ACT Wazalendo kushindwa kutoa msimamo kuhusu bandari kimejiondolea sifa. CHADEMA inaitumia fursa hiyo kuwasulubu

Mkuu Missile of the Nation, kwanza nikupongeze kwa bandiko hili kwasababu watu wenye uwezo wa kufanya analysis kama hizi humu JF, wanahesabika, big up sana kwa hili and keep it up, mabandiko kama haya yanaiheshimisha jf. Pili naunga mkono baadhi ya hoja.

Hivi ndivyo vyama serious vinavyotakiwa kufanya, this is a sign of maturity!. Chama mature, kunapotokea jambo lolote kubwa la chama kutoa kauli ya chama, chama kitakutana to deliberate on the issue, ndipo kinatoa kauli ya chama, kama walivyofanya CCM.

ACT Wazalendo hawajafanya kikao chochote kujadili issue ya Bandari kwasababu ACT Wazalendo sio chama cha matukio!.

Huu ni ukomavu, chama serious hakikurupuki kutoa kauli za chama wala hakilazimiki kufuata mkumbo, kimewapa viongozi wake demokrasia ya uhuru wa maoni yao binafsi, this is very healthy kwenye freedom of expression.

Ni kweli mkataba huu wa DPW na Bandari zetu una. matatizo makubwa ya kisheria

Sio lazima maoni ya kila mtu yafanane, hivyo Zitto Kabwe hajaiona hiyo hatari

Yeye ameona huo mkataba ni karatasi ya kufungia vitumbua,

Sii kweli, labda kwa watu wasiomjua Zitto, lakini wanaomjua wanamjua Zitto ni very serious leader.

Hapa naomba niheshimu tuu mawazo yako japo sikubaliani nawe

Hii ni kitu mpya kwa siasa za Tanzania, inaitwa strategic politicking

duh...!

Sii kweli

Hili neno!.

Hili neno!

Naunga mkono hoja, ACT Wazalendo kilipoanzishwa kilianza vizuri, na mimi nililizungumzia Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza kiukweli Zitto ni very good strategist, ilipojitokeza fursa ya mtafaruku wa CUF, Zitto akaona fursa, akachangamkia fursa, akawameza, sasa nguvu ya ACT Wazalendo ni Zanzibar.

P
Babu ,hongera Kwa kumjbia zito na Act wazalendo vizuri

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Chama cha ACT Wazalendo kilijijengea jina kwa kusimama juu ya masuala muhimu na makubwa. Kilitoa chambuzi nyingi juu ya uchumi, hali ya kisiasa na mambo ya uongozi

Hata hivyo chama hicho kimegeuka bubu kwenye suala la Bandari. Chama kimeshindwa kutoa msiamamo wa chama katika suala hilo nyeti. Tunachosikia ni kauli binafsi za kiongozi mmoja mmoja na baadhi ya kauli hizo ziko "out of touch" na msimamo wa Wananchi katika suala hili.

1. Zitto asema mkataba huu wa IGA ni kama karatasi la kufungia vitumbua
Wakati, Wasomi wazito kwenye nchi hii wakionyesha matatizo makubwa ya mkataba huu, Wasomi wa sheria wa TLS, Profesa Shivji, Dr Nshala na wasomi wengine wa sheria , Kioingozi wa ACT Wazalendo ndugu Zitto yeye haoni kuwa huo mkataba ni hatari kwa mustakbali wa nchi yetu, Yeye anasema huo mkataba ni sawa na karatasi la kufungia vitumbua tu. Kauli hii imewashangaza wengi waliokuwa wakimuona Zitto ni mtu serious

2. Ukimya huu wa ACT unaonyesha dhahiri kuwa ACT ni chama cha kutetea maslahi ya Wazanzibari zaidi kuliko Watanganyika
Ukiwasikiliza viongozi wa ACT Wazalendo kuanzia kwa Zitto, Akina Mzee Duni, Jussa, Abdu Nondo, huwa ni wepesi sana kuonyesha madhila ambayo Zanzibar inapata katika muungano, lakini huwa hawajisumbui kuzungumza madhila ambayo Tanganyika inapata katika huu muungano.

