Acid reflux ni kivipi inasababisha harufu mbaya kinywani?

baba na baba

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
27
Reaction score
33
Habari wakuu naombeni msaada wenu.

Nasumbuliwa na tumbo kuwaka moto, nahisi kukabwa na kitu kooni, natoa vitu vidogo vidogo kama mabaki ya chakula yaliyo Ganda kwenye Koo, sauti kukata nikiongea kwa sauti ya juu na kutoa harufu mbaya kinywa.

Nahitaji kujua kama sababu ya kutoa harufu mbaya kinywani inasababishwa na acid pia?
 
Habari wakuu naombeni msaada wenu.
Nasumbuliwa na tumbo kuwaka moto,nahisi kukabwa na kitu kooni,natoa vitu vidogo vidogo kama mabaki ya chakula yaliyo
Hivyo vitu unavyotoa kooni siyo tonsil stones kweli?

Tonsil stones husababisha harufu mbaya pia.

Lakini, kabla ya hayo mengine, usafi wako wa kinywa ukoje?

Unakisafisha kinywa chako inavyopaswa?
 
Nazingatia usafi siku zote lakini hakuna nafuu nayo pata.
 
Tonsils sina nimetizamwa hospital
 
Nazingatia usafi siku zote lakini hakuna nafuu nayo pata.
Una floss nyuma na chini ya magego yako?

Maana hiyo sehemu ndo huwa moja ya chanzo cha harufu mbaya ya kinywa.

Mabaki ya chakula huwa yanabaki kwenye hiyo sehemu.

Yakibaki huko kwa muda mrefu halafu ukichanganya na joto la kinywa, hayo ni mazingira mazuri ya bakteria kuzaliana.

Bakteria hao ndo husababisha harufu mbaya ya kinywa.

Sijui uko wapi. Ila kama unaweza, nunua hii dental kit.

IMG_6502.jpeg

Ina hizo dental picks ambazo ni mahsusi kwa kuchokonolea mabaki ya chakula yaliyopo nyuma na chini ya magego.

IMG_6503.jpeg
 
Kwanza, pole sana kwa hali unayopitia. Acid Reflux ni ugonjwa unaoumiza sana.

Je, nini husababisha harufu mbaya ya kinywa?
1. Mdomo kuwa mkavu.
Acid reflux inapunguza sana uzalishwaji wa mate, na hivyo kusababisha hali iitwayo kisayansi xerostomia. Mate husaidia sana kusafirisha mabaki ya chakula na bakteri. Sasa ukosefu wake hupelekea mabaki ya vyakula na mate kubakia kinywani, na kuoza na kupelekea harufu mbaya kinywani.

2. Acid ya tumbo.
Tumboni kwetu tuna acid isaidiayo katika mmeng'enyo wa chakula. Acid hiyo ni HCL. Sasa acid reflux husababisha acid hiyo kurudi kwenye oesophagus na kubeba vyakula ambavyo havijameng'enywa kwa ukamilifu kuelekea kwenye koo na baadae mdomoni. Hii husababisha matonge tonge hayo kuleta harufu mbaya sana kinywani.

Ulichouliza hayo matonge tong ni chakula kilichomeng'enywa nusu. Mkuu Nyani Ngabu siyo tonsil stones.

3. Kurudi kwa Acid kunaweza kusababisha vidonda kwenye umio (oesophagus) na koo. Ile acid inachoma kuta za koo, ukichungulia unaona uwekundu. Ni vidonda. Sasa inasababisha infections ambayo huleta harufu mbaya sana kinywani.

4. Bakteria mdomoni.

Ili kupunguza hali hiyo, tafadhali zingatia sana usafi. Pia, pata matibabu. Acha unywaji wa pombe na vinywaji baridi, acha vyakula vyenye viungo vingi na kunywa maji mengi.

Ugua pole Mkuu.
 
Una uhakika siyo tonsil stones kweli? Kwani tonsil stones ni nini kwa ufahamu wako?
 
Habari wakuu naombeni msaada wenu.
Nasumbuliwa na tumbo kuwaka moto,nahisi kukabwa na kitu kooni,natoa vitu vidogo vidogo kama mabaki ya chakula yaliyo Ganda kwenye Koo,sauti kukata nikiongea Kwa sauti ya juu,na kutoa harufu mbaya kinywa.
Naitaji kujua kama sababu ya kutoa harufu mbaya kinywani inasababishwa na acid pia?
Pole mkuu,Kama una GERD unaweza pata io Hali ya harufu mbaya kwa sababu unapata reflux ya undigested contents, bile na pia hizo contents zikikaa kwenye Koo ya chakula Inaweza fanya harufu mbaya,pia io acid ikizidi Inaweza weka mikwaruzo kooni ambapo unaweza kupata infection itakayosababisha kutoka harufu mbaya,jitahidi kunywa maji mengi na kutumia mouth wash izo..🤭
 
Achana na hao madokta uchwara ambao wengi saiz wanaisingizia acid na acid haipo siriouz kiivyo mkuu,,,Niamini mimi una jipu hapo kooni nahayo unayotoa ni usaha kama sio jipu bas patakuwa na donda lenye uozo ambalo hupelekea uvimbe had koo kuziba
 
Kwanza, pole sana kwa hali unayopitia. Acid Reflux ni ugonjwa unaoumiza sana.

