zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Ni kweli Mbowe anaweza kuwa na madhaifu ila ndio ameifikisha Chadema hapo ilipo so kuanzia kumlaumu kwa ofisi wakati alikua muasisi enzi hizo anatumia magari binafsi kujenga chama naona kama tuna downplay sacrifice yake!! Hivi unakumbuka Yale ma Pick up ya M4C? zaidi ya 20 yalinunuliwa ila sijawahi ona akipongezwa humu ilihali yalisaidia sana tokea enzi zile za Operation Sangara.Mkuu uko sahihi sana, mimi ninaposhikilia kuwa Mbowe asiendelee kuwa mwenyekiti wa CDM tena baada ya kipindi kirefu hivyo, huwa ni mambo kama haya. CDM ilipaswa kuwa na ofisi yenye hadhi ya chama hicho, na sio hicho kinachoendelea hapo. Pitia viongozi wote wa CDM wa ngazi za juu toka 2010, aina ya majengo yao binafsi waliyojenga, na hadhi ya hiyo ofisi yao.
Kuna nyuzi zaidi ya moja huku jukwaani kuhusu ujenzi wa ofisi ya CDM. Niliwahi kusema tena zaidi ya mara moja kuwa CDM wangeweza kutenga 500m -1b wakawa na ofisi yenye ghorofa zaidi ya 2, jengo ambalo lingekuwa hadi na kumbi za kubeba watu 500 kwa wakati mmoja. Je ni kweli CDM ilikosa hizo 500m-1b muda wa hii miaka 10 iliyopita?
Kingine Chadema inaamini katika ugatuzi, so nguvu kubwa iliwekwa kwenye ofisi za Kanda na wewe ni shahidi karibu Kanda zote Kuna ofisi nzuri na kubwa za Chadema so strategy ilikua wakimaliza ugatuzi warudi makao makuu.
So nikijibu hoja Yako, pesa hazikukosekana ila kipaumbele ilikua kuimarisha chama kwenye grassroots hasa level ya Kanda.
Kuhusu ufisadi sio kweli CAG ameshakagua mara ngapi sijaona wakimkamata afisa yeyote wa Chadema kwa wizi! In fact JPM alivokua na kisasi unadhani asingempa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuiba pesa ya Chadema?
Mnyika kaahidi ofisi kubwa kujengwa so tumpe muda kama alivyosema na ata deliver