Angalau Wazanzibari wa ACT ningewalewa, lakini Viongozi hawa wa kutoka Tanganyika ndani ya ACT wamegeuka kuwa bootlickers wa camp ya Wazanzibari ndani ya chama. Hawana Interest na mustakbali wa Tanganyika, wao wamegeuka kasuku wa kuimba madhila ya Wazanzibari ndani ya chama.

Pengine kwa sababu Ruzuku ya Chama inatoka Zanzibar ndiyo maana inabidi wamtumikie "Kafiri" wapate mradi wao. Lakini hii maana yake ni kwamba wanaonekana mbele ya umma kuwa hawa siyo wanasiasa wa kitaifa kama wanavyojaribu kujiportray bali ni special interest group.

3. Ukimya wa ACT unalenga kumnusuru Samia
Tunaambiwa Zitto yuko karibu sana na Samia, Tunaambiwa Juma Duni ni rafiki wa Samia. Urafiki na Ukaribu wa watu hao kwa raisi umekiteka nyara chama hicho kuacha kukosoa makosa makubwa kabisa anayofanya Samia kwa mustakbali wa nchi.

Matokeo yake hawa wamekigeuza chama kama Mercinery wa kisiasa. Yaani kukitumia chama kama conduit ya kumsaidia Samia kutawala smoothly licha ya makosa makubwa ya kiuonglzi hata ya kisiasa ambayo Samia anafanya. Hali hii imekigharimu sana chama cha ACT Wazalendo kuaminika na kuonekana kuwa ni chama serious chenye nia ya kuiondoa CCM madarakani.

4. CHADEMA wanakisulubu sana chama cha ACT mbele ya wananchi kwa hoja ya bandari
Kwenye ziara ambazo Chadema wanafanya nchi nzima, bila ya kutaja jina la chama chochote, wamekuwa wakiwaambia wananchi kuwa hakuna chama kilichobeba ajenda ya kutetea bandari zetu isipokuwa Chadema.

Message hii imekuwa ikiresonate ipasavyo kwa wananchi kiasi cha kujenga imani kubwa kwa chama hicho kwa kuamini kuwa ni chama kinachobeba ajenda kubwa. ACT itakuwa ni vigumu sana kupenetrate kwa wananchi kwa kupuuza ajenda nzito kama hii kisa tu ya urafiki wa Zitto na Duni Haji kwa Samia.

5. Watanganyika waanza kuamini kuwa ACT ni chama cha Wazanzibari
Kitendo cha Juma Duni kutoa kauli za kumtetea Samia kuhusuiana na udalali huu wa bandari zetu, na Kitendo cha Jussa kusema kuwa ishu ya bandari ni ya Watanganyika na watajijua wenyewe.

Huku viongozi watanganyika ndani ya chama hicho kudogosha ubovu wa mkataba huu. Kinawafanya Watanganyika waone kuwa hicho chama si chao, bali ni chama cha Wazanzibari, kwa ajili ya Wazanzibari na kwamba hawa viongozi wa Tanganyika ni front face to ya kumask Lengo halisi la chama hicho.

Mwisho:
Hiki chama cha ACT kilianza vizuri, lakini sasa kinapoteza muelekeo. Kimeshindwa kuwa fair kwenye kutetea pande zote mbili za muungano, bali kimeegemea kuisemea Zanzibar zaidi, wakati na Watanganyika kuna mambo wanayanung'unikia.

Pili uswahiba binafsi wa viongozi wake kwa watawala, umetia ukungu utendaji wa chama hicho kupigia kelele makosa makubwa ya kiuongozi yanayofanywa na watawala nchini.

