tinna cute
JF-Expert Member
- Sep 22, 2013
- 4,630
- 2,308
Hasara roho.....pesa makaratasi lol
Hahahahaha waapeee
Hahahahahah dada Mrembo by Nature mie naja na hiii ya mwanahawa ally
Umaskini wangu haunipi tahayuri
Bure mkinikebekhi ni ya mola takadiri
Mimi sizijali stihizai zenu walimwengu
Katu sitobadilika nikauza utu watu....
Nna amini kupata na kukosa ni jaala yake mungu
Sizijali istihizai zenu walimwengu
sitodhalilika nikauza utu wangu
Natangaza hadharani nimekinai
Nimekinai umaskini wangu
Naapa sitodhalilika nikauza utu wangu
Japo mimi maskiniiii
Kwani lipi la ajabu
Nimeumbwa nimeumbwa
Hakuna mtimilifu sote ni waja wa mungu
Yake mola mtihaniii
Ntapasi naamini
Siinyongi roho yangu
Inshaallah mola muweza atanipa langu fungu.
Mwenzenu nimepagawa
Besti kumbe nawe wamo eenh....
Nipe nipe ukinipa bure mi ntalewaaa...
Ulipotoka kwenu
bwigiri, sisi tulikupokea wewe, na vibahasha vya hirizi, shingoni
umevivaa. Ukafundishwa vivazi wewe na kitanda ukapewa wewe, wajifanya
siku hizi, wajifanya unajuaaa. Mdomo umeuchonga wajifanya unajua by
khadija kopa
Achia ngazi bibi mchuma unaondoka huo, achia ngazi bibi mchuma unaondoka
huo. Umeshachelewa naondoka naye umeshaishiwa nina dunda naye. Kipi cha
kung'ang'ania hakutaki ebu timu, mtu mzima hovyo unajieshua mtu mzima
hovyo unajieshua
Huna lolole hutonibabaisha, nenda usojijua, huna lolote
hutonishughulisha nenda usojijua. Huna sura huna mwili vimekutoka
vibavu, utavaaje kimini na usafiri mbovuuuu
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
"Aaaa Mungu kanipa kauli nzuri niongee na watu kwanini wasinipendeeeee"
Msiniite mswahili japo mie mtanzania nazungumza kiswahili na kiswahili asili yangu. Wanajamii taarabu zinamafunzo kweli kweli na huwa hazichoshi kusikiliza. Mfano huyu mdada Leyla Rashidi verse zake zimeenda shule sana.
"Kizingiti cha manani ni mtihani kwa mja, hata uwe mashakani usisite kumtaja"
"Kauli ya molaaaaaaa silaha nzitoooo alipangalo ndilo litakuwaaaa"
Leyla Rashid & Jahazi Modern Taarab - Fungu La Mungu Sikosi - YouTube.
Hivi mnikumbushe na ule wa marupe rupe ndio unasemaje vile?
CC
Wapenzi wenzangu wa nyimbo za mwambao
Alokupa kiti wewe cha kukalia,kumbi akanipa mimi
Ni Mungu si mwenginewe usijitie tafrani,na kunitoa thamani
Kwa vipi unibeue mara juu mara chini,humkumbuki manani
Chuki ziondoe kwangu yatizame yalo yako
Sabah Salum Muchacho
Aahahhaha wacha niendelee na ya mwahawa ally...
Japo mimi masikiniiiii
Katu sijiweki nyuma
Sababu naziamini
Rehema zake karima
Ipo siku ntawini
Mtanyamaza kusema
Ntamegewa na mimi
Zilizo njema rehema
Kwakua maajaaliwa yake rabana
Yake rabana siweki fundo moyoni
Yeye ndie anaetoa humoa amtakae
Wala hajamuonea yule mja akosae
Hana hiyama manani
Napaa sitokufuru nikakesha ugangani
Nipatacho nashukuruuuu
Ndio riziki yangu ilopangwa ardhini
Kanifariji afuru saada na suudi zake
Umaskini haunidhuru wala haunipi joto
Roho tanda nimepoa
Kwa kipi nidhalilike
Aahahhaha wacha niendelee na ya mwahawa ally...
Japo mimi masikiniiiii
Katu sijiweki nyuma
Sababu naziamini
Rehema zake karima
Ipo siku ntawini
Mtanyamaza kusema
Ntamegewa na mimi
Zilizo njema rehema
Kwakua maajaaliwa yake rabana
Yake rabana siweki fundo moyoni
Yeye ndie anaetoa humoa amtakae
Wala hajamuonea yule mja akosae
Hana hiyama manani
Napaa sitokufuru nikakesha ugangani
Nipatacho nashukuruuuu
Ndio riziki yangu ilopangwa ardhini
Kanifariji afuru saada na suudi zake
Umaskini haunidhuru wala haunipi joto
Roho tanda nimepoa
Kwa kipi nidhalilike
Wewe bongo star search inakuhusu sana, naamini sautiyo ipo mulemule.
Seleleaaaa...
Cheza na mimi mpenzi...cheza nami kwa henezi mambo mazuri ya habibi ndo hayataki haraka!!
We kwa vibwagizo tu nakupa heko he he he!!Nakupendaaaa
Nakupendaaa yaa habibi seleleaa
Mmekosa kazi
We kwa vibwagizo tu nakupa heko he he he!!
Mmekosa kazi