GE2025 ACT: Tumepata taarifa kuna njama za Wagombea wetu Zanzibar kuwekewa pingamizi bila sababu za msingi kama ilivyofanyika 2020

GE2025 ACT: Tumepata taarifa kuna njama za Wagombea wetu Zanzibar kuwekewa pingamizi bila sababu za msingi kama ilivyofanyika 2020

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kanuni iliyomuengua mpina itatumika kuwaengua wagombea ubunge na udiwani ACT-Wazalendo waliujiunga nje ya muda wa kutangaza nia endapo watawekewa pingamizi.
 
PRESS RELEASE
Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilitoa Ratiba ya Wagombea wa Ubunge kuchukua na kurejesha Fomu za Kugombea (Fomu za Uteuzi).

Leo tarehe 27/08/2025 ni siku ya mwisho ya kurejesha Fomu na ndio siku ya Uteuzi na sasa ni saa kumi kamili na Wagombea wote wa Ubunge wa ACT Wazalendo kwa Majimbo yote 50 ya Zanzibar wameshakamilisha ujazaji wa Fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi zote za Wilaya za INEC zikiwa zimejazwa sawa sawa.

Tumepata taarifa kuwa kuna njama za kuwekewa pingamizi Wagombea wetu bila sababu za msingi kama ilivyofanyika mwaka 2020. Kuhusiana na hili, Chama chetu kimejitayarisha kupambana na hali hiyo kwa namna yoyote ile.

Natanguliza salam za Chama

ACT Wazalendo – Taifa kwanza leo na kesho
Omar Ali Shehe
Naibu katibu Mkuu – Zanzibar
Kalindeni kura😅😅😅
 
Back
Top Bottom