Kwa muktadha huu nakiona hiki Chama kikiendelea kuwa Chombo cha Uchaguzi zaidi hasa huko Zanzibar badala ya kuwa chombo cha kuwa serikali mbadala nchini chenye kusimamia mambo makubwa kama ambavyo wakti kinaanzishwa kiliahidi au kiujipambanua kufanya.
ACT ni sehemu ya SUK huko Zanzibar, lazima wacheze hii ngoma kwa umakini hasa ukizingatia upande wa Zanzibar ndani ya Act ndio wenye nguvu ndio maana unawaona kama wameegemea zaidi huko.

Kuhusu mkataba wa bandari mpaka tutakapoona msimamo wa Act kama chama kuhusu IGA ndio tunaweza kutoa mjumuisho Ila kwa sasa sio sawa kufanya hivyo.

JokaKuu zitto junior Kalamu Pascal Mayalla Nguruvi3
Mag3 Tindo
 
waAfrika wana laana, hawajawahi kuwa siriaz na mambo yao. ni ujinga ujinga tu!

Jesus is Lord
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza nikupongeze kwa bandiko hili kwasababu watu wenye uwezo wa kufanya analysis kama hizi humu JF, wanahesabika, big up sana kwa hili and keep it up, mabandiko kama haya yanaiheshimisha jf. Pili naunga mkono baadhi ya hoja.

Hivi ndivyo vyama serious vinavyotakiwa kufanya, this is a sign of maturity!. Chama mature, kunapotokea jambo lolote kubwa la chama kutoa kauli ya chama, chama kitakutana to deliberate on the issue, ndipo kinatoa kauli ya chama, kama walivyofanya CCM.

ACT Wazalendo hawajafanya kikao chochote kujadili issue ya Bandari kwasababu ACT Wazalendo sio chama cha matukio!.

Huu ni ukomavu, chama serious hakikurupuki kutoa kauli za chama wala hakilazimiki kufuata mkumbo, kimewapa viongozi wake demokrasia ya uhuru wa maoni yao binafsi, this is very healthy kwenye freedom of expression.

Ni kweli mkataba huu wa DPW na Bandari zetu una. matatizo makubwa ya kisheria

Sio lazima maoni ya kila mtu yafanane, hivyo Zitto Kabwe hajaiona hiyo hatari

Yeye ameona huo mkataba ni karatasi ya kufungia vitumbua,

Sii kweli, labda kwa watu wasiomjua Zitto, lakini wanaomjua wanamjua Zitto ni very serious leader.

Hapa naomba niheshimu tuu mawazo yako japo sikubaliani nawe

Hii ni kitu mpya kwa siasa za Tanzania, inaitwa strategic politicking

duh...!

Sii kweli

Hili neno!.

Hili neno!

Naunga mkono hoja, ACT Wazalendo kilipoanzishwa kilianza vizuri, na mimi nililizungumzia Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza kiukweli Zitto ni very good strategist, ilipojitokeza fursa ya mtafaruku wa CUF, Zitto akaona fursa, akachangamkia fursa, akawameza, sasa nguvu ya ACT Wazalendo ni Zanzibar.

P
umemaliza vizuri 'nguvu ya chama cha ACT ni Zanzibar' kwa hiyo jamaa yupo sahihi kusema ACT ipo kwa ajili ya kuwatetea wazanzibar
 
kitendo cha Juma Duni kusema masuala ya vyama si ya muungano ana maanisha nini? kila upande uwe na chama chake na kuwa ACT haikupaswa iwe ya kitaifa!
 
Chama cha ACT Wazalendo kilijijengea jina kwa kusimama juu ya masuala muhimu na makubwa. Kilitoa chambuzi nyingi juu ya uchumi, hali ya kisiasa na mambo ya uongozi

Hata hivyo chama hicho kimegeuka bubu kwenye suala la Bandari. Chama kimeshindwa kutoa msiamamo wa chama katika suala hilo nyeti. Tunachosikia ni kauli binafsi za kiongozi mmoja mmoja na baadhi ya kauli hizo ziko "out of touch" na msimamo wa Wananchi katika suala hili.

