Tetesi: ACT Wazalendo : Kufanya Mkutano wa Halmashauri Kuu kubadili agenda ya No Reform No election

baro

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,129
Reaction score
4,028
Wakuu

Kwa Taarifa zilizonifikia ni kuwa kikao cha Tundu Lissu pamoja na Ado Shaibu (KM ACT WAZALENDO) na Ismail Jussa, kilichofanyika jana ofisi za chadema AGENDA yao ilikuwa ni kuhusu NO REFORM NO Elections na hivyo wamekubaliana, hiyo imepelekea ACT kuitisha halmashauri kuu ili AGENDA hiyo ipate baraka

Hakika mwaka huu tutaona mengi
 
Kama ndivyo naunga mkono hoja kabisa, unaenda kwenye uchaguzi wa kimangumashi ili iweje, box la kura linatakiwa heshimika na hii itasaidia kupiga hatua kimaendeleo kama nchi , ccm wakishinda kialali kuna shida gani , na kama wapo madarakani na wanasema wamefanya mengi wanaogopa nini kufanya reforms ili box liamue.
 
Kama wamepata akili na wameamua kuunga mkono hili suala kwa maslahi mapana ya Taifa, Mungu awabariki sana.

Narudia tena kuliko kupoteza fedha za walipakodi wa nchi hii wanazozilipa kwa jasho kubwa kufanya maigizo yanayoitwa Uchaguzi ni heri tusifanye tu uchaguzi tujue moja maana nchi hii sio kura za mwananchi zinazoamua kiongozi.

Kama hili litatokea hongereni sana ACT. Tena kama nyie ndo wazoefu sana namna kura zenu zinavyogeuzwa na kupewa CCM kule Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…