ACT Wazalendo kinatumika kuwaondoa wananchi kwenye hitaji la katiba mpya

ACT Tanganyika wasipokuwa makini wataikosa ACT visiwani (cuf Maalim Self)

Kinachofanywa na Act Tanganyika nikusaidia ccm, kudhoofisha upinzani jambo ambalo sidhani Act viwani wanaliafiki.

Inawezekana wakawa wapo pamoja lakini muda nimwalimu Mzuri sana
 
Tatizo la Chadema wanataka Siasa na mitazamo yao ndio iwe mitazamo ya watu wote halafu wanajiiita Wapigania uhuru wa kutoa maoni

Tuna vyama vingi kwa kuwa kila chama kitakuwa na utofauti na vyama vingine otherwise kisingekuwepo

Chadema kama mnaona ianze Katiba Mpya kabla ya Tume huru hayo ni mawazo yenu na msifanye mawazo yenu ndio Msahafu wa vyama vyote vya Upinzani vifuate

Kila siku Chadema wako busy kutuonesha kuwa ACT ni CCM B ila ACT hawana time ya kutuonesha kama Chadema ni nani kwa kuwa wanajua hilo sio jukumu lao
 
Miezi kadhaa iliyopita CHADEMA waliongoza kutaka TUME HURU YA UCHAGUZI. Video hapo chini zinaonyesha bayana kila kitu, hata kwenye mkutano wa shirikisho la vyama vya siasa Mnyika alienda na maombi makuu mawili, moja ni uhuru wa kufanya siasa, mbili ni tume huru ya uchaguzi, mwishoni ndio ikawekwa agenda ya nyingineyo ya Kesi ya Mwenyekiti Mbowe.

Kuna video hapo Kibatala anasema kwanza tume huru ya uchaguzi, then katiba mpya. Kuna Video ya Lissu anasema Tume huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya, na kuna video nyingine za Viongozi chadema wakitaka tume huru ya uchaguzi.

Niishie kwa kuwashauri CHADEMA, wasipoteze muda kuhangaika na katiba mpya, hawana wajumbe wengi bungeni, hata waliokuwepo hawawaamini, wapambane ipatikane tume huru inayoeleweka, then wataingia wengi bungeni, ndio waje na katiba Mpya.

Ni mawazo tu.






 
Wananchi wa wapi walikwambia katiba ndio itawalea msosi?

Hakuna anayetaka Katiba ya kuingiza machadema madarakani
 

Suala la katiba haliwezi kuwa la Cdm pekee nikwa watanzania wote

1. Haki kwa kila mtanzania

2. Maendeleo kwa kila mtanzania

3. Afya kwa kila mtanzania

4. Elimu kwa kila mtanzania

Hayo mambo ma nne yatakuwa bora, kamilifu na thabiti tukiwa na Katiba bora imara na kamilifu.

Tumehuru pekee nikutojali maslahi mapana ya taifa.

Tumehuru pekee ni ulafi wa madaraka na ubinsfsi wa kisiasa

Tume huru bila katiba bora bila msingi wa haki, taasisi imara nk ni ujinga tu.

Hitaji la Katiba nikwa watanzania wote
Wakulima
Wafugaji
Wafanyakazi
Wavuvi
Wamachinga
Mama lishe
Nk

Act inataka tumehuru ya uchaguzi .....urafi wa madaraka na ubinafsi.
 
ACT wachumia tumbo, ni wanafiki sana, zitto akiongoza namba moja
 
Kulazimisha approach yako ya kudai Katiba kutumiwa na kila mtu ni ushamba na ulimbukeni wa kidemokrasia

Kama bado mko upinzani lakin mnashindwa kuheshimu mawazo ya wengine mkipewa madaraka si mtawatia kwny viroba wanaowapinga?
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa kuwa vinahusika na uchaguzi mkuu.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.

ACT wazalendo ni tawi la kijasusi la chama cha CCM la kufanikisha nia ovu za CCM.
 
Kama unajua Yote basi Tambua hiyo Katiba Mpya itayopatikana chini ya CCM na vyombo vya usalama vilivyo chini yake itakuwa bure tu

Kama iliweza hata kuchomeka watu wake kwny Nafasi za juu za uongozi wa Chama kikuu cha Upinzani ndio itashindwa kuchomeka maslahi yake kwny Katiba mpya?, pili kwa sasa mna hiyo nguvu ya kushinikiza Katiba mpya zaid ya kutupia hashtag kwny Mitandao ya kijamii?
 
Wananchi wa wapi walikwambia katiba ndio itawalea msosi?

Hakuna anayetaka Katiba ya kuingiza machadema madarakani
Mawazo ya kijinga

Unataka kukuambia
1. sheria, kanuni na Taratibu hazina umuhimu? Yaani mahakama haina maana?

2. Unataka kutuambia serikali haina maana kuwepo?

3. Unataka kutuambia bunge halina maana kuwepo?

Maana kuwepo kwa judiciary, executive na parliament nikwa mujibu wa katiba.