Je, nini husababisha harufu mbaya ya kinywa?
1. Mdomo kuwa mkavu.
Acid reflux inapunguza sana uzalishwaji wa mate, na hivyo kusababisha hali iitwayo kisayansi xerostomia. Mate husaidia sana kusafirisha mabaki ya chakula na bakteri. Sasa ukosefu wake hupelekea mabaki ya vyakula na mate kubakia kinywani, na kuoza na kupelekea harufu mbaya kinywani.

2. Acid ya tumbo.
Tumboni kwetu tuna acid isaidiayo katika mmeng'enyo wa chakula. Acid hiyo ni HCL. Sasa acid reflux husababisha acid hiyo kurudi kwenye oesophagus na kubeba vyakula ambavyo havijameng'enywa kwa ukamilifu kuelekea kwenye koo na baadae mdomoni. Hii husababisha matonge tonge hayo kuleta harufu mbaya sana kinywani.

Ulichouliza hayo matonge tong ni chakula kilichomeng'enywa nusu. Mkuu Nyani Ngabu siyo tonsil stones.

3. Kurudi kwa Acid kunaweza kusababisha vidonda kwenye umio (oesophagus) na koo. Ile acid inachoma kuta za koo, ukichungulia unaona uwekundu. Ni vidonda. Sasa inasababisha infections ambayo huleta harufu mbaya sana kinywani.

4. Bakteria mdomoni.

Ili kupunguza hali hiyo, tafadhali zingatia sana usafi. Pia, pata matibabu. Acha unywaji wa pombe na vinywaji baridi, acha vyakula vyenye viungo vingi na kunywa maji mengi.

Ugua pole Mkuu.
Asante sana mkuu umenisaidia kufahamfu kiunda sana mungu akubariki
 
Achana na hao madokta uchwara ambao wengi saiz wanaisingizia acid na acid haipo siriouz kiivyo mkuu,,,Niamini mimi una jipu hapo kooni nahayo unayotoa ni usaha kama sio jipu bas patakuwa na donda lenye uozo ambalo hupelekea uvimbe had koo kuziba
Asante nitafanyia kazi hilo
 
Pole mkuu,Kama una GERD unaweza pata io Hali ya harufu mbaya kwa sababu unapata reflux ya undigested contents, bile na pia hizo contents zikikaa kwenye Koo ya chakula Inaweza fanya harufu mbaya,pia io acid ikizidi Inaweza weka mikwaruzo kooni ambapo unaweza kupata infection itakayosababisha kutoka harufu mbaya,jitahidi kunywa maji mengi na kutumia mouth wash izo..🤭
Asante sana mkuu🙏
 
Una uhakika siyo tonsil stones kweli? Kwani tonsil stones ni nini kwa ufahamu wako?
Ameshasema anaumwa GERD.

Kwa hiyo tunachopaswa kujiulza kama ni namna gani GERD inasababisha harufu mbaya.

Vipo sababu kede zisababishazo mdomo kutoa harufu mbaya, ikiwemo madonda ya tumbo, nk.

Tonsil stones nazijua ndiyo. Nina uhakika pia kuwa si sababu inayomsababisha mhusika kuwa na mdomo unaonuka.
 
Ndio ni gred nilienda hospital nikaambiwa...ETN clinic
 
Achana na hao madokta uchwara ambao wengi saiz wanaisingizia acid na acid haipo siriouz kiivyo mkuu,,,Niamini mimi una jipu hapo kooni nahayo unayotoa ni usaha kama sio jipu bas patakuwa na donda lenye uozo ambalo hupelekea uvimbe had koo kuziba
Wewe ni doctor wa mitishamba eti?!!!maana hata uandishi unakushinda na nyie ndiyo huwa kila kitu mnajua au mmeshawahi kutibu.

Huwezi ukaonekana msaada kwa mtu kama utafanya ulichofanya hapo juu kuuponda ushauri wa mwenzako kwa sababu wewe ndiye utaeonekana kanjanja zaidi elewa hapa kila mtu anajaribu kusaidia ukizingatia hakuna mwenye kipimo cha maabara cha mleta mada,hiyo hali anayozungumzia mleta mada (kutoka mabaki ya chakula kinywani) mimi ilishawahi kunitokea na nahisi alichoeleza restart hapo juu yupo sahihi.
 
Sawa ningeomba unambie nionane na doctor wa meno au?
Ndiyo.

Anza kwanza kwa mganga wa meno. Atakufanyia tathmini ya kitaalamu na kukupatia tiba/ ufumbuzi wa tatizo lako/ pendekezo la nini ufanye au wapi uende kwa msaada zaidi.
 
Pole mkuu,Kama una GERD unaweza pata io Hali ya harufu mbaya kwa sababu unapata reflux ya undigested contents, bile na pia hizo contents zikikaa kwenye Koo ya chakula Inaweza fanya harufu mbaya,pia io acid ikizidi Inaweza weka mikwaruzo kooni ambapo unaweza kupata infection itakayosababisha kutoka harufu mbaya,jitahidi kunywa maji mengi na kutumia mouth wash izo..🤭
Naomba kujua ulitumia dawa Gani mkuu
 
Back
Top Bottom