Acheni kununa, hudhurieni uzinduzi wa mtambo wa kusafisha mafuta Kenya

tubalayya

Senior Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
117
Reaction score
203
'Wiki ijayo, Kenya itazindua ujenzi wa mtambo mkuu wa kusafisha mafuta ya petroli, dizeli, ya ndege nk huko Lamu, utakaosafisha mapipa 700,000 kwa siku. Huu utakuwa mtambo wa pili mkubwa zaidi barani kote Afrika

Rais wa Kenya Samuel Samoei Ruto alitangaza hayo kwenye mimbari ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Ghafla nikaikumbuka nchi yangu Tanzania na jinsi ilivyokosa fursa hiyo, ambayo ilikuwa ni haki yake bila mpinzani, lau si kutojipanga, ovyo-ovyo, na 'imbecility' ya viongozi wetu.

Tanzania inapakana na nchi 9 ukiihesabu pia Comoro. Zote ni nchi tulivu zinazoendelea kwa haraka ukitoa DRC. Lakini hata hiyo DRC ni nchi tajiri zaidi kwa rasilimali kuliko yoyote Afrika! Kwa vigezo hivyo tu, mwekezaji yeyote anayetazama mustakbali, angeichagua Tanzania bila hata ya kuhitaji kushawishiwa.

Kufananisha na Kenya inayopakana na nchi dhaifu zenye migogoro tele. Hata ukiihesabu Ethiopia, ambayo kidogo ndiyo nchi yenye matumaini....lakini haiishi migogoro. Hivi niandikavyo huenda waasi wakaingia mji Mkuu Addis Ababa wakati wowote ule!
Ni mwekezaji kichaa pekee ndiye angeichagua Kenya katika uwekezaji mkubwa namna hiyo, juu ya Tanzania.

Lakini Tanzania yetu inaugua. Hata ningekuwa Mimi nisingethubutu kuwekewa dola bilioni 16 (Robo ya bajeti nzima ya mwaka ya Tanzania)!
Hakuna kitu anachokithamini mwekezaji- asiyekuwa Mchina- kama ' rule of law and discipline' mamlaka ya Sheria na nidhamu. Nchi ambayo Sheria zaweza kutungwa, Mawaziri waweza kuapishwa na kutenguliwa kwa saa chahe...mtu aweza kuwa huru asubuhi, akawa mfungwa mchana... Ji CCM laweza kukukalia kooni hadi umpe atakacho ndipo uweze kufanya lililo haki yako, hata kama ni kuwasaidia Watanzania (nakumbuka kisa cha rafiri yangu Mmisri aliyetaka kuweka kiwanda cha kuchakata matunda kuwasaidia wakazi wa Kijiji chenye maembe yanayooza barabarani wakati wa msimu, akaombwa mrungula zaidi ya bei ya kiwanda chenyewe)!.

Siyo hivyo tu. Nchi yenye uhaba mkubwa wa 'quaified manpower' kutokana na mfumo wa Elimu yetu (hii human capacity ni muhimu kwa muwekezaji hata kuliko ukubwa au udogo wa Kodi)! na zaidi ya hayo, nchi ambayo sasa mustakbali wake hautabiriki

Nimeamua kuandika hii ili tu niwape viongozi wetu somo juu ya 'diplomacy, regional relationships na politics' kutokana na nilicchokiona baada ya Dangote kukaa kuwekeza Tanzania. Kwamba badala ya viongozi wetu kujiangalia upya na kujitathmini kwa kujiuliza wapi tumekosea, wao walijibu kama ajibuvyo mtoto mdogo aliyenyimwa pipi na mamaye......'kununa'! Hicho ndicho walichokifanywa na kukivisha haraka haraka vazi la makubaliano ya kujenga kijimtambo kidooogo na Uganda!

Jambo la kitoto sana. Hata mtambo huo ukijengwa, hauwezi kutosheleza hata mahitaji ya siku ya Tanzania pekee! Pengine itabidi wavuke Ghuba na kuupita mtambo wa Kenya, ili kununua mafuta ya 'kujazilia'!
Ndipo ujue siasa zetu haziongozwi na watu 'mature'.

