Achana na kusave pesa bank

Achana na kusave pesa bank

PintoG

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2017
Posts
612
Reaction score
732
Nilipokuwa na miezi sita kwenye ajira yangu ya kwanza tayari nilikuwa na utaratibu wa kusave bank kwa njia ya kukatwa juu kwa juu kiasi flani.

Siku moja nikakutana na aliyekuwa mwalimu wangu chuo. Katika kubadilishana mawazo akaniambia kusave bank kwa njia ile si sahihi kwangu. Akanishauri niingie kwenye vikundi vya hisa na succos.

Kweli nilijiunga na vikundi vitatu tofaut vya hisa, ambavyo kila mwezi nilikuwa nanunua hisa si chini ya 250,00 kwa mwezi lakini pia nikajiunga na saccos ya ofsini nikawa nakwatwa 50,000 kila mwezi.

Kwa muda wa miaka miwili sasa naona matunda makubwa sana mfano kwenye vikundi hisa naweza kopa hela bila masharti magumu, lakini kila mwaka pesa inaongezeka ukilingana na nilipokuwa nasave bank.

Lakini pia vikundi hisa vina faida pale mwanachama anapopata matukio ya kijamii kama misiba, sherehe na ugonjwa. Lakini pia nimejifunza sisi wanaume nidhamu ya kusave pesa kidogo ni ndogo sana, mfano umepata 30,000 nje ya salary, ukiwa na vikundi hisa rshisi sana kutoa 15,000 ukaitupa kweny hisa.

Bank itumike tu kuweka pesa nyingi ikiwa kwenye njia za biashara ama uwekezaji na si kibubu.

Vijana tujiunge kwenye vikundi hisa vinasaidia sana. Na vikundi vizuri ni vile ambavyo vina wanachama wengi wanawake kwani wana nidhamu sana ya pesa na kuheshimu ratiba za vikundi.
 
Siku hizi ndio style za watu wengi kua na SACCOSS na VICOBA na kwa kweli mimi binafsi vimenisaidia sana. Tatizo saa nyingine watu wanakua hawapo serious sana hali inayopelekea kuvunjika kwa utaratibu huu kabla hamjatimiza malengo yenu.
Natamani sana ningepata kikundi /watuwalio serious kufanya nao hii kitu.
 
Risk yakei
Inashauriwa kujiunga na vikundi hisa unavyovijua na vyenye wanachama mnaojuana vizuri, risk ni minimal sana, japo hakuna jambo lilo salama asilimia mia.
 
Siku hizi ndio style za watu wengi kua na SACCOSS na VICOBA na kwa kweli mimi binafsi vimenisaidia sana. Tatizo saa nyingine watu wanakua hawapo serious sana hali inayopelekea kuvunjika kwa utaratibu huu kabla hamjatimiza malengo yenu.
Natamani sana ningepata kikundi /watuwalio serious kufanya nao hii kitu.
Mkuu upo sahihi, mfano tu unataka kukopa milio 2, kweny succoss ama kikundi hisa kilichostable ni rahsi tu, lakin kakope bank uone... Mashariti yalivyo tait.
 
Kuficha hela bank ni UPUMBAVU kwa dunia ya sasa, natamani watu wengi zaidi wangemwelewa mtoa hoja,bank ni kwa ajili ya akina Mengi wanaokopa vijisenti vyetu tulivyovikusanya huko,
 
Kidogo naanza kuelewa.

Maana kuna watu nasikia wanaendesha vibiashara kwa vikoba na mfuko wa Tulia.

Ngoja nami nifanye mchakato.
Mkuu ukitaka kuamin hilib, angalia pia wakina mama wengi ambao ni head of the family, wana biashara ndogo ndogo lakin wanasukuma maisha kwa kusomeaha na hata kujenga, wanasave kupitia vikundi hisa na vikoba. Faida yake huja pale mnapovunja mwisho wa mwaka, faida zinatokana na zile interest za mikopo, faini na hata biadhaa za vikundi kama kikundi kinafanya hivo pia.
 
