GE2025 ACT mmeshindwa hata kuvunga kuwa nyie sio CCM B? Eti Mpina kama mgombea Urais! Watu sio wajinga bana!

GE2025 ACT mmeshindwa hata kuvunga kuwa nyie sio CCM B? Eti Mpina kama mgombea Urais! Watu sio wajinga bana!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mimi sio nabii but uchaguzi wa mwakani watu watakua wachache pamoja na kutumia wasanii majukwaani kuvuta watu siku ya kupiga kura watu watakua wachache sana
 
Kusema kweli wamekurupuka, njaa haijawahi kuwa rafiki
 
unaongea kama uliechanganyikiwa. Kuwa mpina alikuwa mtu wa mana akiwa CCM ama? wengi wa vijana wa chadema ni mataahira
 
Kulingana Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa;

"Vyama vinavyopata ruzuku ni vile vilivyopata angalau asilimia tano ya kura zote halali zilizopigwa katika Uchaguzi Mkuu na vyama vyenye Wabunge au Madiwani. Kigezo kinachotumika ili chama kiweze kupata ruzuku ni kuangalia matokeo ya uchaguzi kuona kama chama kimepata asilimia tano ya kura au kama chama kimeshinda nafasi za ubunge au udiwani, kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 16 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, namba 5 ya mwaka 1992."

Mpina ulikuwa mtu wa maana sana na Kisesa walikuwa wanakuheshimu kwelikweli, mwisho umekuja kutuonesha wewe naye huna maana, ni wapuuzi kama wapuuzi wengine unaochangia kuwakandamiza Watanzania. Umetuonesha yale yote ulikuwa unafanya yalikuwa maigizo tu, huna tofauti yote na vijani wengine waliooza.

CHADEMA imetetemesha CCM, imewafanya waumwe kichwa, wananchi wameamka na hawataki ujinga, comments mtandaoni na mijadala mitaani inathibitisha hilo, ili watoboe ilibidi watafute kuungwa mkono ili kuonesha upinzani umeshiriki ilhali wanamuengua mpinzani wao mkubwa CHADEMA.

Lengo la kumpeleka Mpina kuhamia ACT Wazalendo inamaana ataongeza amsha amsha kule ACT Wazalendo, ukijumlisha na CHAUMMA tayari watakuwa na nguvu ya kusema wapinzani walishiriki uchaguzi, na hapa kuna mawili;

1. Utokee wizi wa maana yaani ile ya 2020 kuwa cha mtoto, halafu asilimia za kura zigawanywe hivi

Mpina na CCM B, ACT wakipewa 3.4%
Mbowe aaah ni Ubwabwa - CHAUMMA wakapewa 4.5% au .7
Halafu wengine wakagawana wagawane 2% au 3%
Kubwa la maadui mama anatosha ametufikisha hapa wakalama 90% au zaidi

Kwenye hii ni kuwa watapiga umafia wa kutisha kiasi cha kuwanyima na ruzuku kabisa:LaughHard: (nacheka ka mazuri) na hakutakuwa na rorote la kuwafanya sababu uhalali tayari wanao, wapinzani wameshiriki lakini watanzania wameelewa show ya mama mpaka wamebubujikwa na machozi ya Lucas Mwashambwa, tukapeta na 100% chama kimoja

2. Watoe 5% kwa chama kimoja wapo either CCM B au C, afu wapili apate 3% wale 14 watagawana 2%, teminator apate 90% au zaidi wakiminya sana, mchezo umeisha.
Hapa wataonesha kuna chama kingine cha upinzani kimeibuka baada ya CHADEMA kufa, na kwakuwa ndio kwanza kimeanza kupata wafuasi ndio wamejitahidi kufikia hiyo asilimia 5%, demokrasia imezidi kuimarika nchini Tanzania:KEKWlaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Ni kwanini 90% katika option zote mbili? Hapo lazima wazipiku kura za Magu, kuonesha kuwa Mama (kama ataendelea kuwa mgombea baada ya mpasuko kuendelea kutokea) amekubalika kuzidi Magu, yaani watanzania wamempenda mpaka wamempenda zaidi:PepeLaugh::luffyLaugh:.

Mpina ungekuwa na nia njema na Watanzania na kweli ulikuwa unataka kuleta mageuzi kwenye siasa, ungeenda kugombea ubunge, maana wewe na sisi tunajua huna ubavu wa kugombea Urais, yaani huna hiyo Pawa ya sasa kutoshea kwenye kile kiti, sasa hata baada ya kujua yote hayo kwanini ushift na kwenda moja kwa moja kutaka Urasi na ACT Wazalendo wakukubali chaap bila upinzani, halafu Watanzania tuamini kwamba hiyo siyo sinema?

Na mlivyokuwa wajinga mkampokea na shushushu mwingine siku hiyo hiyo kwenye chama, aloooo sisi siyo wajingwa bwana:BearLaugh::BearLaugh::BearLaugh: Endeleeni na sinema ila Watanzania wa leo sio wa jana!
We ni poyoyo tu na viporojo vyako
 
Kama ile biashara aliyoifanya Mbowe na Lowassa. Pale ndio niliwaona wapinzani wa nchi hii ni hovyoooooo.
 
Samahan mkuu je lowasa alipokuja chadema .
Chadema nayo ilikua ccm B
CHADEMA YA MBOWE..NDIO!..CHADEMA YA LISSU ..BIG NO!
Ila Kuna wakati ni Bora ujikalie kimya usubiri kuona another Cinema
 
We ndio msemaji wa watanzania wote.peleka ujinga uko kura tutapiga tena Kwa wingi .alaf mataira kama ww mtabaki kulalamika mtaan kua ccm aijashinda kihalali wakat mmehamasishana wenyewe kutopiga kura
Utapiga na nani?

Sema nitapiga .
 
Utapiga na nani?

Sema nitapiga .
Na wajumbe wa ccm na wananchi wa Tanzania ambao wameona maendeleo ya Tanzania
Nyie ambao mko kenya ndio hamtapiga na hio ndio kitu tunataka
 
Hivi kwa upumbav wenu mnazani kila mtu ana akili za kijinga na mihemko kma nyie
 
CHADEMA YA MBOWE..NDIO!..CHADEMA YA LISSU ..BIG NO!
Ila Kuna wakati ni Bora ujikalie kimya usubiri kuona another Cinema
Uyu lisu alie enda peleka umbea mpk ndege yetu ikashikwa ?
Huyu alietetea ushoga
Huyu alietetea kampuni ya barrick
Huyu kila cku kwenda kutuchongea nchi za nje
Watz hatujui tunatak nn
 
Na wajumbe wa ccm na wananchi wa Tanzania ambao wameona maendeleo ya Tanzania
Nyie ambao mko kenya ndio hamtapiga na hio ndio kitu tunataka
Gwajima ... Pole pole . Malisa ,ndugai ndo huyoooo????


Wajumbe gani wengine unawazungumzia?
 
Back
Top Bottom