Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kuna mawili:Membe atakuwa kamuunga mkono Lissu au kashindwa kuelewana na wenzake katika swala la kumuunga mkono Lissu iwapo kweli hakuwa tayari kufanya hivyo kama alivyosikika hivi karibuni na sasa kaamua kuendelea na issue zake zingine.
Lakini,huenda kapata dharura hivyo tusimuhukumu moja kwa moja bali tujipe muda ingawa dharura hiyo haipaswi kufanywa siri kama kweli kapata dharura.
Bila kupinga maelezo yako mazuri, mimi kama mimi sitaki hata Membe amuunge mkono Lisu, maana hata asipomuunga mkono bado Lisu na support ya kweli ya wapinzani. Huyo Membe ni mwanaccm leo hadi kesho, na ataingia kaburini akiwa mwanaccm.Sana sana akimsupport Lisu atalazimisha kuingia kwenye vikao vya mikakati vya cdm, kisha akirudi ccm anakuwa na siri kama kina Lowassa na Sumaye.
Tusikubali kabisa Membe kumuunga mkono Lisu ni hatari kubwa. Huko ACT mpinzani wa kweli ni Maalim Seif na Wapemba wenzake. Lakini hawa wakina Zito ni kukaa nao kwa akili.