Kwani tuna wabunge? Mbunge anatakiwa awe si mwakilishi tu bali mtetezi wa mwananchi. Kwa bahati mbaya tunalo Bunge linalopitisha sheria kandamizi ya kodi lakini wanahakikisha wao hawalipi kodi hizo.
Badala yake wanajilipa mamilioni kama posho kwa kutimiza wajibu wao bungeni na hiyo ni nje ya mishahara yao minono isiyolipiwa kodi. Ni hawa hawa Mwigulu aliwatumia kupitisha zoezi lake la wizi hivyo wote ni wezi.