1. Zitto asema mkataba huu wa IGA ni kama karatasi la kufungia vitumbua
Wakati, Wasomi wazito kwenye nchi hii wakionyesha matatizo makubwa ya mkataba huu, Wasomi wa sheria wa TLS, Profesa Shivji, Dr Nshala na wasomi wengine wa sheria , Kioingozi wa ACT Wazalendo ndugu Zitto yeye haoni kuwa huo mkataba ni hatari kwa mustakbali wa nchi yetu, Yeye anasema huo mkataba ni sawa na karatasi la kufungia vitumbua tu. Kauli hii imewashangaza wengi waliokuwa wakimuona Zitto ni mtu serious

2. Ukimya huu wa ACT unaonyesha dhahiri kuwa ACT ni chama cha kutetea maslahi ya Wazanzibari zaidi kuliko Watanganyika
Ukiwasikiliza viongozi wa ACT Wazalendo kuanzia kwa Zitto, Akina Mzee Duni, Jussa, Abdu Nondo, huwa ni wepesi sana kuonyesha madhila ambayo Zanzibar inapata katika muungano, lakini huwa hawajisumbui kuzungumza madhila ambayo Tanganyika inapata katika huu muungano.

Angalau Wazanzibari wa ACT ningewalewa, lakini Viongozi hawa wa kutoka Tanganyika ndani ya ACT wamegeuka kuwa bootlickers wa camp ya Wazanzibari ndani ya chama. Hawana Interest na mustakbali wa Tanganyika, wao wamegeuka kasuku wa kuimba madhila ya Wazanzibari ndani ya chama.

Pengine kwa sababu Ruzuku ya Chama inatoka Zanzibar ndiyo maana inabidi wamtumikie "Kafiri" wapate mradi wao. Lakini hii maana yake ni kwamba wanaonekana mbele ya umma kuwa hawa siyo wanasiasa wa kitaifa kama wanavyojaribu kujiportray bali ni special interest group.

3. Ukimya wa ACT unalenga kumnusuru Samia
Tunaambiwa Zitto yuko karibu sana na Samia, Tunaambiwa Juma Duni ni rafiki wa Samia. Urafiki na Ukaribu wa watu hao kwa raisi umekiteka nyara chama hicho kuacha kukosoa makosa makubwa kabisa anayofanya Samia kwa mustakbali wa nchi.

Matokeo yake hawa wamekigeuza chama kama Mercinery wa kisiasa. Yaani kukitumia chama kama conduit ya kumsaidia Samia kutawala smoothly licha ya makosa makubwa ya kiuonglzi hata ya kisiasa ambayo Samia anafanya. Hali hii imekigharimu sana chama cha ACT Wazalendo kuaminika na kuonekana kuwa ni chama serious chenye nia ya kuiondoa CCM madarakani.

4. CHADEMA wanakisulubu sana chama cha ACT mbele ya wananchi kwa hoja ya bandari
Kwenye ziara ambazo Chadema wanafanya nchi nzima, bila ya kutaja jina la chama chochote, wamekuwa wakiwaambia wananchi kuwa hakuna chama kilichobeba ajenda ya kutetea bandari zetu isipokuwa Chadema.

Message hii imekuwa ikiresonate ipasavyo kwa wananchi kiasi cha kujenga imani kubwa kwa chama hicho kwa kuamini kuwa ni chama kinachobeba ajenda kubwa. ACT itakuwa ni vigumu sana kupenetrate kwa wananchi kwa kupuuza ajenda nzito kama hii kisa tu ya urafiki wa Zitto na Duni Haji kwa Samia.

