Acheni tu taarabu ni tamu, na zinafunza jamii haswaa!

Acheni tu taarabu ni tamu, na zinafunza jamii haswaa!

"Aaaa Mungu kanipa kauli nzuri niongee na watu kwanini wasinipendeeeee"

Msiniite mswahili japo mie mtanzania nazungumza kiswahili na kiswahili asili yangu. Wanajamii taarabu zinamafunzo kweli kweli na huwa hazichoshi kusikiliza. Mfano huyu mdada Leyla Rashidi verse zake zimeenda shule sana.

"Kizingiti cha manani ni mtihani kwa mja, hata uwe mashakani usisite kumtaja"

"Kauli ya molaaaaaaa silaha nzitoooo alipangalo ndilo litakuwaaaa"

Leyla Rashid & Jahazi Modern Taarab - Fungu La Mungu Sikosi - YouTube.

Hivi mnikumbushe na ule wa marupe rupe ndio unasemaje vile?

CC

Wapenzi wenzangu wa nyimbo za mwambao

aah basi wenzanguuuuu
huo si ujabariiiiiii
hayo ni maruperupeeee
nyinyi si mungu mpunguze wenu munkari naye mapepe e ee ee
kosa langu kukaaa nanyi vizuri ............
.................
Mrembo by Nature sijui ndi hivo, maana nausikiaga tu nahuwa unanivutia kuusikia
 
Last edited by a moderator:
aah basi wenzanguuuuu
huo si ujabariiiiiii
hayo ni maruperupeeee
nyinyi si mungu mpunguze wenu munkari naye mapepe e ee ee
kosa langu kukaaa nanyi vizuri ............
.................
Mrembo by Nature sijui ndi hivo, maana nausikiaga tu nahuwa unanivutia kuusikia

Ndio huu bwana, basi naupendaje
 
Kuna taarabu ilikuwa na jina la 'mtwangio', sikumbuki hata mwimbaji ni nani.
 
Taarab ni music mzuri mno!Travetine Magomeni nilipelekwa mwaka huu kuangalia Taarab kwa mara ya kwanza toka nizaliwe;Kwa kweli nakiri nimepitwa na mengi kwenye music huu!Yule Mzee Yusuf anajua taarab!
Mrembo by Nature wapi naweza pata collection ya taarab za zamani kama vile sikutegemea kama ww una mambo; Sanamu la Michelin;Mambo ipo huku;utalijua Jiji;Nafanya hesabu sipati jawabu(kuruka ukuta);Muhogo wa Jang'ombe na zinginezo nimpe dada yangu kama zawadi bday yake maana yy anapenda mno taarab!

Mm nipo Ikolo-Kyela na kama inawezekana wasiliana na DEMBA tujue bei na malipo yake na how tutapata huo mzigo!

CC DEMBA

Sina mpenzi, jeuri yangu youtube tuu wala sina hata collection yoyote
 
mie taarabu imenipitia pembeni.....ila huyu Patricia huwa ananikosha sanaaa.......
 
Hahahahahah dada Mrembo by Nature mie naja na hiii ya mwanahawa ally

Umaskini wangu haunipi tahayuri
Bure mkinikebekhi ni ya mola takadiri
Mimi sizijali stihizai zenu walimwengu
Katu sitobadilika nikauza utu watu....

Nna amini kupata na kukosa ni jaala yake mungu
Sizijali istihizai zenu walimwengu
sitodhalilika nikauza utu wangu

Natangaza hadharani nimekinai
Nimekinai umaskini wangu
Naapa sitodhalilika nikauza utu wangu

Japo mimi maskiniiii
Kwani lipi la ajabu
Nimeumbwa nimeumbwa
Hakuna mtimilifu sote ni waja wa mungu

Yake mola mtihaniii
Ntapasi naamini
Siinyongi roho yangu
Inshaallah mola muweza atanipa langu fungu.

Hahahaha wewe hata si masikini, sema tu ni swala la muda
 
Sio kusi kasikazi wema wangu bado,kwa neema yake jalari bahati haina siri muda wake ukifikia,muomba mungu kwa dhati husitirika,kila muomba mungu hatoki mtupu daima hata uwe sungusungu hata kunyima Bi mwanahawa ally weeeeee hapana chezea
 
Hewalaaaa...huu wimbo naukumbuka sana kwani enzi hizo za ujana wangu wenyewe tukijiita 'cheki bobu' basi kulikuwa na binti namsarandia akiitwa kwa jina Sina.

Sasa wimbo huu nilipotoa tu dedikesheni kwa binti Sina, ukawa umenirahisishia kazi ngumu ya tongozo (vijana wa zamani wanajua jinsi tongozo lilivyokuwa ni kibarua kigumu kama cha kuchuna ngozi ya kitimoto)...

Sina mimi sina, mwingine zaidi yako weweeee
Sina mimi sina, atakayekushinda weweeeee

Ni wewe hakuna mwingine anipendezaye
Wala kulingana nawe simuoni huyooo *2
Ni wewe peke yako unitoshayeee
 
Ha ha ha, vijana watajulia wapi wakati washarahisishiwa na instagram, fb na twira?

Ilikuwani kibarua cha miaka kabisa.

Hewalaaaa...huu wimbo naukumbuka sana kwani enzi hizo za ujana wangu wenyewe tukijiita 'cheki bobu' basi kulikuwa na binti namsarandia akiitwa kwa jina Sina.

Sasa wimbo huu nilipotoa tu dedikesheni kwa binti Sina, ukawa umenirahisishia kazi ngumu ya tongozo (vijana wa zamani wanajua jinsi tongozo lilivyokuwa ni kibarua kigumu kama cha kuchuna ngozi ya kitimoto)...
 
mi naipenda ninapokuwa kwenye mduara...afu mbele yangu kuna lijimama linanyonga mauno na liwowo lainiiii...,afu limama lenyewe liwe linajua kucheza mugongomugongo na kupekechapekecha km linabrashi via2 vile...!!
 
Ha ha ha!! sio kama vile maungo ya nyuma yanaporindima pale linaposugua kisigino baada ya kutoka kujikosha mwili kwenye mabafu yetu yale ya uani...

02.JPG
 
Back
Top Bottom