudanganya Mungu ni wa wazee tu? Kila siku tunamhitaji Mungu kwenye maisha yetu bila kujali umri wetu
 
Nimevisoma baadhi ya vitabu hivyo kama rich dad poor dad na thnk big,si kwamba watu wasivisome ubaya watu wanavitumia vibaya tu kwa kuvisoma bika kutake action na pia ni sawa na mtu and phd ya busnes lakn hada genge hana.HIV VITAB NI KWA STARTING POINT AND IDEA.KUMBUKA BILL GATES KILA MWISHO WA MWAKA ANASAFIR KWENDA KUKAA SEHEMU MBAL NA NYUMBAN NA KUSOMA VITABU BORA VYA UJASILIAMALI NA UONGOZI.SIRI YA MAFANIKIO INAANZIA NA IDEA AMBAYO IPO KWENY VITABU.usikurupuke tu eti natafuta hela,utafirisika bila kutulia.
 
Mpinga kristo @work, Kwa taarifa yako Mungu(Jehova) ndio kila kitu, wengine hatujasimuliwa bali tuna ushahidi juu ya hili, Tumemuona akitupigania zaidi hata ya jinsi tulivyowaza,

Biblia inasema ktk Isaya kuwa "Tazama vijana watachoka na kuzimia lakin wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya, watakwenda juu kama tai"

Sasa we kalia kutoa povu na upotoshaji wako wengine hatuna wasi kabisa juu ya elimu wala maisha kwani tunayemwamini anaweza yote yaani yeye ni MUNGU JUU YA YOTE.
 
miaka 70 ni kijana?..rudia upya hadithi yako.
 
Jamaa alikuwa sahihi kusali kwa kuwa laitoka na utaratibu huo,hapa kwetu .kimsingi binafsi ninaamini kushiriki ibada ni jambo muhimu kwa kuwa hukuweka karibu kabisa na mungu,sio lazima ufanikiwe kwa kupitia rushwa n.k na sidhani uzee ni umri mzuri wa kuanza kumuabudu mungu.mungu anaabudiwa wakati wowowe/popote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…