Acheni tu taarabu ni tamu, na zinafunza jamii haswaa!

Acheni tu taarabu ni tamu, na zinafunza jamii haswaa!

Kazi kweli kweli! Heaven kwa mashairi hayo uliyokariri ukigombana na mtu si atajificha au ni tofauti na uhalisia wako.
"Kwanza tuheshimianee, mimi nawe hatushei mume walau nikudiscuss. Uongo tusizuliane na vibaya usiniseme ukanitilia nuksi". Afu pale sasa "una hamu nikuseme, nikikusema utaliaaa, una hamu nikuchambe, nikikuchamba utazimiaaa"

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Haloooooooooo!!!!!!!!!!!! mashairi siyajui vizuri lakini napenda,,,,
kitanda kidogo eee chanibana bana nataka kulala na bwana raha zikizidi tutaangusha!!!!!!!

hii mistari yanikosha pia,,,,,,,,,,;
nimerudi kwa muadhama aaaa pesa roho wa mapenzi mmmmmh!!!!!
kwenu nimekwisha hama aaaaaaaa mmeshindwa kunienzi iiiiiiiiiiiiiiii huku nna lishwa nyama ya mishkaki ya mbuzi

Tina Tina Tina na pesa!!! we haya wee!
 
Kuna lile song la Mzee Yusuph...ndani yake kuna maneno kama 'kanishika hapa kanishika pale....'

Ule wimbo una maneno ya mahabati sana

hahahahaaa watu8 umenikosha nimeipendaje, hebu rudia tena!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hahaaaaa yami mm nikiona mwanaume anapenda tarabu najua ni chakla tu
 
hapa ni jukwaa ka taarabu sio

Njiwa peleka salamuu

Aaa kwa yule wangu muhibu,

CC DEMBA
 
Last edited by a moderator:
Inaitwa modern taarab bwana, za zamani ni classical

Analotaka Razaki,katu halirudi nyumaa
Yenu ni kuliafiki,sharia itasimama
Ni bure kunidhihaki,na kunijaza lawama
Midomoni sibanduki,waja hamwishi kusema
Mimi kupewa riziki vipi roho zawaumaaa
Mpewa hapokonyeki muelewe wanadama

My favourite
 
"Kwanza tuheshimianee, mimi nawe hatushei mume walau nikudiscuss. Uongo tusizuliane na vibaya usiniseme ukanitilia nuksi". Afu pale sasa "una hamu nikuseme, nikikusema utaliaaa, una hamu nikuchambe, nikikuchamba utazimiaaa"

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

domo la udaku joha kassim huyo
 
"Aaaa Mungu kanipa kauli nzuri niongee na watu kwanini wasinipendeeeee"

Msiniite mswahili japo mie mtanzania nazungumza kiswahili na kiswahili asili yangu. Wanajamii taarabu zinamafunzo kweli kweli na huwa hazichoshi kusikiliza. Mfano huyu mdada Leyla Rashidi verse zake zimeenda shule sana.

"Kizingiti cha manani ni mtihani kwa mja, hata uwe mashakani usisite kumtaja"

"Kauli ya molaaaaaaa silaha nzitoooo alipangalo ndilo litakuwaaaa"

Leyla Rashid & Jahazi Modern Taarab - Fungu La Mungu Sikosi - YouTube.


Hivi mnikumbushe na ule wa marupe rupe ndio unasemaje vile?

CC

Wapenzi wenzangu wa nyimbo za mwambao

Nimesoma kichwa cha habari nikaja spiiiiid karibu nijikwae nikidhani mambo yetu yale ya Mombasa!!! Arrrghhh!

"Njiwa peleka salaam........."
 
Kazi kweli kweli! Heaven kwa mashairi hayo uliyokariri ukigombana na mtu si atajificha au ni tofauti na uhalisia wako.

Hapana jamani, napenda tu taarabu, ugomvi ht siuwezi et

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hahahahahah dada Mrembo by Nature mie naja na hiii ya mwanahawa ally


Umaskini wangu haunipi tahayuri
Bure mkinikebekhi ni ya mola takadiri
Mimi sizijali stihizai zenu walimwengu
Katu sitobadilika nikauza utu watu....

Nna amini kupata na kukosa ni jaala yake mungu
Sizijali istihizai zenu walimwengu
sitodhalilika nikauza utu wangu

Natangaza hadharani nimekinai
Nimekinai umaskini wangu
Naapa sitodhalilika nikauza utu wangu

Japo mimi maskiniiii
Kwani lipi la ajabu
Nimeumbwa nimeumbwa
Hakuna mtimilifu sote ni waja wa mungu

Yake mola mtihaniii
Ntapasi naamini
Siinyongi roho yangu
Inshaallah mola muweza atanipa langu fungu.
 
Last edited by a moderator:
Mweenye maneno mengi, huwa namuangalia, wala ubaya sijengi, pote nampotezeaaaaa

Lolote lile watakutafutia, ili upate upige kelele, miye mdomo sitaufunua, ndo kawaida milele. Wajinga wajinga nawapotezea katu hawanipigishi kelele, binadamu ndo wamezoea, kuzusha hili na lile.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Analotaka Razaki,katu halirudi nyumaa
Yenu ni kuliafiki,sharia itasimama
Ni bure kunidhihaki,na kunijaza lawama
Midomoni sibanduki,waja hamwishi kusema
Mimi kupewa riziki vipi roho zawaumaaa
Mpewa hapokonyeki muelewe wanadama

My favourite

Hahahahaha waapeee
 
Back
Top Bottom