Acheni tu huyu Dotto Magari aendelee Kutudharau Sisi Wasomi wa Tanzania na ninakubaliana nae kwa 100%

Acheni tu huyu Dotto Magari aendelee Kutudharau Sisi Wasomi wa Tanzania na ninakubaliana nae kwa 100%

"Wasomi nikiwa nawasema Kutwa msiwe mnanichukia kwani nawatoeni Ushamba na nawafundisha jinsi ya Kufikiri. Unakuta Msomi ananunua Simu aina ya Iphone 15 yenye Thamani ya Shilingi Milioni Tano halafu unakuta amepakuwa App ya Bolt. Sasa kwanini hiyo Shilingi Milioni Tano yako usingenunua tu Pikipiki ya Shilingi Milioni Mbili iwe inakupeleka unakokenda Kutwa na hiyo Shilingi Milioni Tatu ukanunu hata Kiwanja mahala kuliko kutafuta Sifa za Kijinga uonekane una Simu Kali wakati Akili huna?"amesema Influencer Dotto Magari.

Hakuna Mtu GENTAMYCINE namkubali kama Dotto Magari, kwani anachokisema Kwetu Wasomi yuko sahihi 100% zote.
Huu bdio ukweli ambao wasomi wengi hatupendi kusikia, perfect !

Watakwambia kila mtu ana vipaumbele vyake lakini lazima ukweli usemwe.
 
Logic za masikini hua unaziamini?😄
Mnapewa logic za Maisha na Doto magari,kweli elimu haijawakomboa
Ukienda kwenye nyumba ya ibada ukaambiwa tenda mema ili mwisho wa siku usichomwe moto, wale wanaosema hayo maneno kwako quote vifungu vya maandiko.

Je una uhakika wao huwa wanayafuata na kuyaishi hayo wanayo yafundisha?

Je, kwanini unaita logic za masikini?

Je mtu yeyote mwenye elimu hapaswi kujifunza jambo jipya ”japo” kutoka kwa mtu asie na elimu?

Kwamba mtu masikini hawezi kutoa hoja yenye mashiko?
 
"Wasomi nikiwa nawasema Kutwa msiwe mnanichukia kwani nawatoeni Ushamba na nawafundisha jinsi ya Kufikiri. Unakuta Msomi ananunua Simu aina ya Iphone 15 yenye Thamani ya Shilingi Milioni Tano halafu unakuta amepakuwa App ya Bolt. Sasa kwanini hiyo Shilingi Milioni Tano yako usingenunua tu Pikipiki ya Shilingi Milioni Mbili iwe inakupeleka unakokenda Kutwa na hiyo Shilingi Milioni Tatu ukanunu hata Kiwanja mahala kuliko kutafuta Sifa za Kijinga uonekane una Simu Kali wakati Akili huna?"amesema Influencer Dotto Magari.

Hakuna Mtu GENTAMYCINE namkubali kama Dotto Magari, kwani anachokisema Kwetu Wasomi yuko sahihi 100% zote.

Anatudharau sababu toka tujue ili mambo yetu yaende lazima kuwa chama dola, tumekuwa kama zombies 😂 😂 😂. hata kufikiria hatutaki tena. Tunasubiri huruma ya kiboko ya wachawi ili tuokolewe 😂
 
Yaani unamiliki simu ya 5m unatembea kwa miguu!!
Tatizo lenu mnaangalia jambo moja tu, yaani item moja tu simu!

Je wanaohonga pakubwa na kula padogo mbona hamuwasemi?

Mtu anajengea hawara, wakati bado akiishi pangoni!

Wanaume wapumbaf ni wengi kuliko tunavyodhania.
Hao wa simu ghali na huku wakiishi maisha ya hovyo wana nafuu kwa sababu angalao wanamiliki hata hicho kitu.

Kuliko wanaotumikia kichwa cha chini 99% ya mapato yao hadi wanazeeka na kukosa uelekeo.
 
Back
Top Bottom