Kwa nini nawataka viongozi wa Tanzania wawepo kwenye hafla ya kuzindua ujenzi kule Lamu, tena ikibidi waombe hasa waruhusiwe kuwa huko:

1. Wataonekana wamekomaa na hawayumbishwi na hisia

2.Utarudisha uhusiano wetu na Kenya ulioingia kakasi kwa hil

3. Dangote, ambaye ameahidi kujenga kiwanda cha mbolea Tanzania, atahisi ana dhima ya kutekeleza mradi huo, badala ya kuona anakwamishwa kwa vile amekataa Tanzania (Kama tuna viongozi wenye akili, wangeweza kushikilia zaidi huu mradi wa kiwanda cha mbolea na wakamshawishi ajenge kikubwa zaidi cha kutosheleza mahitaji ya nchi zote za Kusini mwa Afrika.

Kumbuka, mafuta ya petroli pengine uhai wake ni miaka 50 tu kutoka SASA, baada ya hapo aidha hayatahitajika sana, au hayatahitajika kabisaa. Wakati mahitaji ya mbolea ni hadi hapo Mamlaka ya Bwana yafike!
 
A forum user, tubalayya, expresses disappointment that Kenya, not Tanzania, is set to build Africa's second-largest oil refinery in Lamu, capable of refining 700,000 barrels per day. The author attributes Tanzania's missed opportunity to poor planning and the "imbecility" of its leaders.

The user argues that Tanzania is a far more attractive investment destination due to its nine stable, rapidly developing neighboring countries, compared to Kenya's conflict-prone borders. However, the core reason for Tanzania's failure to attract such investments, according to the author, is the lack of "rule of law and discipline." The post cites examples of arbitrary law changes, swift ministerial appointments and removals, sudden arrests, and rampant corruption/extortion by the ruling party (CCM) as major deterrents for investors (especially non-Chinese ones), despite Tanzania's geographical advantages.
 
Hapa tulichezea shilingi chooni Ruto is very smart alishanusa huu utajiri na ilikuwa tuu plan yakupanga karata na alifanikiwa tunafelishwa sana na hatuna watu wakuplan hususani wizara ya uwekezaji tunahang hang tuu kwenye kilimo tuu tumekwama.
 
inawezekana hata kwa tanzagiza huo mradi ulipigwa chini na cartel wa kusamabaza na kuuza mafuta wanaoagiza mafuta na kusambaza nchi nzima mpaka nchi jirani, kuwa na refinery ni tishio kwao kwani ingebadilisha game kabisa baada ya kukamilika, hivyo kuna uwezekano mkubwa wameipiga chini kwa makusudi hapa tanzagiza ...
 
Kenya Ina migogoro gani wana Tume angalu nzuri na katiba hata UN wanajenga offce zao kenya hujui?
 
inawezekana hata kwa tanzagiza huo mradi ulipigwa chini na cartel wa kusamabaza na kuuza mafuta wanaoagiza mafuta na kusambaza nchi nzima mpaka nchi jirani, kuwa na refinery ni tishio kwao kwani ingebadilisha game kabisa baada ya kukamilika, hivyo kuna uwezekano mkubwa wameipiga chini kwa makusudi hapa tanzagiza ...
Hili lina make sense 100%
 
'Wiki ijayo, Kenya itazindua ujenzi wa mtambo mkuu wa kusafisha mafuta ya petroli, dizeli, ya ndege nk huko Lamu, utakaosafisha mapipa 700,000 kwa siku. Huu utakuwa mtambo wa pili mkubwa zaidi barani kote Afrika

Rais wa Kenya Samuel Samoei Ruto alitangaza hayo kwenye mimbari ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Ghafla nikaikumbuka nchi yangu Tanzania na jinsi ilivyokosa fursa hiyo, ambayo ilikuwa ni haki yake bila mpinzani, lau si kutojipanga, ovyo-ovyo, na 'imbecility' ya viongozi wetu.

Tanzania inapakana na nchi 9 ukiihesabu pia Comoro. Zote ni nchi tulivu zinazoendelea kwa haraka ukitoa DRC. Lakini hata hiyo DRC ni nchi tajiri zaidi kwa rasilimali kuliko yoyote Afrika! Kwa vigezo hivyo tu, mwekezaji yeyote anayetazama mustakbali, angeichagua Tanzania bila hata ya kuhitaji kushawishiwa.

Kufananisha na Kenya inayopakana na nchi dhaifu zenye migogoro tele. Hata ukiihesabu Ethiopia, ambayo kidogo ndiyo nchi yenye matumaini....lakini haiishi migogoro. Hivi niandikavyo huenda waasi wakaingia mji Mkuu Addis Ababa wakati wowote ule!
Ni mwekezaji kichaa pekee ndiye angeichagua Kenya katika uwekezaji mkubwa namna hiyo, juu ya Tanzania.

