Acheni tu Joti abomolewe nyumba, alikebehi sana watu kwenye kipindi chao

Machudaa

Senior Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
123
Reaction score
311
Unajua akina Joti wameumiza watu na kuwaathiri kisaikolojia kwa kile kipindi chao infamous KUFULIA. Walizidi sana hadi walipigwa stopu. Lunyamila hana ugomvi na mtu wakamuigiza kafulia. Eti Vengu ndie Lunyamila sasa hivi jamaa anaumwa yuko kitandani.

Walishamuigiza mama Asma kadogo (taarab)kafulia ilibaki wairushe hewani
akafariki wiki iyo iyo ikabidi waifute. Bila aibu Mc Regan likahudhuria msibani na yeye ndie aliigiza kama Asma.

Na wabongo wanavyopenda umbea na watu kufulia yani kipindi kilikuwa maarufu sana.

Muosha uoshwa. Sasa nalo linavunjiwa nyumba bila fidia.

Hii hapa chini ni video moja tu ya kipekee ambayo ipo youtube ya kipindi cha hovyo kabisa Kufulia walivyomdhalilisha Muumin Mwinjuma kocha wa dunia.

Mods msiunganishe uzi


Orijino komedi na umefulia - YouTube
 
Hawa majamaa licha ya kuwadhalilisha watu pia walichangia sana Sizonje kuingia mjengoni...nakumbuka wakiwa uwanja wa Kambarage walimpigia sana debe na kuigiza kuwa Lowassa ni mgonjwa,hawakuwajua kuwa jini huwa halina urafiki na mwanadamu!
 
As if akivunjiwa wewe utapata nafuu ya maisha!

Huwezi kufanikiwa kwa kuwachukia waliofanikiwa. Wabongo tunapenda utajiri ila tunachukia matajiri.

By the way, unavunjwa ukuta (fence) na sio nyumba!
 
Kufulia kila mtu anaweza kufulia tu sio dhambi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…