Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Naam tozo bado zipo tena nyingi tu. Jemadari wa tozo Field Marshal, mtaalam wa uchumi mwenye PhD, karudisha tu majeshi nyuma wakati mbinu za chini chini zikifanyika kuzikarabati zisiweze kutambulika kirahisi.
Kama kweli tozo zingefutwa hivi leo Kamanda Mkuu wa Tozo, aliyetutishia wananchi kama hatutaki tuwe wakimbizi Burundi, angekuwa mapumzikoni. Lakini hadi sasa yuko pale pale akipanga safu na mashambulizi mapya.
Tozo ilikuwa ni fursa iliyopambwa kama mwali na manyang'au yasiyo na chembe ya huruma kwa mateso tunayopitia wananchi. Ni bahati ilioje kuwa wapo wazalendo walioishtukia tozo na malengo yake.
Pamoja na vitisho, wazalendo hao hawakukaa kimya, walipaza sauti wakilia kwa uchungu wakipinga kuibiwa hata kile kidogo walichobakiza. Tozo ilikuwa ni udanganyifu, unyang'anyi na wizi wa mchana kweupee!
Ni wizi uliosimamiwa na wale wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza tukiwalipa mamilioni kupitia kodi zetu. Bado wakabuni mbinu ya kutukamua zaidi ili waweze kutembelea ma V8 za milioni mia tano kila moja.
Kwa kuwa Field Marshall bado yuko pale pale akiendelea na mipango yake endelevu, sasa ni lazima tuzidi kupaza sauti zetu. Yeye na tozo ni kama pete na kidole huwezi kuwatenganisha...kama ni kufa, lazima wazikwe pamoja!