Acheni tu huyu Dotto Magari aendelee Kutudharau Sisi Wasomi wa Tanzania na ninakubaliana nae kwa 100%

Kama jobless simu ya 5m kaitoa wapi? Wazazi waweza kuwa na pesa wakampa hawataki mtoto wao apate shida hata kama jobless
Wazazi hawataki mtoto wao apate shida! wakamsomesha mpaka chuo ili asipate shida then wakamnunulia simu ya 5m huku anakaa home kula kulala.

Kuzurula kutwa kutafuta ajira kwa kazi ya 9k th?!

Mimi ukinipa simu ya thamani hiyo leo, kesho naiuzaa!
 
Wazazi hawataki mtoto wao apate shida! wakamsomesha mpaka chuo ili asipate shida then wakamnunulia simu ya 5m huku anakaa home kula kulala.

Kuzurula kutwa kutafuta ajira kwa kazi ya 9k th?!

Mimi ukinipa simu ya thamani hiyo leo, kesho naiuzaa!
Shida nini kwani ?

Kitanda analalia cha milioni 10

Kwa hiyo kama hana ajira na mzazi ana pesa kwa hiyo alale kwenye mkeka wa elfu moja na simu awe na Nokia torch ?

Pole kwa kuzaliwa familia maskini ambako wanaona simu ya milioni 5 ni Big deal

Watoto wa wenye nazo unakuta hana ajira na mzazi kumnunulia gari ya milioni 80.ya kutembelea anapoenda kutafuta kazi au interview anajaziwa mafuta

Kuwa hana kazi ndio aishi kimaskini wakati familia tajiri haiwezekani itakuwa kushusha hadhi ya familia na watu nje kuona mtoto ananyanyaswa kisa hana kazi

Lazima aishi maisha standard ya level ya utajiri wa familia hata kama ni jobless
 
Na haandamani
 
Elimu kwa mtoto wa don ni kama burudani ni extra tu.
 
Hilo jambo niliwahi kuliona kitambo sana.

Wabongo wanapenda sana simu na magari.

Unakuta ana mshahara mdogo lakini ana simu ya gharama kubwa sana.

Au unakuta kapanga lakini ana gari la milioni 30;

Sasa unajiuliza badala ya kununua gari la milioni 30 wakati umepanga si bora ununue kiwanja na kupandisha mjengo?

Kawaida sana kwa wabongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…