Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu akizungumza na wanahabari leo, Alhamisi Oktoba 10.2024, Dar es Salaam amesema kuwa mawakala wanalazimishwa kufika kwenye ofisi za Halmashauri husika ili kuapa suala ambalo wengi hushindwa kutokana na umbali uliopo kati ya Halmashauri na maeneo wanayotoka
"Kuapishwaji wa mawakala wa undikishaji wapiga kura (kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa), tumepokea taarifa katika maeneo mengi kwamba wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri wameitisha zoezi la viapo vya mawakala kufanyika katika ofisi za Halmashauri husika, kwa jiografia ya nchi yetu, maeneo mengi yako mbali na Halmashauri, hivyo ni ngumu kwa mawakala kufika kwa ajili ya viapo, utaratibu huo utawaacha mawakala bila viapo na ikiwa hawataapishwa maana yake hawatakuwa na sifa za kusimamia zoezi la uandikishaji"
"Newala, kule viongozi wetu wa chama (ACT Wazalendo) wametakiwa kuwapeleka mawakala wote Newala mjini kwenda kuapishwa ambapo baadhi ya maeneo yana zaidi ya Kilometa 70 mfano yale yanayopakana na Msumbiji"

LIVE : WANAOPINGA TAMISEMI KUSIMAMIA UCHAGUZI WAIBUA MAPYA / WAHOJI UKIMYA WA WANANCHI 'KESI YAO'