Tunaposema ZITTO na CHAMA chake Sio WAPINZANI ni pamoja na Kuamua Kudai TUME ya UCHAGUZI badala ya KATIBA MPYA.
KATIBA ndio kila Kitu hiyo TUME ya Uchaguzi Waitakayo kina ZITTO lazima IONGOZWE na Sheria Zilizomo kwenye KATIBA , TUME iliyopo Iliundwa baada ya KATIBA, Inashangaza sana MWANASIASA Anayejitangaza Eti ni MPINZANI Wakati Anadhohofisha Mipango ya WAPINZANI.
CCM haitaki KATIBA MPYA na ZITTO na ACT nao Hawataki KATIBA MPYA.
Kwanini HAWATAKI?
Ni wakati wa KUONGEZA MAPAMBANO ya KUDAI KATIBA MPYA hata kama ITACHUKUA MIAKA 5 TUDAI TU.
ACT WAZALENDO sio CHAMA cha UPINZANI ni TAWI la CCM.
View attachment 2082736View attachment 2082737
Sent from my SM-J600F using
JamiiForums mobile app
Zitto amekuacheni kwa mbali sana, Chadema ndio mana inakufa fofofo., Strategies za Chadema ni zile zile za tokea mwaka 1992, Zitto anaenda na wakati ametafakari sana na yeye angekuwa kama chadema ACT ingekwishakufa kitambo na yeye tukamtoa kwenye ramani za kisiasa lakini Zitto amejinoa zaidi kisiasa alipounganisha chama na kule Zanzibar amekuwa mwanasiasa wa sasa.
Si kila wakati unatakiwa uonyeshe kumchukia Adui bali unatafuta namna kumzunguka Adui yako kwa kupiga hatua faster kisiasa ndivyo ilivyokuwa kwa gwiji la siasa Tanzania Maalim Seif Sharif Hamad alitumia njia nyingi sana na karibu 90% alifanikiwa.
Chadema hujaribu direct lakini kwa siasa za Tanzania ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu., Hizi njia zimekuwa zikifeli kila uchao
Huwezi kuwa kiongozi wa upinzani halafu unategemea kuhamasisha siasa na kujenga chama kwa nchi kama Tanzania kupitia youtube na twitter,
Chadema nikiipenda sana ila kwa sasa wamekosa muelekeo kisiasa chama kimekufa kabisa, Tundu Lissu alitangaza kutoitambua serikali ya Tanzania lakini Samia alivyoingia madarakani kwanini alimpigia simu na kutaka kuzungumza naye ni kama vile kuna vitu anavisimamia lakini baadae anashindwa.
Juzi alitanga kurudi kwenye March na April Swali Je? huo ulinzi aliotaka ahakikishiwe na Serikali ya tanzania ndio arudi keshaupata?
Mwenyekiti wao yuko ndani sasa ni takriban siku 180, yeye ni mwanasheria wa chama hakujitafakari sasa kujitosa kumsaidia Mwenyekiti iwavyo na iwe kwa vile wanadai kesi ya kubambikiza anakuwa anaandika tu kwenye twitter
Kuna siku Tundu alipigiwa simu toka Ikulu Mama kutaka aongee naye akijadi yupo kwenye meeting sijui upuuzi mtupu, Meeting za nje ya nchi kwa siasa za Tanzania hazina impact yoyote naweza kusema unafkiri Mkuu wa nchi atakuwa na muda nampigia sijui tundu lissue nitamchek tena baadae mambo ya uraiani
Chadmea imekosa muelekeo hao wanachama milioni 8 wanaodai wako wapi? Mwenyekiti yupo ndani
Wanadai Katiba Mpya well., Katiba mpya unadai kwenye twitter? toa hao wanachama milioni nane au japo nusu yake tuone movement yenu basi ndio njia zinazotumika huko duniani kwa wale wenye kwenda direct., Chadmea imekosa mipango na sasa naweza kusema limebaki jina tu., ACT itawaacha mbali sana