5. Watanganyika waanza kuamini kuwa ACT ni chama cha Wazanzibari
Kitendo cha Juma Duni kutoa kauli za kumtetea Samia kuhusuiana na udalali huu wa bandari zetu, na Kitendo cha Jussa kusema kuwa ishu ya bandari ni ya Watanganyika na watajijua wenyewe.

Huku viongozi watanganyika ndani ya chama hicho kudogosha ubovu wa mkataba huu. Kinawafanya Watanganyika waone kuwa hicho chama si chao, bali ni chama cha Wazanzibari, kwa ajili ya Wazanzibari na kwamba hawa viongozi wa Tanganyika ni front face to ya kumask Lengo halisi la chama hicho.

Mwisho:
Hiki chama cha ACT kilianza vizuri, lakini sasa kinapoteza muelekeo. Kimeshindwa kuwa fair kwenye kutetea pande zote mbili za muungano, bali kimeegemea kuisemea Zanzibar zaidi, wakati na Watanganyika kuna mambo wanayanung'unikia.

Pili uswahiba binafsi wa viongozi wake kwa watawala, umetia ukungu utendaji wa chama hicho kupigia kelele makosa makubwa ya kiuongozi yanayofanywa na watawala nchini.

Kwa muktadha huu nakiona hiki Chama kikiendelea kuwa Chombo cha Uchaguzi zaidi hasa huko Zanzibar badala ya kuwa chombo cha kuwa serikali mbadala nchini chenye kusimamia mambo makubwa kama ambavyo wakti kinaanzishwa kiliahidi au kiujipambanua kufanya.
ACT NI CCM B ITAPINGAJE?
 
Ha
Ajabu ni kwamba,pamoja na kelele mingi za cdm,watanzania wengi ,wanawaona useless, wengi wanaona ACT,ndipo mahala sahihi,
N.b,Ndimi za kutukana,kudhalilisha,kufedhehesha,zinashabikiwa tu na wavuta bangi na wenye upungufu wa akili,wenye akili zao timamu wanatulia na Ku digest.
Hao watanzania wengi umewaona wapi au ni wewe na familia yako tu
 
ACT ni sehemu ya SUK huko Zanzibar, lazima wacheze hii ngoma kwa umakini hasa ukizingatia upande wa Zanzibar ndani ya Act ndio wenye nguvu ndio maana unawaona kama wameegemea zaidi huko.

Kuhusu mkataba wa bandari mpaka tutakapoona msimamo wa Act kama chama kuhusu IGA ndio tunaweza kutoa mjumuisho Ila kwa sasa sio sawa kufanya hivyo.

JokaKuu zitto junior Kalamu Pascal Mayalla Nguruvi3
Mag3 Tindo
Kwa sababu Hii basi ni utumwa kwa viongozi wa bara kuzungumzia masuala yenye maslahi na Tanganyika.
 
Ajabu ni kwamba,pamoja na kelele mingi za cdm,watanzania wengi ,wanawaona useless, wengi wanaona ACT,ndipo mahala sahihi,
N.b,Ndimi za kutukana,kudhalilisha,kufedhehesha,zinashabikiwa tu na wavuta bangi na wenye upungufu wa akili,wenye akili zao timamu wanatulia na Ku digest.
akili timamu mnauza bandar ni mazezeta pekee ndio mtayapata huko ccm na ccm B, ndio maana mkutano wenu pale kirumba ulibuma pamoja na gharama za kusomba watu hadi Geita,busega,bariadi na kwingineko, na jana pale Geita mjini tumewasulubu mpaka sasa mmepata insanity hamuamin nguruwe nyinyi.
 
Zitto mwanzoni kabisa alishasema hatampinga Samia, na hiyo ni kawaida yake, hata enzi za JK alikuwa kimya hivyo hivyo, akawa anadai JK ni kama baba yake, hivyo labda na sasa Samia atakuwa sawa na mama yake pia.