Lakini Tanzania yetu inaugua. Hata ningekuwa Mimi nisingethubutu kuwekewa dola bilioni 16 (Robo ya bajeti nzima ya mwaka ya Tanzania)!
Hakuna kitu anachokithamini mwekezaji- asiyekuwa Mchina- kama ' rule of law and discipline' mamlaka ya Sheria na nidhamu. Nchi ambayo Sheria zaweza kutungwa, Mawaziri waweza kuapishwa na kutenguliwa kwa saa chahe...mtu aweza kuwa huru asubuhi, akawa mfungwa mchana... Ji CCM laweza kukukalia kooni hadi umpe atakacho ndipo uweze kufanya lililo haki yako, hata kama ni kuwasaidia Watanzania (nakumbuka kisa cha rafiri yangu Mmisri aliyetaka kuweka kiwanda cha kuchakata matunda kuwasaidia wakazi wa Kijiji chenye maembe yanayooza barabarani wakati wa msimu, akaombwa mrungula zaidi ya bei ya kiwanda chenyewe)!.

Siyo hivyo tu. Nchi yenye uhaba mkubwa wa 'quaified manpower' kutokana na mfumo wa Elimu yetu (hii human capacity ni muhimu kwa muwekezaji hata kuliko ukubwa au udogo wa Kodi)! na zaidi ya hayo, nchi ambayo sasa mustakbali wake hautabiriki

Nimeamua kuandika hii ili tu niwape viongozi wetu somo juu ya 'diplomacy, regional relationships na politics' kutokana na nilicchokiona baada ya Dangote kukaa kuwekeza Tanzania. Kwamba badala ya viongozi wetu kujiangalia upya na kujitathmini kwa kujiuliza wapi tumekosea, wao walijibu kama ajibuvyo mtoto mdogo aliyenyimwa pipi na mamaye......'kununa'! Hicho ndicho walichokifanywa na kukivisha haraka haraka vazi la makubaliano ya kujenga kijimtambo kidooogo na Uganda!

Jambo la kitoto sana. Hata mtambo huo ukijengwa, hauwezi kutosheleza hata mahitaji ya siku ya Tanzania pekee! Pengine itabidi wavuke Ghuba na kuupita mtambo wa Kenya, ili kununua mafuta ya 'kujazilia'!
Ndipo ujue siasa zetu haziongozwi na watu 'mature'.

Kwa nini nawataka viongozi wa Tanzania wawepo kwenye hafla ya kuzindua ujenzi kule Lamu, tena ikibidi waombe hasa waruhusiwe kuwa huko:

1. Wataonekana wamekomaa na hawayumbishwi na hisia

2.Utarudisha uhusiano wetu na Kenya ulioingia kakasi kwa hil

3. Dangote, ambaye ameahidi kujenga kiwanda cha mbolea Tanzania, atahisi ana dhima ya kutekeleza mradi huo, badala ya kuona anakwamishwa kwa vile amekataa Tanzania (Kama tuna viongozi wenye akili, wangeweza kushikilia zaidi huu mradi wa kiwanda cha mbolea na wakamshawishi ajenge kikubwa zaidi cha kutosheleza mahitaji ya nchi zote za Kusini mwa Afrika.

Kumbuka, mafuta ya petroli pengine uhai wake ni miaka 50 tu kutoka SASA, baada ya hapo aidha hayatahitajika sana, au hayatahitajika kabisaa. Wakati mahitaji ya mbolea ni hadi hapo Mamlaka ya Bwana yafike!
Hii nchi shida Sana,
Wenzetu wanazindua refinery kubwa, huku kwetu, mkuu wa majeshi anaenda kuzindua eti ukumbi wa kufanyia sherehe! Na, kwa upeo wa akili yake anaona ni jambo LA maana Sana, hizi, ni, biashara za kufanywa na kina niffer! Sio taasisi kubwa!
Nchi yetu inadogoshwa na ufinyu wa akili na upeo wa viongozi, wanaoongoza taasisi,
Kizimkazi, kwake heshima binafsi ni Bora kuliko nchi! Sasa lipo limejifungia kizimkazi eti kisa,EDA, Mambo ya islamic rituals na geopolitics wapi na wapi! Inatia kichefu chefu
 
Back
Top Bottom