Achana na tetesi: Lil Ommy, go and get 'em, bro!

Achana na tetesi: Lil Ommy, go and get 'em, bro!

Baada ya Mtangazaji mwenye ushawishi wa kituo cha Times FM Ommary Rajabu Saleh Tambwe aka Lil Ommy kuaga rasmi kuwa hatoendelea kuwa mfanyakazi wa kituo hikch alichokifanyia kazi kwa muda mrefu akitokea VoT FM (Voice of Tabora FM) takribani miaka 10, tetesi zimekuwa nyingi.

Wengine wanadai nguvu ya pesa imemnyakua, na kuwa anaenda kujiunga na kituo cha redio cha Wasafi FM.

Ukirejea kauli zake kadhaa na mahojiano aliofanya kwenye kipindi cha Salama, alidai alishawahi kukutana na Marehemu Ruge na alikuwa akimuhitaji ila walikuwa kwenye mazungumzo.

Kikubwa alisisitiza ofa ni nyingi ila hawafiki kwenye makubaliano/muafaka na kupelekea abaki kwenye kituo mama anachofanyia kazi.

Lil Ommy ana deal nyingi sana. Pengine mshahara wa Times ulikuwa wa kawaida ila aliamua ajitengenezea himaya akiwa pale.

Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:

Je, ni kweli anaenda kujiunga na Wasafi FM?

Je, Clouds wanatimiza mazungumzo yaliyoanzishwa na Ruge?

Anaenda kujenga empire yake na kuwa mkubwa zaidi kama walivofanya Sky Walker, Sam Misago na MillarAyo?

Anaenda ku-deal na kipindi chake walichokuwa wameanza kukitengeneza na Raque?

Kuna kampuni kubwa imemtaka kumsimamia kwa ukubwa zaidi ndiyo maana kasepa na timu yake?

Tuache muda uzungumze na tuachane na "Tetesi", pesa anayopata/alizopata kutoka kwenye matangazo ni nzuri: Minutes Maid, TOTAL, Johar Rotana, Coca Cola, nk zinaweza kumfanyia kitu na siyo kwenda kuwa chini ya watu tena.

NB: Next week, J3, atawajuza nini anafanya na yupo wapi.

Tchao!

Lill Ommy nani alikwambia kuna tetesi? Mbona wajitungia?
 
Lill Ommy nani alikwambia kuna tetesi? Mbona wajitungia?
umeelewa kilichoandikwa lakini..?, nani katunga..?, kilichosemwa humo ni kuwa watu waachane na tetesi za kuwa amesajiliwa na wasafi na wasubiri muda utazungumza,
next time ukisoma uwe unafika mpaka mwisho
 
Sheria ndo zinawabana ili uweze kipata kibali cha kusikika nchi nzima lazima uwe umetimiza angalau miaka mi3 toka uanze kurusha matangazo ya radio yako kwa iyo sio kwamba diamond hana uwezo bali ni taratibu na masharti ndo yanambana we subir atimize hivo vigezo uone ni swala mda mfupi kuskika nchi nzima.
sheria huwa miaka3, ila mbona Efm Wenyewe baada ya miaka2 tu wakaanza kwenda mikoani,na Times wanamiaka mingi sana ila wanasikika mikoa miwili tu...?
 
Slowly,
Uko sahihi kabisa, Ndio maana hata hizi Radio nazo zinajiboresha kwa kutengeneza Studio nzuri amabazo zinaendana na matakwa ya Online, Pia focus iko kwenye marketing na Profit,
WASAFI Youtube channel ina takribani subscriber 1.15M, Ambapo content zinazowekwa zinafikisha mpaka views 360k per week, malipo yake ni mazuri ukiringanisha na wadhamini walioko kwenye baadji ya vipindi, lakini pia kutokana na views wanaoleta matangazo kwenye You Tube channel ni wengi tofauti na kwenye Radio station
Mfano mwepesi tu, hujiulizi kwa nini TV za kisasa zimewekewa "Internet" capability? Yani ni TV tu ila pamoja na function za kawaida za TV imepewa na uwezo wa wewe kuwa connected na mtandao na unaweza ku stream na kuperuzi kwenye social medias. Hili halijaja kwa bahati mbaya ila ni kwa kuwa dunia ndiko ilikofikia kwa sasa.
 
Mfano mwepesi tu, hujiulizi kwa nini TV za kisasa zimewekewa "Internet" capability? Yani ni TV tu ila pamoja na function za kawaida za TV imepewa na uwezo wa wewe kuwa connected na mtandao na unaweza ku stream na kuperuzi kwenye social medias. Hili halijaja kwa bahati mbaya ila ni kwa kuwa dunia ndiko ilikofikia kwa sasa.
Dunia inaenda kasi sana, ukibaki nyuma na usipoenda na kasi nayo ni shidaaa
 
Back
Top Bottom