Uhusiano wa utawala na chama tawala kwa upande mmoja na vyama vya upinzani kwa upande mwingne, haukuwa wa kuridhisha ukiringanisha na hali ilivyo hivi sasa chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Haikuwa ni hali ya kawaida kuona viongozi wa juu wa kisiasa wenye itikadi tofauti, kuketi pamoja wakinena jambo, lakini kwa sasa hali hii sio ya kushangaza tena, kuona kiongozi wa juu kutoka chama pinzani wakikaa pamoja na kiongozi wa juu kutoka chama tawala (CCM) hii ni hatua kubwa na alama bora katika ujenzi wa demokrasia yetu kama taifa.
Tarehe 28th Juni 2022, Jopo la uongozi wa chama cha upinzani inchini Tanzania ACT Wazalendo wakiongozwa na kiongozi wao Mhe. Zitto Kabwe walikutana na kufanya mazungumzo na
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huu umeonesha ishara njema katika mambo kadhaa. Moja, Rais Samia ametoa nafasi kwa vyama vya kisiasa kukaa na kujadili nae ana kwa ana juu ya mambo yao ya kisiasa na sio majibizano kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii
Pia, mkutano huu unaleta picha nzuri yenye matumaini juu ya hali ya kisiasa hasa ustawi wa demokrasia yetu baina ya chama na chama, serikali na vyama pinzani.
Lakini pia, ujenzi wa umoja wa kitaifa, hali hii inatoa funzo na kuelewesha umma wa watanzania kuwa siasa sio uadui bali ni kupingana kwa hoja na si chuki kama watu wengine wafikiriavyo.
Mhe Rais Samia amekuwa akikutana na na viongozi wa juu kutoka vyama tofauti vya siasa hapa inchini ili kuleta umoja wa kitaifa na ustawi wa demokrasia yetu, Ikumbukwe pia mwezi uliopita alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mama Samia, anayo nia ya dhati kwa taifa letu.