Acheni tu taarabu ni tamu, na zinafunza jamii haswaa!

Acheni tu taarabu ni tamu, na zinafunza jamii haswaa!

Hahaaaaa siutani mwangu nimemchomekea mmoja kajajuu tarabu si kwa mwanaume bana
 
Taarab ile ya Zanzibar bana..kama sijasahau walikuwa wanaitwa The Voice of Zanzibar.
 
Nazichukia sn taarabu.
Hata nikifika ghafla nyumbani nikikuta wanasikiliza wanawahi kuzima fasta.
Mimi nahisi taarabu kama vile kuwasimanga majirani zangu, na nishawahi kuvunja cd za mpenda taarabu nyumbani mwangu!

Ila uwongo mbaya nikisikia maneno kwenye wimbo fulani wa taarabu yanasema UMEKUNYWA SODA ZANGU... UTANIBEBA LEO!...natamani yaendelee hayo tu!...huko kwingine kunakoendelea sikupendi!
 
"Jua ulianza ufizi ndio meno yakajaaaaaaa, namuamini mwenyezi ndio nguzo ya hajaaaaaaa"

Taarab ni music mzuri mno!Travetine Magomeni nilipelekwa mwaka huu kuangalia Taarab kwa mara ya kwanza toka nizaliwe;Kwa kweli nakiri nimepitwa na mengi kwenye music huu!Yule Mzee Yusuf anajua taarab!
Mrembo by Nature wapi naweza pata collection ya taarab za zamani kama vile sikutegemea kama ww una mambo; Sanamu la Michelin;Mambo ipo huku;utalijua Jiji;Nafanya hesabu sipati jawabu(kuruka ukuta);Muhogo wa Jang'ombe na zinginezo nimpe dada yangu kama zawadi bday yake maana yy anapenda mno taarab!

Mm nipo Ikolo-Kyela na kama inawezekana wasiliana na DEMBA tujue bei na malipo yake na how tutapata huo mzigo!

CC DEMBA
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo Mzee Yusuph humuelewi..?

Hata mm nikikuwa nashangaa sana mwanamme kupenda taarab lkn nilipo pelekwa nikajua nimepitwa na raha nyiingi sana!

Taarab nzuri sana hasa wale madada waitikiao wanajua sana kuchezesha miili yao!Walahi mm mshamba wa Kyela nikawa najichekea tu nawatumbulia macho!

Ngalikihinja hawa watu wa Bara kaka hawampendi Mzee Yusuf ahahaha!
 
Last edited by a moderator:
Binaadam wenzangu wananichukia
Sina ubaya rohoni mwangu wananishuhudia
Mama nipe radhi binadamu hawana wema
Kila nifanyalo hawaachi kunisema
 
Taarabu za zamani bana

Ni bure zenu fitina, si wala hatuachanani
Wenyewe tumependana, kuachana ni muhali

Konnie hebu nikumbushe mashairi ya ule wimbo wa "Sina mimi sina, mwengine zaidi yako" nadhani mwimbaji alikuwa ni Bi Nasma Khamis Kidogo R.I.P

Kuna siku niliona weye na mtani wangu snowhite mwabadilishana maneno ya hilo jisongi...
 
Last edited by a moderator:
"Aaaa Mungu kanipa kauli nzuri niongee na watu kwanini wasinipendeeeee"

Msiniite mswahili japo mie mtanzania nazungumza kiswahili na kiswahili asili yangu. Wanajamii taarabu zinamafunzo kweli kweli na huwa hazichoshi kusikiliza. Mfano huyu mdada Leyla Rashidi verse zake zimeenda shule sana.

"Kizingiti cha manani ni mtihani kwa mja, hata uwe mashakani usisite kumtaja"

"Kauli ya molaaaaaaa silaha nzitoooo alipangalo ndilo litakuwaaaa"

Leyla Rashid & Jahazi Modern Taarab - Fungu La Mungu Sikosi - YouTube.

Hivi mnikumbushe na ule wa marupe rupe ndio unasemaje vile?

CC

Wapenzi wenzangu wa nyimbo za mwambao

Samahani dada naomba kama una Full stop wa Khadija Kopa uniwekee hapa, si mpenzi wa Taarabu lakini huu wimbo nimetokea kuupenda mbaya

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nazichukia sn taarabu.
Hata nikifika ghafla nyumbani nikikuta wanasikiliza wanawahi kuzima fasta.
Mimi nahisi taarabu kama vile kuwasimanga majirani zangu, na nishawahi kuvunja cd za mpenda taarabu nyumbani mwangu!

Ila uwongo mbaya nikisikia maneno kwenye wimbo fulani wa taarabu yanasema UMEKUNYWA SODA ZANGU... UTANIBEBA LEO!...natamani yaendelee hayo tu!...huko kwingine kunakoendelea sikupendi!

pijei umekuwaje siku hizi??ha ha ha umenchekesha kweli eti umekunywa soda zangu utanibeba leo ha ha ha mi napenda kama gari gari lako nitapanda daladala ha ha ha
 
halo halo haloooooooooooo wapi Zinduna !!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Sina mimi sina, mwingine zaidi yako weweeee
Sina mimi sina, atakayekushinda weweeeee

Ni wewe hakuna mwingine anipendezaye
Wala kulingana nawe simuoni huyooo *2
Ni wewe peke yako unitoshayeee

Back
Top Bottom