ACT Wazalendo kinatumika kuwaondoa wananchi kwenye hitaji la katiba mpya

ACT Wazalendo kinatumika kuwaondoa wananchi kwenye hitaji la katiba mpya

Hoja za Zitto kila mara huwa na ukakasi, CCM wameamua kuwapaka wadanganyika mafuta kwa mgongo wa chupa ati ya kuwapa Tume huru. Yaani ni sawa na kuwa na njaa ya siku mbili afu mtu ana box la biskuti anakutupia kipande cha biskuti kimoja kukupima imani yako.

CCM ili kufanikisha hilo wanamtumia ndugu Zitto kujaribu kuwashawishi wapinzani na sisi wadanganyika kuwa Tume huru ndiyo ati italeta Katiba Mpya...kweli ndugu zangu? Bado tunazidi kudanganyika tu karne hii ya 21.

Ndugu Zitto hajawahi kuaminika, huyu ni mzee wa kula lotekote na kupuliza...huwa haachii fursa ikitokea ipite.

Huyu ndiye Kiongozi Mkuu wa ACT - cheo ambacho kitadumu hadi chama kitakapokufa ama yeye akifa.
 
Tatizo nikupinga mambo ya msingi bila kuelewa uzito wake.

Wewe uliwahi kuridhika na chakula ulichokula jana? Au ungependa kuboresha kadri siku zikienda?

Umewahi kuridhika na mafanikio yako na kubweteka bila kuhitaji kuboresha kadri siku zinavoenda. Au kujenga nyumba bora ya wakati au kununua kari bora ya wakati.

Binadamu mwenye akili timamu siko zote anapambana kuboresha maudhui yaliyopo yawe bora zaidi na hawezi kuridhika. Tunaboresha kuenda na wakati.

Tunaboresha mavazi
Tunaboresha magari na mitambo ....
Tunaboresha mifumo ya technology

Sasa kuboresha katiba kunatatizo gani?

Kuachana na katiba ya hovyo ili tutengeneza vasheni mpya bora inayokidhi mahitaji ya wakati kuna tatizo gani?
Na silazima watu wote wawe na mtazamo na mawazo sawa, munaeona hafanani na nyny ktk harakati za kuitafuta hiyo katiba mpya musione msaliti na mhaini asiefaa hata kuishi
 
Tunaposema ZITTO na CHAMA chake Sio WAPINZANI ni pamoja na Kuamua Kudai TUME ya UCHAGUZI badala ya KATIBA MPYA.
KATIBA ndio kila Kitu hiyo TUME ya Uchaguzi Waitakayo kina ZITTO lazima IONGOZWE na Sheria Zilizomo kwenye KATIBA , TUME iliyopo Iliundwa baada ya KATIBA, Inashangaza sana MWANASIASA Anayejitangaza Eti ni MPINZANI Wakati Anadhohofisha Mipango ya WAPINZANI.

CCM haitaki KATIBA MPYA na ZITTO na ACT nao Hawataki KATIBA MPYA.

Kwanini HAWATAKI?

Ni wakati wa KUONGEZA MAPAMBANO ya KUDAI KATIBA MPYA hata kama ITACHUKUA MIAKA 5 TUDAI TU.

ACT WAZALENDO sio CHAMA cha UPINZANI ni TAWI la CCM.

View attachment 2082736View attachment 2082737

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Ndugu...
Kila mtu anataka hiyo Katina mpya.
Lakini hebu niambie tutaipataje??
Mara ya mwisho ukawa walikimbia baada ya CCM kuamua kutumia wingi wao kupitisha maslahi yao...
Tena kpindi kile CHADEMA walikuwa karibia 80 bungeni... leo Yuko mmoja tu na wale covid hata mkimuagiza atoke hakuna atakaejua.
Hivi hujui kuwa kila kipengele cha katiba kinapigiwa kura na ili kipite ni lazima Iwe kwa 66%??
Kumbuka jumla ya wapinzani hata 10% hawafikiki


Njoo na mkakati wako tunapataje 66% kupitisha kipengele mfano kama kile cha Serikali 3 kinyume na sera ya CCM ya serikali 2??
Hoja hapa tunapita wapi tupate MAJORITY kupitisha maslahi yetu?
 
Mawazo ya kijinga

Unataka kukuambia
1. sheria, kanuni na Taratibu hazina umuhimu? Yaani mahakama haina maana?

2. Unataka kutuambia serikali haina maana kuwepo?

3. Unataka kutuambia bunge halina maana kuwepo?

Maana kuwepo kwa judiciary, executive na parliament nikwa mujibu wa katiba.

Acha ujinga wewe.
Hivyo vyote ulivyovitaja havipo au? Havifanyi Kazi? Acha upoyoyo,wananchi wanahitaji ustawi wa maisha sio maujinga ujinga ya chadema.
 
Back
Top Bottom