Ni kweli, kua na nidhani ya pesa haswa sisi wanaume kuna kaugumu kidogo...

Ila mimi vikundi sinaga imani navyo... napenda fix deposit, na ndiyo nachofanya...

Naweka bank tofauti tofauti ila kwa fix deposit.

Cc: mahondaw
Vikundi mara nyingi ni kuangalia aina gan ya wanachama, location na mahusiano, katiba, uwezo wa wananchama wengi, source za hela za wanachama wengi. Mkuu mm hata nikiwa nan20,000 mfukoni nawaza teni niongeze hisa, ten nikae kuangalia game ya liva na man cty na bia zangu mbil au tatu basi.
 
250,000 halafu 50,000... Watanzania walio wengi huo ndio mshahara! Ikitokea anamkopo benki au bodi ya mkopo ndio inabaki kiasi kidogo zaidi! Nionavyo wewe mshahara upo juu au bado hujawa na majukumu! Wazo zuri ila vidole haviringani
 
Mkuu hii kitu haijalishi unapata kiasi gan, utanunua hisa kulingana na uwezo wako, amin kuna mtu anapata take home one m lakin still kusave ni shida, mkuu wakina mama wenye biashara ndogo ndogo kabisa wanatumia vikundi hisa kusave, so hata mweny take home ya laki 3 vikundi vya namna hii ndo mkombozi wa kununua plot na hata kuweka msingi.
 
250,000 halafu 50,000... Watanzania walio wengi huo ndio mshahara! Ikitokea anamkopo benki au bodi ya mkopo ndio inabaki kiasi kidogo zaidi! Nionavyo wewe mshahara upo juu au bado hujawa na majukumu! Wazo zuri ila vidole haviringani
Walaaa tena wanaojiunga wanakuaga watu wa vipato vya kawaida sanaaaa. Kinachotakiwa ni nidhamu tu yakujua kwamba kila mshahara ukiingia kabla hujafanya matumizi yoyote 50,000 au 100,000(inategemea kiwango cha kikundi) sio yako ni ya SACCOSS /VICOBA.
Mikopo huku ni ya masharti nafuu na mara nyingi collateral ni hisa yako haihitaji sijui kiwanja wala gari. Na pia hua vikundi vingi vinakua na utaratibu wa kusaidiana kwa shughuli za kijamii mf. Misiba, uzazi, harusi, ugonjwa etc. bila mhusika kukatwa wala kuumiza kichwa!!
Advantage ni kubwa ndo maana wanaoelewa hata kama mshahara/kipato ni kdg lazima ajiunge.
We unafikiri kina mama Ada, kodi na pesa za kukidhi mahitaji tunapata wapi kina baba wanapokwama??
Sasa pesa ukiweka benki haizai lakini huku hisa inakua na faini ndogo ndogo zinatunisha mfuko shares zinakua.
 
True
 
Asante sana mtoa mada. Ulichosema ni kweli kabisaa. Nilipoajiriwa tu nioijiunga na saccos na kuanza kununua hisa na kuweka akiba. Baada ya mwaka mmoja nikianza kukopo na kufungua biashara. Hadi sasa nimebakiza miez kama 6 hivi naachana na kazi naenda kusimamia biashara yangu. 90% ya mtaji wangu nmeupata saccos
 
Very true.
Mi kuna vitu nimefanikisha ambavyo kwa savings zangu binafsi za benki au bila kikundi nisingeweza fanikisha. Ila through Vicoba nimefanya na ninaendelea kwa kifupi nimenogewa. Kuna wakati naona wadada wapo wapo tu hana vikundi wala hana savings natamani niwahubirie ,yani natamani niwashike mikono wajiunge na vicoba.
Anae elewa ataelewa tu!!!
 
Back
Top Bottom