ACT Wazalendo kinatumika kuwaondoa wananchi kwenye hitaji la katiba mpya

Hoja za Zitto kila mara huwa na ukakasi, CCM wameamua kuwapaka wadanganyika mafuta kwa mgongo wa chupa ati ya kuwapa Tume huru. Yaani ni sawa na kuwa na njaa ya siku mbili afu mtu ana box la biskuti anakutupia kipande cha biskuti kimoja kukupima imani yako.

CCM ili kufanikisha hilo wanamtumia ndugu Zitto kujaribu kuwashawishi wapinzani na sisi wadanganyika kuwa Tume huru ndiyo ati italeta Katiba Mpya...kweli ndugu zangu? Bado tunazidi kudanganyika tu karne hii ya 21.

Ndugu Zitto hajawahi kuaminika, huyu ni mzee wa kula lotekote na kupuliza...huwa haachii fursa ikitokea ipite.

Huyu ndiye Kiongozi Mkuu wa ACT - cheo ambacho kitadumu hadi chama kitakapokufa ama yeye akifa.
 
Na silazima watu wote wawe na mtazamo na mawazo sawa, munaeona hafanani na nyny ktk harakati za kuitafuta hiyo katiba mpya musione msaliti na mhaini asiefaa hata kuishi
 
Ndugu...
Kila mtu anataka hiyo Katina mpya.
Lakini hebu niambie tutaipataje??
Mara ya mwisho ukawa walikimbia baada ya CCM kuamua kutumia wingi wao kupitisha maslahi yao...
Tena kpindi kile CHADEMA walikuwa karibia 80 bungeni... leo Yuko mmoja tu na wale covid hata mkimuagiza atoke hakuna atakaejua.
Hivi hujui kuwa kila kipengele cha katiba kinapigiwa kura na ili kipite ni lazima Iwe kwa 66%??
Kumbuka jumla ya wapinzani hata 10% hawafikiki


Njoo na mkakati wako tunapataje 66% kupitisha kipengele mfano kama kile cha Serikali 3 kinyume na sera ya CCM ya serikali 2??
Hoja hapa tunapita wapi tupate MAJORITY kupitisha maslahi yetu?
 
Hivyo vyote ulivyovitaja havipo au? Havifanyi Kazi? Acha upoyoyo,wananchi wanahitaji ustawi wa maisha sio maujinga ujinga ya chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…