Kwanza, pole sana kwa hali unayopitia. Acid Reflux ni ugonjwa unaoumiza sana.
Je, nini husababisha harufu mbaya ya kinywa?
1. Mdomo kuwa mkavu.
Acid reflux inapunguza sana uzalishwaji wa mate, na hivyo kusababisha hali iitwayo kisayansi xerostomia. Mate husaidia sana kusafirisha mabaki ya chakula na bakteri. Sasa ukosefu wake hupelekea mabaki ya vyakula na mate kubakia kinywani, na kuoza na kupelekea harufu mbaya kinywani.
2. Acid ya tumbo.
Tumboni kwetu tuna acid isaidiayo katika mmeng'enyo wa chakula. Acid hiyo ni HCL. Sasa acid reflux husababisha acid hiyo kurudi kwenye oesophagus na kubeba vyakula ambavyo havijameng'enywa kwa ukamilifu kuelekea kwenye koo na baadae mdomoni. Hii husababisha matonge tonge hayo kuleta harufu mbaya sana kinywani.
Ulichouliza hayo matonge tong ni chakula kilichomeng'enywa nusu. Mkuu
Nyani Ngabu siyo tonsil stones.
3. Kurudi kwa Acid kunaweza kusababisha vidonda kwenye umio (oesophagus) na koo. Ile acid inachoma kuta za koo, ukichungulia unaona uwekundu. Ni vidonda. Sasa inasababisha infections ambayo huleta harufu mbaya sana kinywani.
4. Bakteria mdomoni.
Ili kupunguza hali hiyo, tafadhali zingatia sana usafi. Pia, pata matibabu. Acha unywaji wa pombe na vinywaji baridi, acha vyakula vyenye viungo vingi na kunywa maji mengi.
Ugua pole Mkuu.