CCM haina ofisi Angola,Na kwambia hivi hujui lolote na kama unajua ni unafiki wako. Huwo ni ushirikiano na ccm kuhujumiwa kutokuingia huko. Kwanini hawajazuiwa sehem nyingine wakati Angola haijpakana na Tanzania?
Mimi na wewe nani yuko addicted?CCM haina ofisi Angola,
na wala haifahamu kama kulikua na jambo hilo lisilo halali kwa mujibu wa mamlaka za angola?
kwahiyo wale waliotoka Africa kusini, msumbiji na ulaya walizuiwa na EFF ya malema sio gentleman?
au uko addicted na CCM kuliko kubeti right?π
jikite kwenye mada bila mihemko wala kubabaika gentleman,Mimi na wewe nani yuko addicted?
Wewe unapolala na mumeo unaiwaza chadema badala ya ccm mada zako nyingi unazungumzia chadema it means uko addicted nayo.
nasema tena ccm ndio waliofitini hayo.
Ukichoandika kingeleta maana kama ungesema sababu ya kuzuiwa.Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo waliokuwa wamezuiwa kuingia nchini Angola wamerejea Tanzania usiku wa Machi 14, 2025, saa 9:40.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa ACT Wazalendo leo Machi 14, 2025, Mwanaisha Mndeme, viongozi waliorejea ni Kiongozi wa Chama, Dorothy Jonas Semu, Naibu Katibu wa Mambo ya Nje, Nasra Nassor Omar, na Katibu wa Haki za Binadamu, Pavu Abdallah.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, bado yupo jijini Luanda, Angola, akisubiri kukamilisha taratibu za safari ya kurejea nchini.
ACT Wazalendo imeeleza kusikitishwa na kimya cha Serikali ya Tanzania, hususan Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuhusu tukio hilo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kutotoa kauli rasmi kunavunja misingi ya kidiplomasia na kuhatarisha mshikamano wa Afrika pamoja na uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Angola.
Chama hicho kimeitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu kilichotokea kwa viongozi wake na kueleza hatua zinazochukuliwa, hasa ikizingatiwa kuwa mmoja wa waliokumbwa na tukio hilo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
ACT Wazalendo pia kimetaka Serikali kumuita mara moja Balozi wa Angola nchini Tanzania ili kutoa maelezo kuhusu tukio hilo. Chama kimeeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda heshima ya viongozi wa taifa na mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Hi Tlaatlaah katika watu wajanja na wenye akili Dar na wewe unajihesabu? Utafanya nihame Dar. Kwanza niambie, Angola wamefuta Watanzania kwenda kule kwa visa?umezubaa sana kifikra gentleman, pole.
but pamoja na Marais na viongozi wengine wastaafu kutoka mataifa mengine Africa na duniani kote, mamlaka za kiusalama za Angola hazikua na taarifa za ujio wa viongozi hao wala hapakua na tarifa za kuwepo kwa mkutano huo uliotarajiwa kuangazia masuala ya kisiasa na kidemokrasia duniani,
na kwahiyo,
delegates walihitajika kuandaliwa usalama wa kutosha na mamlaka za angola kabla ya kutua Angola kama walivyotua utadhani vibaka π
kwahiyo gentleman,Hi Tlaatlaah katika watu wajanja na wenye akili Dar na wewe unajihesabu? Utafanya nihame Dar. Kwanza niambie, Angola wamefuta Watanzania kwenda kule kwa visa?
kwamba serikali ya Tanazania ianze kupiga mayowe kwasabb viongozi wa ACT WAZALENDO kudhibitiwa Angola kwa kuingia nchini humo kinyume na sheria za nchi husika au?πView attachment 3270297
View attachment 3269977
UKIMYA WA SERIKALI YA TANZANIA JUU YA KUZUIWA KWA VIONGOZI WETU ANGOLA HAUKUBALIKI
HALI HALISI YA SASA
Tunapenda kuujulisha umma kuwa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Dorothy Jonas Semu akiambatana na Naibu Katibu wa Mambo ya Nje Ndugu Nasra Nassor Omar na Katibu wa Haki za Binadamu Pavu Juma Abdalla wamerejea nchini Tanzania takribani saa 9:40 usiku wa tarehe 14 Machi, 2025 baada ya kuzuiwa kuingia nchini Angola.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndugu Othman Masoud Othman bado yupo Jijini Luanda nchini Angola kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usafiri kurejea nyumbani Tanzania. Chama kitaendelea kutoa taarifa mara kwa mara kwa umma juu ya maendeleo ya suala hili.
UKIMYA WA TANZANIA HAUKUBALIKI
Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na ukimya wa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kulikalia kimya suala hili. Ni jambo linaloshangaza na kusikitisha kwa Serikali ya Tanzania kushindwa kutoa kauli yoyote dhidi ya kitendo hiki kinachokiuka taratibu za kidiplomasia, ari ya mshikamano wa Afrika na undugu wa kihistoria baina ya Tanzania na Angola.
Tunaitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itoke hadharani na kufafanua kilichotokea Angola na msimamo wa Serikali juu ya hilo ikizingatiwa kuwa miongoni mwa viongozi waandamizi waliokumbwa na kadhia hiyo yumo pia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Pia, tunarejea rai yetu ya kuitaka Serikali kumuita mara moja Balozi wa Angola nchini Tanzania kujieleza kuhusu kilichotokea kwa viongozi wetu nchini Angola.
Wakati wanaondoka waliiaga serikali?Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo waliokuwa wamezuiwa kuingia nchini Angola wamerejea Tanzania usiku wa Machi 14, 2025, saa 9:40.