RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
MHADHARA (87)
👁️Ewe mwanaume;
Kama huna lengo la kuzaa usimpe mimba mwanamke, kama utampa mimba mtunze/tunzaneni. Ikiwa utampa mimba mwanamke na kumtelekeza utamfanya ateseke, pia utamtenganisha na fursa nyingi za maisha kwasababu ya muda mwingi atakuwa kwenye malenzi ya mtoto bila baba.
Changamoto wanazokumbana nazo wanawake za kulea watoto bila baba zao ndizo ambazo zinapelekea watoto wengi wanatupwa kwa bibi zao. Nasema "wanatupwa" kwasababu hakuna matunzo yoyote yanayopelekwa huko. Baba amemtelekeza mama na mtoto, na mama naye anamtelekeza mtoto kwa bibi yake.
Watoto wengi wanaotupwa kwa bibi zao wanakumbana na maisha magumu mno kwasababu bibi zao pia wana maisha magumu. Matokeo ya ugumu huo ndio chanzo cha wizi, ukabaji, kubakwa, kulawitiwa, kuuawa, omba omba, na rundo la watoto wa mtaani.
Mimba sio ugonjwa kama kwamba inakuja bila kutarajia, ikiwa unapanda mbegu safi ardhini tegemea mbegu kuota. Kama imetokea mimba ambayo mnadhani hamkuitarajia basi mnapaswa kushikamana pamoja.
👁️Ewe Mwanamke;
Kumtelekeza mwanao kwa bibi yao (mama yako) ilhali unajua kuwa mama yako ana maisha magumu ni kumfanya mwanao apitie magumu sana.
RIGHT MARKER
Dar es salaam.