Zaidi ya hapo, ACT kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na CCM kule Zanzibar kumewafanya wawe kama nyumba ndogo ya CCM, huu ndio ukweli.

Wanajua hawawezi kufurukuta kuwapinga CCM kwa lolote, kisha madai yao yakapewa uzito. Tabia ya Zitto kujikomba kwa viongozi wa CCM, inamshushia heshima yeye binafsi na chama chake, na zaidi, inawapunguzia umaarufu, watanzania sio wajinga.

Mfano kule Zanzibar, wakati ACT walipopinga uteuzi wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hakuna chochote CCM walichofanya ili kuyashughulikia yale madai yao, na wao ACT bado wako kimya mpaka leo, ni kama vile wameshakubali matokeo, sasa chama cha namna hii kitaheshimika vipi?
Hayo ni maoni yako na mawazo yako lakini ukweli haiko hivo Hao ACT mikutano yao yote huku zanzibar wanaikosoa CCM tena kwa sana tu
 
kitendo cha Juma Duni kusema masuala ya vyama si ya muungano ana maanisha nini? kila upande uwe na chama chake na kuwa ACT haikupaswa iwe ya kitaifa!
Hiyo ni tafsiri yako wewe huyo babu juma duni amesema masuala ya vyama vya siasa hayamo katika Mkataba wa Muungano
 
akili timamu mnauza bandar ni mazezeta pekee ndio mtayapata huko ccm na ccm B, ndio maana mkutano wenu pale kirumba ulibuma pamoja na gharama za kusomba watu hadi Geita,busega,bariadi na kwingineko, na jana pale Geita mjini tumewasulubu mpaka sasa mmepata insanity hamuamin nguruwe nyinyi.
Unakuwa kama unaugeni na watanzania weye, watanzania wape habari za kulaumu,kunungunika,kuchambana na mipasho,WATAJAA LUKUKI HAPO.
 
Mkuu umeweza kupotosha umma,

ACT ilitoa msimamo wake kuhusu suala la bandari mapema sana, tena waliotoa kisomi zaidi tofaut na CHADEMA wanaoropoka tu kila siku bila kuja na suluhisho la ufanisi wa bandari,

ACT walisema iundwe kampuni moja ambayo DP world watakuwa na share, Serikali itakuwa na share na share nyingine ziwekwe DSE, kisha kampuni hio ndio isimamie bandari,

Sijui CHADEMA wao mapendekezo yao ni yapi zaidi ya kuwa Pinga Pinga FC
 
Ajabu ni kwamba,pamoja na kelele mingi za cdm,watanzania wengi ,wanawaona useless, wengi wanaona ACT,ndipo mahala sahihi,
N.b,Ndimi za kutukana,kudhalilisha,kufedhehesha,zinashabikiwa tu na wavuta bangi na wenye upungufu wa akili,wenye akili zao timamu wanatulia na Ku digest.
Wewe ndio mburula kabisa. Kigezo gani umetumia kugundua ACT inakubalika zaidi bara kuliko CDM? MBWA WEWE
 
..Ccm iko madarakani hivyo inatakiwa iwe na majibu.

..chama tawala kutegemea kupewa majibu na chama cha upinzani ni dalili ya uvivu, na uchovu wa fikra.
Kwani walioko madarakani ndio Wana akili kuliko wengine?
 
Hiyo mi ACT si miisiramu tu hiyo.
 
Tatizo huwezi kuungana na walevi na waliougua maleria na sasa wananchi wengi wameanza kuiona picha halisi ya uongozi wa Chadema .

Ngazi kuu ya chadema ni madicteta na siku wakifanikisha kuichukua nchi hii wananchi watasaga meno.ila nashangaa hadi leo wameshindwa kuwarudisha wanawake waliorubuniwa bungeni ,mtakuja kuweza kuuzuia Mkataba wa bandari,subutuu.
Endeleeni na ndoto zenu za mchana aka day dreams.
 
Back
Top Bottom