TAARIFA KWA UMMA
TUNAITAKA SERIKALI YA JMT, KUWACHA MARA MOJA UTOWAJI WA LESENI KWA ENEO LA FUNGU MBARAKA NA BAHARI KUU UPANDE WA ZANZIBAR
Tokea mwaka (2009) ambapo Baraza la Wawakilishi na Serekali ya awamu ya sita ya Dr. Abedi Amani Karume na aliekua Waziri wa sekta hiyo ndugu Mansour Yussuf Himid, kuweka msingi wa wazi na kishujaa wa kulinganganua suala la mafuta na gesi asilia kutoka makucha ya Tanganyika.
Gesi ya Mtwara inanufaisha Zanzibar kaa ilivyo madini , Utalii n.k. ikiwemo Ardhi .
Waya wa Umeme kutoka Tanganyika unakarabatiwa kwa bilioni 240 na JMT au Tanganyika. Zbar hawajakataa!!
UDSM inajenga campus, TIA wamekamilisha, Mweka wanajenga chuo Zanzibar, Uhamiaji wanajenga chuo Zanzibar na majengo. Zote hizo ni kodi za Tanganyika, Wazanzibar hawakatai hayo!
Wazanzibar wanajikatia mapande ya Ardhi Tanganyika! Kuna siku Watanganyika watawaulizakuhusu mipaka !
Jambo ambalo Serekali ya Zanzibar haipaswi kuona aibu kuficha wala kulifumbia macho juu ya khatma ya utafutaji wa mafuta na gesi katika eneo la Fungu Mbaraka na Bahari Kuu upande wa Zanzibar. Fungu Mbaraka au Fungu Kizimkazi au Kisiwa cha Latham, Kisiwa ambacho masafa kutoka rasi ya Kizimkazi hadi katika Kisiwa hicho ni mail 36 (Kilomita 57.9). Kisiwa hicho kina urefu wa mita 320 na upana wa mita 164.5 kwa vipimo vya mwaka 1898. Kisiwa hicho kilitangazwa rasmi kuwa mali ya Zanzibar saa 12 asubuhi ya tarehe 10 october 1898.
Kilitangazwa na nani? Mpaka wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa wapi baada ya Uhuru ? Latham ilikuwa wapi!
Sultan kutamka haina maana iwe hivyo! Tanganyika haikuwahi kutawaliwa na Sultan!
ACT Wazalendo tunazo taarifa zenye kuaminika kwamba Serekali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, ipo katika maandalizi ya kutangaza utowaji mpya wa leseni kwa vitalu vipya kwa awamu ya tano (5th licencing round) katika eneo la ziwa Tanganyika na bahari ya hindi ikiwemo eneo la Fungu Mbaraka na eneo la bahari kuu upande wa Zanzibar, uzinduzi ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 05/3/2025 huku mgeni rasmi akitegemewa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, kufanya hivo ni kuingilia mipaka ya Zanzibar jambo ambalo halikubaliki kisheria.
Kumbe Zanzibar ina mipaka! Haya maneno msije kuyasahau maana Tanganyika ina mipaka pia.
Mipaka ya Zanzibar inalindwa na nani? Kama ni JWTZ , ni hawa ambao bajeti yao ni ile ya Tanganyika?
Kuna Watumishi 805 wa Uhamiaji wanaolipwa na Bajeti ya Tanganyika. Hawa wanalinda mipaka ipi huko Zanzibar
Ukimya huu kwa Serekali zote mbilli ile ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na hii ya Zanzibar pamoja na Taasisi zao zote zinazohusika na masuala ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta unatia mashaka na kuibua maswali mengi kwa wananchi.
JMT ina Zanzibar ndani yake. Hapa ni Serikali ya JMT na Zanzibar, ACT wanawalumu Watanganyika kwa lipi? Tanganyika imefichwa haina serikali.
5. Serekali ya Zanzibar itoke hadharani na kueleza umma kwa tamko rasmi la serekali kwamba eneo la Fungu Mmbaraka ni eneo la Zanzibar na haipaswi kwa mamlaka nyengine yoyote kufanya shuhuli yoyote bila ya ridhaa ya Serekali ya Zanzibar.
Mpaka haujadiliwi na upande mmoja. ACT tuungane Tanganyika irudi halafu tujadili mipaka na matumizi ya rasilimali. Mtakuwa na rasilimali zenu , Tanganyika haitabeba mzigo wa gharama . Ugomvi utakwisha!
Kwasasa mnajadili mpaka na nani? Humuwezi kujadili na Tanzania kwasababu mpaka wa Tanzania umefika Zanzibar
Msiishie mafuta na gesi, mtuambie hiyo mipaka yenu inalinwa na nani na kwa bajeti kutoka wapi?
Tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwacha mara moja mpango wake wa utowaji wa leseni kwa eneo la la Fungu Mbaraka eneo ambalo ni mali ya Zanzibar na kuindoa mara moja eneo lote la Zanzibar katika mpango wao wa baadae wa uchimbaji wa mafuta na gesi ili kuondoa migogoro inayoweza kutokea.
Haya maneno myakumbuke maana ipo siku Watanganyika wataitaka serikali ya Muungano kuzuia uporaji wa Ardhi kwa Watu kutoka Zanzibar!
Chama cha ACT Wazalendo, Tunamtaka Raisi Samia Suluhu Hassan asikukubali kutumika kuiziba mdomo Zanzibar kwa kushiriki katika ufunguaji huu wa leseni mpya za vitalu vya mafuta na gesi kwa Tanganyika bila yakutatua mkanganyiko uliopo sasa.
Mna hiari na Rais Samia!
Hata hivyo Chama chetu, hakitasita na kuendelea kua sauti ya Wazanzibari kwa kusimamia Serekali juu ya masuala yote yanayohusu rasilimali za Zanzibar kwa maslahi ya wanachi wa Zanzibar.
Rasilimali za Tanganyika ni za wote , za Zanzibar ni kwa masilahi ya Wazanzibar.
Watanganyika wanawasikia vizuri ipo siku watawajibu, hata kama si leo au kesho haya maandishi yatajibiwa !
Imetolewa leo, tarehe 03/01/2025 na,
Ndg. Said Ali Mbarouk
Msemaji wa Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar
0779955778
Tumewaambia Watanganyika siku nyingi , hiki Chama cha ACT ni cha Zanzibar!
JokaKuu Pascal Mayalla