Acid reflux ni kivipi inasababisha harufu mbaya kinywani?

Inahitaji kwanza kujua ni tatizo gani unalo, labda ni reflux, labda ni peptic ulclers

Kwanza kapime kuhakiki kama ni peptic ulcers tibu kwanza hili moja. Reflux ni tatizo kubwa zaidi, pengine ni hizo ulcers tu ndio ulizonazo
 
Dr Restart,
Ushauri wako ni mzuri kweli sana. Mimi nilikuwa na tatizo hilo na nimepata matibabu na ninafuata masharti kama ulivyomshauri mleta hoja na ninaendelea vizuri.

Ila mbona nimekatazwa kula kila aina ya nyama iwe nyekundu au nyeupe! Nimepewa na masharti mengine mengi. Kunywa maji mengi na kuacha vyakula vyenye viungo vingi kunanisaidia sana. Nakupongeza sana mkuu.
 
Ndiyo.

Anza kwanza kwa mganga wa meno. Atakufanyia tathmini ya kitaalamu na kukupatia tiba/ ufumbuzi wa tatizo lako/ pendekezo la nini ufanye au wapi uende kwa msaada zaidi.
Daktari mhusika kabisa wa tonsil stones ni ENT specialist.

Dentist ni specific kinywani. Huko kooni ni kwa ENT. Ijapokuwa hata mtaalam wa meno anaweza kuziona ila anapaswa daktari ambaye ni mtaalam wa kuzijua, kuzichunguza na kung'amua matatizo mengine ni Specialist wa ENT.

Ambaye kwa taarifa ya mhusika alishamtembelea. Japo yeye anasema ETN.
 
Inahitaji kwanza kujua ni tatizo gani unalo, labda ni reflux, labda ni peptic ulclers

Kwanza kapime kuhakiki kama ni peptic ulcers tibu kwanza hili moja. Reflux ni tatizo kubwa zaidi, pengine ni hizo ulcers tu ndio ulizonazo
Peptic ulcers ni nn? Naomba kufahamishwa
 
Okay, sawa.
 
Mkuu, kwanza pole na hongera kwa kuanza kupata nafuu kwa tatizo ulilonalo.

Umezuiwa matumizi ya nyama kwa sababu kuu mbili;
a)Moja, mmeng'enyo wa nyama ni wa taratibu sana. Sasa kama upo taratibu maana yake acid itaendelea kuachiwa kwa muda mrefu na hivyo kuendelea kuongeza tatizo.

b)Mwilini kuna valve au tuseme koki, inayofunguka na kuachia. Koki mfano ya mkunduni, nyingine inaitwa lower oesophagical sphincter. Sasa ukila nyama kunasabisha koki hii (LES) kulegea. Na ikilegea inaachia acid kuflow kwenye oesophagus. Na hivyo kusabanisha tatizo kuwa kubwa zaidi.

Hata hivyo unaweza kutumia kwa kiwango kidogo sana.

Endelea kufuata maelekezo Mkuu.
 
Nimekuelewa sana Dr. Restart. Na ndivyo nilivyoambiwa na mtaalamu mwenzako. Kwa kweli naendelea vizuri sana. Mbarikiwe sana nyote. Kwa wengine nawaomba mfuate ushauri wa Dr. Restart. Mimi ni shahidi na ninaendele vizuri kabisa. Nyama nimeacha kwa kiasi kikubwa. Once in a while nakula kidogo nyama. Nakula mboga za majani kwa wingi.
 
Unazingatia vitu vidogo sana huenda una akili ndogo pia mimi sijashindwa kuandika ilo neno kama na wewe ni dr uchwara saman kwa hilo,,,kama ulishawahi patwa na hii kitu msaidie ndugu yetu mana huu ugonjwa unatesa wengi sana wanaambiwa ni acid alafu suruhu hamna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…