Acha ujinga wewe.
 

Nyie bwana mnakuwa na mawazo ya ajabu Sana,
Mnasahau kuwa mko Africa, Yan Kwa akili yako unadhan serikali za Africa wanaweza kuweka katiba mpya?
 
Zitto hajawahi kuwa mpinzani wa kweli hata siku moja!
Huyu mtu ni ndumi la kuwili haswaa na mtu wsa maslahi binafsi.
Mmewahi kuona akipata misukosuko ya wapinzani wengine wa kweli?
 
shida ni kwamba wanaamini katiba mpya itakua suluhu ya matatzo yote nchini, kua na katiba mpya ni jambo moja na kufuatwa na kuheshimiwa hiyo katiba ikishapatikana ni jambo jengn
 
Act wazalendo ni Mistress wa Chama cha Mafisadi duniani CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fool
 
shida ni kwamba wanaamini katiba mpya itakua suluhu ya matatzo yote nchini, kua na katiba mpya ni jambo moja na kufuatwa na kuheshimiwa hiyo katiba ikishapatikana ni jambo jengn

Tatizo nikupinga mambo ya msingi bila kuelewa uzito wake.

Wewe uliwahi kuridhika na chakula ulichokula jana? Au ungependa kuboresha kadri siku zikienda?

Umewahi kuridhika na mafanikio yako na kubweteka bila kuhitaji kuboresha kadri siku zinavoenda. Au kujenga nyumba bora ya wakati au kununua kari bora ya wakati.

Binadamu mwenye akili timamu siko zote anapambana kuboresha maudhui yaliyopo yawe bora zaidi na hawezi kuridhika. Tunaboresha kuenda na wakati.

Tunaboresha mavazi
Tunaboresha magari na mitambo ....
Tunaboresha mifumo ya technology

Sasa kuboresha katiba kunatatizo gani?

Kuachana na katiba ya hovyo ili tutengeneza vasheni mpya bora inayokidhi mahitaji ya wakati kuna tatizo gani?
 
Zitto amekuacheni kwa mbali sana, Chadema ndio mana inakufa fofofo., Strategies za Chadema ni zile zile za tokea mwaka 1992, Zitto anaenda na wakati ametafakari sana na yeye angekuwa kama chadema ACT ingekwishakufa kitambo na yeye tukamtoa kwenye ramani za kisiasa lakini Zitto amejinoa zaidi kisiasa alipounganisha chama na kule Zanzibar amekuwa mwanasiasa wa sasa.

Si kila wakati unatakiwa uonyeshe kumchukia Adui bali unatafuta namna kumzunguka Adui yako kwa kupiga hatua faster kisiasa ndivyo ilivyokuwa kwa gwiji la siasa Tanzania Maalim Seif Sharif Hamad alitumia njia nyingi sana na karibu 90% alifanikiwa.

Chadema hujaribu direct lakini kwa siasa za Tanzania ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu., Hizi njia zimekuwa zikifeli kila uchao

Huwezi kuwa kiongozi wa upinzani halafu unategemea kuhamasisha siasa na kujenga chama kwa nchi kama Tanzania kupitia youtube na twitter,

Chadema nikiipenda sana ila kwa sasa wamekosa muelekeo kisiasa chama kimekufa kabisa, Tundu Lissu alitangaza kutoitambua serikali ya Tanzania lakini Samia alivyoingia madarakani kwanini alimpigia simu na kutaka kuzungumza naye ni kama vile kuna vitu anavisimamia lakini baadae anashindwa.

Juzi alitanga kurudi kwenye March na April Swali Je? huo ulinzi aliotaka ahakikishiwe na Serikali ya tanzania ndio arudi keshaupata?

Mwenyekiti wao yuko ndani sasa ni takriban siku 180, yeye ni mwanasheria wa chama hakujitafakari sasa kujitosa kumsaidia Mwenyekiti iwavyo na iwe kwa vile wanadai kesi ya kubambikiza anakuwa anaandika tu kwenye twitter

Kuna siku Tundu alipigiwa simu toka Ikulu Mama kutaka aongee naye akijadi yupo kwenye meeting sijui upuuzi mtupu, Meeting za nje ya nchi kwa siasa za Tanzania hazina impact yoyote naweza kusema unafkiri Mkuu wa nchi atakuwa na muda nampigia sijui tundu lissue nitamchek tena baadae mambo ya uraiani

Chadmea imekosa muelekeo hao wanachama milioni 8 wanaodai wako wapi? Mwenyekiti yupo ndani

Wanadai Katiba Mpya well., Katiba mpya unadai kwenye twitter? toa hao wanachama milioni nane au japo nusu yake tuone movement yenu basi ndio njia zinazotumika huko duniani kwa wale wenye kwenda direct., Chadmea imekosa mipango na sasa naweza kusema limebaki jina tu., ACT itawaacha mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…