Acheni kulazimisha kumpeleka kumzika marehemu kule ambako alikataa alipokuwa hai

Acheni kulazimisha kumpeleka kumzika marehemu kule ambako alikataa alipokuwa hai

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kumbe Marehemu Mrema akiwa Hai aliacha kabisa Maagizo kuwa Akifa asipelekwe Kuzikwa Kilimanjaro (Moshi) na badala yake azikwe hapa hapa Mkoani Dar es Salaam na kwamba Watakaolazimisha Kumsafirisha basi wajiandae Kuondoka nae rasmi Duniani (Kufa) kama ilivyotokea.

Najua wapo mtakaolibishia hili kwa kutaka tu Ligi (Ubishi) ila Binafsi nina Shuhuda zangu Tatu za mfano huu huu wa Marehemu Mrema na Wote waliolazimisha leo wamekuwa ni Historia (Wameshakufa) muda mfupi baada ya Mazishi ya Wapendwa Wao waliowalazimisha kuwapeleka Vijijini Kwao kwa Maziko.

Kuna Marehemu Mmoja aliacha Wosia kwa Wanae kuwa Akifa tu Nyumba yake isiuzwe na iwe ni Nyumba ya Wajukuu zake Kuishi na alivyokufanyia Watoto Wakaamua Kuiuza na kinachoendelea sasa huyo aliyeinunua Usiku Kucha Yeye na Wanafamilia wake hawapati Usingizi ila Kukikucha tu na muda wa kwenda Kuwajibika ndiyo Wanapata Usingizi hall iliyosababisha Wengine kufukuzwa Makazini kutokana na Kupungua kwa Ufanisi wao wa Kiutendaji.

Heshimuni mno Kauli za Marehemu.
 
Acha porojo wewe. Hiyo ni coincidence tu ukishakufa huna influence yoyote tena kwa yatakayotokea duniani, influence yako itabaki kama ulifanya ya maana tu ila kama ulipuyanga unazidiwa hata na mti uliochomwa mkaa maana mkaa utapikia watu wale chakula.
 
Leta huo ushahidi wa mrema kwamba alisema asizikwe Kilimanjaro...

Vinginevyo haya ni mawazo na imani yako binafsi.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Mkuu,Mm sikuwepo wakati huo na sijui alisema nini ila nataka nikwambie tu.Mtu akishakufa hana uhusiano na walio hai na iwapo lolote litafanyika kwa dhihaka dhidi yake na waliosalia basi usishangae wakapatwa na jambo.
 
Acha porojo wewe. Hiyo ni coincidence tu ukishakufa huna influence yoyote tena kwa yatakayotokea duniani, influence yako itabaki kama ulifanya ya maana tu ila kama ulipuyanga unazidiwa hata na mti uliochomwa mkaa maana mkaa utapikia watu wale chakula.
Ukifa unataka tukuzike hapa hapa Dar es Salaam au tukupeleke Kijijini Kwenu?
 
Ukifa unataka tukuzike hapa hapa Dar es Salaam au tukupeleke Kijijini Kwenu?
Mkanizike sehemu ambayo hata hawanikumbuki halafu muiache familia yangu mjini?Nani kasema hivyo?Kwanza nizikwe jirani na nyumba yangu ili niwe natoroka makaburini mara mojamoja nione waliokuwa wanamtamani mama Bhoke! 😂😂😂😂
 
Mimi napenda yawe yanawatokea watu wabishi ili waheshimu kauli au maagizo ya ndugu zao.
Nina Ndugu yangu Mmoja Mlevi balaa alishasema Akifa ( Akidanchi ) tu katika Jeneza lake tumuwekee Safari Lager Tatu na Mzinga Mmoja wa Konyagi hivyo tayari tumeshatenga pembeni Bajeti kwa ajili hiyo. Hatutaki kabisa kwenda Kinyume nae ysije kutupata ya Mrema na Tukio zima la Korogwe.
 
Back
Top Bottom