ACT - Wazalendo badala ya kupambana kupanda, wanatamani CHADEMA ishuke ili wao waonekane juu

ACT - Wazalendo badala ya kupambana kupanda, wanatamani CHADEMA ishuke ili wao waonekane juu

Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote
Mkuu,agizo soda baridi nakuja kulipa.
 
Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote
Hakuna chama kichokuwa juu kikashuka kwa sababu ya migogoro ndani ya Chama chenyewe, kikakosa kudai ni mchongo wa CCM. Meema aliponyang'anywa NCCR Mageuzi pale Tanga alidai wanatumiwa na CCM. Hali kadharika CUF walidai vivyohivyo na sasa Chadema. Vyama vya upinzani visipoimarisha Demokrasia, mifumo ya utendaji, na sera za kusimamia ndani ya chama vitaendelea kupumbaza wapenzi na wanachama kuwa kila mgogoro ni mkono wa CCM. CCM inayozidi kuimarika kila mgogoro ktk upinzani inapojitokeza.
 
Kinachowaponza chadema ni kishindwa kujua wanapigania nini?

Awali wananchi waliwaelewa walipokuja na ajenda ya ufisadi akaingi JPM na hyo ajenda, kawabana wote mafisadi,badala ya kumuunga mkono,wakabaki wanawakingia mafisadi kifua, na kuanza kumponda JPM

Haya Sasa, wataingia Kwa wanananchi na ajenda gani wawaelewe km hapo mwanzo?

Infact hawana Tena mvuto,kwani nao wameshaonekana wana ajenda mbaya nyuma ya pazia.

Hata kipindi Cha Corona,wakawa wanalazimisha Watu wafungiwe ndani!!

Hapo ndipo uzalendo wao ulizidi kuonekana ni zero.

Maelezo ni mengi, heri CCM waendelee tu,Hadi chama kingine chenye Nia njema na nchi hii kitakapo anzishwa
[emoji419]Umesahau pia pale walipokuwa wakiwasaidia MABEBERU walipokamata ndege ya ATCL Kule Afrika Kusini.
 
Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote.

Lengo la CCM siyo kuipandisha ACT bali kuitumia ACT chini ya Zitto kuihujumu Chadema, chama kinachoonekana kuwa na msimamo kama iliyokuwa CUF ya Maalimu Seif ILI kukifanya kuwa kama CUF ya Lipumba. Baada ya CCM kufanikiwa lengo lake ACT itatupwa na kubaki kama ilivyo CUF na Zitto atadharaulika kama walivyo Lipumba na Mrema.

Zitto asijenge ACT kwa kutegemea mgongo wa Chadema na CUF akijenge chama chake kwa misingi waliyojiwekea kama chama. Chadema ina misingi yake akifata misingi ya Chadema kujenga chama chake atapotea.

“Huwezi kuwa tajiri kwa kuombea tajiri afirisike”.
Chama Puppet,,
 
Kwa style ya Zitto hawawezi kabisa kuipiku CHADEMA. Kwanza unajua ACT ipo hapa dar, Zanzibar, kigoma, labda kidogo na Mwanza .

Hata hivyo tunaongelea kwamba ACT hata huko ambako ipo bado ni kidogo sana na bado wachanga mno.

Sasa style ya kuongoza ya bwana Zitto ni ya ujanja ujanja na ubishi flani pamoja ana akili ya kuwapanga watu wakae Frontline ili yeye aweze kukaa ofisini kupanga namna ya kupiga mchuzi na mtu asimstukie.

Tusubiri 2025 haya maneno yangu mtayarusia, Ila wengi aliowaweka kwenye uongozi hawakubaliki na watu au wanachama ambao aliwavuna kutoka CUF walioamua kujiunga ACT kumfuata Marehemu Maalim.

Mtifuano umeanza na bado watatifuana maana kile cheo walichowekewa Cha umoja wa kotaifa Cha makamu wa pili wa Rais kimewekwa mahususi ili wavurugane wasiwaze kuchukua nchi Bali kula na kukaa kimya.

That being the case watamalizana kwelikweli na Zitto mpenda madaraka kule hawezi kugusa anatamani angekuwa mzanzibari aonje umakamu wa Rais Ila ndio hivyo.

His days a counted
ACT iko mitandaoni zaidi.
 
Back
Top Bottom