ACT WAZALENDO Kuhusu Kusitishwa kwa Misaada ya Afya na Serikali ya Marekani

ACT WAZALENDO Kuhusu Kusitishwa kwa Misaada ya Afya na Serikali ya Marekani

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
ACT Wazalendo imeguswa na uamuzi wa Serikali ya Marekani kusitisha kwa muda kwa mikopo na ruzuku za kusaidia huduma za afya duniani, hatua inayoweza kuathiri mamilioni ya Watanzania waliowekwa kwenye utegemezi wa huduma za afya zinazofadhiliwa na mashirika ya nje.

Tanzania, kama moja ya wanufaika wakubwa wa misaada ya hiyo kutoka Marekani kupitia Shirika la Misaada ya Marekani (USAID), Mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na UKIMWI (PEPFAR), Mfuko wa Dunia (Global Fund), Mpango wa Kupambana na Malaria (PMI) imechangia kwa kiasi kikubwa katika mapambano dhidi ya magonjwa kama UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria, na huduma za chanjo kwa watoto.

Kwa mfano, hadi kufikia Machi 2024, Tanzania ilikadiriwa kuwa na watu milioni 1.7 wanaoishi na VVU, ambapo zaidi ya milioni 1.5 wanatumia dawa za kufubaza makali ya UKIMWI (ARVs) tunazotegemea kutoka nje. Mapema mwaka huu Global Fund ilitangaza ufadhili wa dola za Marekani milioni 602. Sawa na Shilingi trilioni 1.57 kwa matibabu endelevu ya waathirika wa VVU.
Aidha, ACT Wazalendo kupitia Baraza Kivuli la Mawaziri tumekuwa tukiionya Serikali kuhusu utegemezi huu wa kifedha kutoka nje kwenye kutoa huduma za afya, ambapo unaweka rehani maisha ya Watanzania. Takriban 41% ya bajeti ya afya ya Tanzania inategemea Mashirika ya misaada ya kimataifa, tena kwa huduma za magonjwa hatari zaidi.
Kwa miongo mitatu, Serikali ya CCM imekuwa ikiacha suala la afya kwenye mabega ya wananchi wenyewe au wafadhili kutoka nje. Bajeti ya afya ya Tanzania ni chini ya asilimia 5 ya Bajeti Kuu ya Serikali, kinyume na makubaliano ya Abuja yanayotaka kutengwa kwa asilimia 15 ya bajeti kuu kwa ajili ya sekta ya afya.

ACT Wazalendo inaitaka Serikali kuchukua jukumu kamili la kuhakikisha sekta ya afya haitegemei tena misaada ya nje na katika kunusuru maisha ya mamilioni ya wananchi ambao sasa wako katika hatari kubwa kwa kuchukua hatua zifuatazo;

i. Serikali iwasilishe bungeni bajeti ya nyongeza (Supplementary Budget) ya Shilingi bilioni 263 ili kuziba pengo la fedha zilizositishwa na wafadhili, kuhakikisha huduma za afya zinaendelea bila kutetereka katika miezi iliyobaki.

ii. Serikali ihakikishe kuanzia mwaka wa fedha 2025/26, bajeti ya Wizara ya Afya itokane kwa asilimia 100 na vyanzo vya ndani, kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuimarisha usimamizi wa mapato kwenye uvunaji wa rasilimali zetu kama vile nadini, misitu, wanyama na gesi.

iii. Serikali iharakishe utekelezaji wa mfumo wa kuwaunganisha watanzania na Hifadhi ya Jamii na kutoa bima ya afya kwa wote ili kuongeza uwezo wa serikali kugharamia na kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya bila ubaguzi wa kifedha.

iv. Serikali iandae Utaratibu wa kuzalisha dawa za kufubaza vimelea vya Ugonjwa wa Ukimwi (ARV) hapa hapa nchini. Uzalishaji ufanywe kwa usimamizi makini na wa Karibu.
ACT Wazalendo tunasisitiza kuwa wajibu wa Serikali ni kuhakikisha inatumia rasilimali vizuri ili kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wote kwa usawa, si kwa kutegemea wafadhili wa nje. Tunaitaka Serikali kuchukua hatua hizi mara moja ili kunusuru maisha ya wananchi wetu. Serikali haipaswi kufanya mambo ya anasa huku ikiwaacha wanachi wake wanaishi kwa kutegemea hisani.

Dkt. Elizabeth Benedict Sanga
Waziri Kivuli wa Afya
ACT Wazalendo
30 Januari, 2024
 
Kuna mkuu kwenye uzi mmoja hivi nimesahau ID yake aliniambia hizi dawa ni gharama sana nisichukulie poa.

Angalia hapo kwa Taifa lilipofikia trilioni
1.57 ni ya kututia aibu hivi? Kwa ukubwa wa Tanzania na so called Uchumi wa kati bajeti ya trilioni
1.57 ni ya kutushinda kweli?
 
Pesa zinazoibwa kutokana na ufisadi kwasasa zitumike kucover hiyo misaada iliyositishwa. Pesa za kununulia ma Youtong za kijani na pikipiki za kijani.
 
Huku deni la Taifa linakaribia 100%?
Nakisi ya bajeti ya serikali inafidiwa na misaada ya Wafadhiri tutapata wapi pesa ya kutosha kwa ajili ya huduma za Afya?
Anyway Wachumi waje watuambie!
 
Back
Top Bottom