Acheni Ushamba, Hakuna gari za kike wala za kiume

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,932
Reaction score
4,544
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa naona mada humu JF zikiwa zinaponda magari, kwamba magari kama Toyota Passo, Vitz, IST, Starlet, na n.k ni magari ya kike.

Naomba wote wanaoamini kuwa kuna magari ya kike watoe ushahidi, ni wapi ambako chombo cha moto kimeandikwa kuwa:

A Vehicle Special for females au for males?

Acheni Ushamba nyie watanzania ambao hamjui lolote ktk Dunia hii yenye mambo mengi na mazito.

Tanzania isiyotengeneza hata sindano eti wananchi wake wanadharau magari yanayotengenezwa nje na kuya Classify kuwa hili ni la kike na lile ni la kiume, huu ni ujuha wa hali ya juu.

Watanzania ambao hata kula yao ni shida kwa siku eti nao wanabagua magari, kwa lipi?

Ukienda, Japan, US, UK, Germany, Sweden na popote duniani ambako wanatengeneza magari, hawawezi kukuambia kuwa hili ni gari la kile na lile ni la kiume.

Siku zote maskini ni mtu anayejiona ni bora kuliko wote japokuwa hana lolote. Sasa wewe umehangaika ukapata vipesa vyako unanunua gari anakuja mjinga anakuambia ni la kike, wapi imeandikwa kuwa ni la kike, Ujinga uliokithiri.
 
ivi KE hawamiliki ndegeee, yaani nasikia Arusha mabilionea wanamiliki ndege ni Me, KE huwa hawapendi kumiliki ndege?????
 
Gari za kike ni zile zinazogaiwa bure tu kama zipo
kama gari inanunuliwa kwa pesa na pesa haina jinsia basi gari za kike hakuna..
Unaweza kukuta mtu ana Vits ya milioni 24 na mwingine ana Benz ya milioni 10
sasa 'uanaume' ni upi hapo?
 

Inaelekea wewe ni BABA mwenye Vits!
 

naona kabisa una vitz mkuu.
 
wiseboy uko sahihi lakini kwa rangi hapana, it looks weird kwa mwanaume kuendesha gari yenye rangi ya pink kama usafiri binafsi
 
Last edited by a moderator:
Ujuha wao tu...
Tutasikia na mitaa ya kike na ya kiume, nyumba za kike na za kiume, mashamba ya kike na ya kiume, halafu tutahamia kwenye noti/sarafu za kike na za kiume.
 
wabongo noma...siku moja kitaa washkaji wamekaona ka-vitz kamepaki nje ya nyumba flan wakajua kuna mtt wa kike yupo ndani..basi wakakablock kwa mbele..nia,lengo na dhumuni lao mtt akitoka nje awaombe wasogeze gari lao ili wapate nafasi ya kuzeveza kidogo..basi kilitoka kipande cha mtu hicho..miraba minne..washkaji wakachoka
 
na ka passo kangu wakisema ka kike kwani nabadilika na kuwa mwananke??acha waseme tu kwa ujinga wao huku hata baskeli hawana.....
 
Hii mada tushadiscuss sana hapa last year au ndo mmeamua kutu refresh back
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…