The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo waliokuwa wamezuiwa kuingia nchini Angola wamerejea Tanzania usiku wa Machi 14, 2025, saa 9:40.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa ACT Wazalendo leo Machi 14, 2025, Mwanaisha Mndeme, viongozi waliorejea ni Kiongozi wa Chama, Dorothy Jonas Semu, Naibu Katibu wa Mambo ya Nje, Nasra Nassor Omar, na Katibu wa Haki za Binadamu, Pavu Abdallah.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, bado yupo jijini Luanda, Angola, akisubiri kukamilisha taratibu za safari ya kurejea nchini.
ACT Wazalendo imeeleza kusikitishwa na kimya cha Serikali ya Tanzania, hususan Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuhusu tukio hilo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kutotoa kauli rasmi kunavunja misingi ya kidiplomasia na kuhatarisha mshikamano wa Afrika pamoja na uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Angola.
Chama hicho kimeitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu kilichotokea kwa viongozi wake na kueleza hatua zinazochukuliwa, hasa ikizingatiwa kuwa mmoja wa waliokumbwa na tukio hilo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
ACT Wazalendo pia kimetaka Serikali kumuita mara moja Balozi wa Angola nchini Tanzania ili kutoa maelezo kuhusu tukio hilo. Chama kimeeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda heshima ya viongozi wa taifa na mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.