ACT: Tunaitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza matukio yote ya Mauwaji, Vipigo na Utekaji, Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-04-02 at 12.05.42_8bf56e63.jpg

WhatsApp Image 2025-04-02 at 12.05.42_69a8c8ff.jpg

TAARIFA KWA UMMA​

(Tunaitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza matukio yote ya Mauwaji, Vipigo na Utekaji, Zanzibar)

ACT-Wazalendo, tumepokea kwa mshituko taarifa ya kutekwa, ndugu Fakih Ali Salim, mwenye umri wa miaka 40 na mkazi wa Kijiji cha Chozi, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Siku ya tarehe 27 Machi 2025 na watu wasiojulikana, na hadi sasa hajapatikana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake, zinaeleza kuwa alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimtaka amtafutie kuku wa kununua. Baada ya kufanikisha ombi hilo, alikutana na gari aina ya Haria katika Kijiji cha Minyenyeni, Majira ya Saa 5:00 asubuhi, akaingia ndani ya gari, na tangu wakati huo hajulikani alipo.

ACT-Wazalendo tunalaani vikali kitendo hiki cha kutekwa kwa Fakih Ali Salim na tunaitaka Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kutimiza wajibu wao wa kulinda rai na mali zao, hivyo basi kuhakikisha, ndugu Fakih Ali Salim anapatikana akiwa mzima wa Afya.

ACT Wazalendo, Tumeshanganzwa na kushitushwa na ukimya wa Jeshi la Polisi, licha ya tukio hili kuripotiwa kwao, kupitia RB Wete 27/3/2025.241, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa mpaka sasa. Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama kuhakikisha kwamba wanalinda raia na mali zao, hasa katika kipindi hiki cha matayarisho ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, na kuongeza juhudi katika uchunguzi wa tukio hili na kutoa taarifa kwa umma kuhusu hatua zinazochukuliwa ili Wananchi Zanzibar waondokane na ghofu iliyoanza kujenga wa matukio haya ya utekaji na mauwaji.

Ni hivi karibuni tu matukio kadhaa yameripotiwa kutokea, kama tukio la Kidoti, tukio la Kiungoni na tukio la Mkoani, lakini hakuna hatua au taarifa yoyote kutoka katika, Jeshi la Polisi kutokana na matukio hayo, ambao yanaondosha imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi.

ACT-Wazalendo tunasimama na familia ya Fakih Ali Salim, katika kipindi hiki kigumu, tutaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya uchunguzi huu na hatutakaa kimya hadi haki ipatikane.

ACT Wazalendo, Tunatoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kufanya mambo yafuatayo:-

1. Tunaitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza matukio yote ya Mauwaji, Vipigo na Utekaji yaliyoanza kutokea na kuiweka hadharani taarifa hiyo na kuwafikisha wahusika wote katika vyombo vya sharia

2. Tunaitaka Serikali kuhakikisha kwamba wanavielekeza Vyombo vya ulinzi na Usalama kutotumia vibaya madaraka na mamlaka yao.

3. Tunaitaka Tume ya Haki za Binaadamu, kufanya Uchunguzi na kuweka hadharani taarifa yao.

4. Tunawaelekeza Wananchi wote wa Zanzibar, kuchukua tahadhari ya kujilinda na matukio ovu yalioanza kushamiri kama vile, mauwaji, vipigo na utekaji.

Imetolewa leo, tarehe 02/04/2025 na,
Hamad Mussa Yussuf,
Msemaji wa Ofisi, Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar
 
ACT, CCM hawawezi fanya hayo ambayo wao ndiyo chanzo! Suppose ameyaamulu mkuu wao, atakubali kujichunguza? tafuta njia nyingine , siyo hiyo
 
Back
Top Bottom